matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Sikukuu hii imekuwepo kabla ya kuhusishwa na Ukristo. Inasemekana ili ukristo ujivunie waumini ilibidi waiingize kwenye dini na kuihusisha na Yesu. Matokeo yake wazungu wengi wasio na dini walivutwa.
Mimi ni mkristo, ila siichukulii siriasi licha ya huhusiswa na Yesu. Naichukulia kama Zile sikukiu za kijadi za mavuno ambazo watu vijijini hununua nguo mpya, kunywa soda nyingi, kula vitumbua na maandazi (hasa usukumani) na kula biskuti.
Kama tunakuwa na hamasa kubwa katika tamaduni na jadi za kizungu, basi tusisahau kuhudhuria na sikukuu zetu za kijadi vijijini kwetu. Tujifunze kupenda na vya kwetu kwa uzito uleule tunaopenda za kigeni.
Mfano. Denmark ni nchi inayoongoza kwa watu wengi ambao hawaamini uwepo wa Mungu na mambo ya dini, llakini ikifika sikukuu hii karibu wote wanasherekea maana historia inaonyesha kwenye utamaduni wao wa zamani kabla ya ukristo hizo sherehe zilikuwepo.
Kama waarabu walivyosambaza jadi na tamaduni zao kupitia dini, wazungu nao walipopokea ukristo kutoka kwa Wayahudi waliugeuza fursa ya kupenyezea jadi zao.
Ni hayo tu.
Ni vizuri ukifanya mambo ukiwa namaarifa mapana
Sikukuu njema
Mtumishi Matunduizi.