Nimekuwa kwenye fani ya ualimu kwa muda mrefu sasa, moja ya vitu nilivyogundua (baada ya research) ni kuwa walimu wazuri ni wale waliosomea diploma ya ualimu, wakaenda makazini, au makazini then chuo kikuu. Sababu ni
1. Wanajua teaching strategies zaidi ya ambao wameunganisha chuo kikuu.
2. Wanajituma kazini zaidi
3. Wanajua matumizi ya lugha nyepesi na inayoeleweka kwa wanafunzi.
4. Wana manage discipline ya darasa vyema
5. Wanapenda kujifunza mambo mapya
Nimepitia maisha ya ualimu ivyo nayajua vizuri,anidanganyi mtu...
unajua kuna tofauti kubwa kati ya mwalimu wa diploma na wa degree,haswa kisaikolojia na ufahamu wa vile vitu anavyofundisha...
Walimu wa degree wanajua sana vitu,na pia wanajiamini,wanajitambua,wanaumiza vichwa usiku na mchana kutafuta maslai zaidi..
Walimu wa diploma ni wanyenyekevu kupita kiasi,wamelidhika na maisha na wako shalo vibaya kichwani..
Pia wa dip wanapenda sana vyeo ata kama havina faida yoyote,ndio maana utawaona ful kujipendekeza kwa ma afisa elimu..wanawapelekeaga vitunguu,kuku,nyanya,matunda yote ni kujaribu kukumbukwa kwenye ufalme.
Ni kama mtoa mada alivyokuja kupunguza stress zake hapa!
ndio tatizo lenu walimu wa diploma,mnafikiri mwalimu lazima uvae kishambashamba ndio haiba...mwalimu akivaa kileo basi mnamwita sharobaro.
Nimepitia ualimu na nilikuwa wa degree,unakutana na ticha wa dip kavaa shati la zambarau,tai ya kijani,suruali ya njano ina vidraft vyeupe alafu inamarinda kibao,kiatu brown''asante mchaga'',booonge la mkanda kiunoni,muda wote anatema jasho...sasa akikutana na mwalimu kavaa shati zuri e.g levis,suruali kadeti,kiatu ngozi safi e.g gucci ,ananukia vizuri,akiwa ofisini mara kafungua laptop mara kaingia bbm...hapo utakuta ticha wa diploma anakujengea bifu staff ukimuuliza kisa nini eti oooh uyu jamaa analinga sana kwa ajili ana degree,anajifanya sharobalo...
pinga kwa hoja mkuu!