Nyakageni
JF-Expert Member
- Feb 1, 2011
- 15,045
- 5,108
- Thread starter
- #61
Hao walimu watakuwa bora kwa vigezo vyako kama watabaki na diploma zao ila wakienda kusoma degree wakirudi watakuwa na vigezo sawa na waliounganisha degree bila kupita diploma. Sababu kubwa wa dip. wanafundishwa sana utii 'ndiyo mzee' kuliko kuhoji (nadhani) na hawaoni future nyingine zaidi ya ualimu na hutenda kazi kwa bidii wakiwaza kufikiriwa kwenye vyeo vya ngazi ya shule ambavyo wa degree huwa haviwazii sana. Nasema hawahoji mfano nshawahi kufanya field chuo cha ualimu Songea kwanza nkagundua wimbo wa chuo wanaouimba kila j'tatu ulikuwa na baadhi ya mistari inayomalizikia "ualimu ni witooo" sa unategemea akienda kazini atahoji chochote. Pia nilikuta walimu vijana wenye degree pale wako busy na mambo yao (kazi za nje) ya kuongeza kipato mfano wengine wanapiga dili hadi open university na hao wenye dip. ndo wengi walikuwa wamekamata vyeovyeo vya idara na wanaonesha kuridhika. Mambo mengi sana yanawafanya wa diploma wawe walimu 'haswa'.
ukubali ukatae, ualimu lazima uwe na wito. Weka siasa pembeni HAKI NA WAJIBU