Mtazamo wangu: Walimu wa diploma ni bora kuliko ambao hawajapitia diploma wakapata degree

@Nyakageni, nimesema wengi na bado nasimama kwenye point yangu. Wengi wao hata hawana sifa ulizotaja kama mshauri,mnasihi, kiongozi nk. Hao niliotaja hapo juu kwangu ni the best angalau hawakusomea ualimu.Wana sifa zote kuanzia kufundisha mpaka sifa ulizotaja wewe. NAONGEZA WENGINE AMBAO KWANGU NITAWAKUMBUKA, NA HAWA NI WALIMU WLIOSOMEA,WANA SHAHADA HAWA; MKANDAWILE MWALIMU WA KEMIA, ALIWAHI FUNDISHA PUGU BAADAE LOLOYA, BUSANJI ALIKUWA PUGU AKAENDA MAKONGO. HAO NI MIONGONI MWA WALIMU WACHACHE SANA, NAJUA WAPO WENGI WAZURI LAKINI RATIO YA WAZURI NI NDOGO SANA 0.00000000000000001.WENGI WALIKIMBILIA HUKU BAADA YA KUONA SEHEMU NYINGINE HAWAEZI KWENDA.
 
@foundation, nimekuelewa mkuu. Hii profession imedharaulika sana
 
Ualimu ni wito....wapo wafanyao kama kazi,hao wamepata ujira wao lakini hii haiondoi ukweli kwamba ualimu ni wito na sisi tumeitikia
 
upo sahihi kabisa ni kwamba mwalimu mzuri ni yule aliyeanzia primary kafundisha then akaenda diploma akarudi kufundisha ndipo akaenda kusoma degree na baadae elimu ya juu zaidi ya hiyo huyo anaweza kua mwalimu mzuri sana
 
MWL wa degree ni noma bana tukubaliane! Elim ku-define, na kumention! Its all about being libereted, kuonesha jamii usahihi, kutokuwa muoga dhidi ya ubonyezaji, na kuwambia watu facts. Na siyo kuva suruali za vitambaa na kupandisha mayeno na kusema muabudu badala ya mtiifu wa mamlaka. Alafu hawa ndio wagum kwel kugoma hata hakizao zikizikwa zikiwa hai. Oh mi basi bana.
 
Walimu wa dip wamezoea kutawaliwa! Hivyo mi cdhani ni cfa nzuri ya mwl. Mwl anatakiwa awe mbishi lakini kimantikia. Hawa wa dip wakisikia mgomo wa CWT huwaga wana-let down sana. Mi hawanifurahishi sana.
 
Ualimu ni wito....wapo wafanyao kama kazi,hao wamepata ujira wao lakini hii haiondoi ukweli kwamba ualimu ni wito na sisi tumeitikia

maneno yako kama ya wimbo wa chuo cha ualimu butimba. Kudos mkuu
 
MWL wa degree ni noma bana tukubaliane! Elim ku-define, na kumention! Its all about being libereted, kuonesha jamii usahihi, kutokuwa muoga dhidi ya ubonyezaji, na kuwambia watu facts. Na siyo kuva suruali za vitambaa na kupandisha mayeno na kusema muabudu badala ya mtiifu wa mamlaka. Alafu hawa ndio wagum kwel kugoma hata hakizao zikizikwa zikiwa hai. Oh mi basi bana.

kaka acha siasa kwenye taaluma. Rudi kwenye mada. Acha uanaharakati, zungumzia teaching na siyo extra curricular activities
 
Walimu wa dip wamezoea kutawaliwa! Hivyo mi cdhani ni cfa nzuri ya mwl. Mwl anatakiwa awe mbishi lakini kimantikia. Hawa wa dip wakisikia mgomo wa CWT huwaga wana-let down sana. Mi hawanifurahishi sana.

mkuu umefanya utafiti?
 
Nadhani hatumtendei haki mtoa uzi, kwa kudivert kwenye hoja! Ni ukweli usiopingika kuwa kumwandaa mwalimu bora ni mchakato{process} na si ku pick-up watu wenye grade flani la ufaulu na kuwapa mafunzo flanflani then unawaita walimu! Mwl aliyepitia Dip na badae Degree ni bora elfu mara elfu katika upande wa 'ualimu' nikiwa na maana ya mbinu za ufundishaji, malezi na haiba kwa ujumla wake. Lakini hawa wa moja kwa moja ni wazuri zaidi katika eneo moja la kontenti tu! Fanya utafiti utagundua. Na ualimu ni zaidi ya kufundisha,unavuka kingo hizo, kama mwl unatakiwa mwanafunzi akufurahie si tu darasani bali hata katika mambo mengine ambapo atakuamini, na hivyo unaweya kumpa mwangaza katika mambo mbali2 kwa faida ya ukuaji wake ktk domain zote, katika haya walm wa moja kwa moja wanakosa sifa hzi. University wanafundishwa how to teach, bt Diploma wana emphasize how to become A GOOD TEACHER.
 
Walimu wa dip wamezoea kutawaliwa! Hivyo mi cdhani ni cfa nzuri ya mwl. Mwl anatakiwa awe mbishi lakini kimantikia. Hawa wa dip wakisikia mgomo wa CWT huwaga wana-let down sana. Mi hawanifurahishi sana.

Yani walimu na raia karibia wote tunaumwa "siasamgomophobia" yani kila kitu tunawaza migomo na kupolitisaizi kila jambo. Fikiri kidogo; Je walimu wakipewa vyooote wanavyo demand, no more migomo/migogoro, yupi ni mwl bora kati ya yule aliyepitia Dip then aka graduate na yule aliyegraduate bila kupitia Dip? NIJIBU MKUU USIONE HAYA.
 
Nadhani hatumtendei haki mtoa uzi, kwa kudivert kwenye hoja! Ni ukweli usiopingika kuwa kumwandaa mwalimu bora ni mchakato{process} na si ku pick-up watu wenye grade flani la ufaulu na kuwapa mafunzo flanflani then unawaita walimu! Mwl aliyepitia Dip na badae Degree ni bora elfu mara elfu katika upande wa 'ualimu' nikiwa na maana ya mbinu za ufundishaji, malezi na haiba kwa ujumla wake. Lakini hawa wa moja kwa moja ni wazuri zaidi katika eneo moja la kontenti tu! Fanya utafiti utagundua. Na ualimu ni zaidi ya kufundisha,unavuka kingo hizo, kama mwl unatakiwa mwanafunzi akufurahie si tu darasani bali hata katika mambo mengine ambapo atakuamini, na hivyo unaweya kumpa mwangaza katika mambo mbali2 kwa faida ya ukuaji wake ktk domain zote, katika haya walm wa moja kwa moja wanakosa sifa hzi. University wanafundishwa how to teach, bt Diploma wana emphasize how to become A GOOD TEACHER.

salute kwako mkuu! Content iko kichwani lakini je inamfikiaje mtoto ndo wengi wao wanashindwa. Kudos
 
tuna tatizo la msingi kwenye vyuo vikuu vyetu

Sina uakika kama tatizo ni vyuo vikuu ama serikali. Mwanafunzi anaenda chuo kikuu mahala ambako yuko huru kwenda darasani kuhudhuria mjarabu au kujisomea jioni ?preparation. Kwa uhuru huo hana muda wakujisomea ifikapo siku ya test au university examination anaingia na nondo au desa anatazamia ili aweze kupata marksi ya juu katika mtihani huo.

Pili wasimamizi nao wanachangia sana unakuta wanafunzi hadi wanajadili kabisa wakati wako kwenye mtihani lakini hakuna hatua wanazowachukulia. Ukiongea nao (wasimamizi) wanasema wanakatishwa tamaa na wakuu wao ambao wao wakipelekewa kesi hizo huwaachia wanafunzi hao. Unategemea wahitimu wa shahada wakaenda kufundisha vizuri?
 
Kila kitu bongo ni kibovu isipokuwa ubovu wenyewe ndo upo high quality!!
 
ni kweli kabisa, mwalimu wa diploma anjiamini na anaelewa mwanafunzi anahitaji nini, kwa kifupi anamsoma mwanafunzi kama darubini. Hawa wa degree moja kwa moja huwa ni wabovu sana kumsoma mwanafunzi na pia wawapo darasani wengi wao huwa hawajiamini
 
ahsante kwa uchambuzi wako
 
Back
Top Bottom