Mtego Muhimu kwa Kocha wa Simba SC Pablo ambaye pia anatakiwa sana na Orlando Pirates FC wasio na Kocha Mkuu kwa sasa

Mtego Muhimu kwa Kocha wa Simba SC Pablo ambaye pia anatakiwa sana na Orlando Pirates FC wasio na Kocha Mkuu kwa sasa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Akiivusha Simba SC kwenda Nusu Fainali ya CAFCC dhidi ya Orlando Pirates FC atakuwa ameponya Kufukuzwa (kuwa Sacked) Msimbazi, ila tayari Matajiri wa Orlando Pirates FC nao wameshampa Ofa (tena Kubwa tu) kama akikubali kutua Kwao muda wowote kuanzia sasa.

GENTAMYCINE ningekuwa ndiyo Kocha Pablo Franco Martin kwa Hadhi ya Ligi Kuu ya South Africa, Uweledi wake, Utajiri wao na hata Mazingira yake wala nisingepoteza muda na Waswahili ambao kila mara tu (kila Siku) wananitishia Kunifukuza na wananifanya nifanye Kazi yangu kwa Presha Kubwa ukizingatia Michezaji yao mingi ( ya Kigeni na Wazawa ) sikuwasajili Mimi na walisajiliwa Kimipango Mipango ( Kisamjo Samjo ) tupu tu huku 10% zikitawala kwa hao Waliowaleta Klabuni.

Nikisema Mechi itakuwa Ngumu kutokana na Mazingira mengi ninayoyaona na hapo bado CEO wa Yanga SC Senzo Mazingisa Mbatha (ambaye anaijua vyema Simba SC na Michezo yake ya Nje ya Uwanja hasa kwa Timu Ngeni zinazokuja Kucheza nasi) hajawaambia Nduguze hao Siri zetu zote kama ambavyo pia alifanya kwa Kaizer Chiefs FC walipokuja Kucheza nasi mwaka Jana hamnielewi na mnanichukia huku mkidhani naichukia Simba SC wakati kumbe Kiuhalisia ni kwamba Naipenda, ila nawakosoa ili Wajitathmini, Wajipange na Wakazane kwakuwa hatua ya sasa ni ya 'Kiumeni' zaidi.
 
Nafikiri Jf ianzishe tuzo ya kuazisha nyuzi nyingi, ikifanya hivyo itawasaidia vijana kama huyu kujipatia kipato chao cha kila siku.
Wengine kwa Mapenzi makubwa tuliyonayo kwa Mtandao huu Pendwa wa JamiiForums na kwa Faida Kubwa tulizozipata kwa kuwa Mmoja wa Members wake wala hatuhitaji Tuzo kutoka Kwao sana sana labda Mimi ( Sisi ) ndiyo tunatakiwa Kujiandaa na kuwapa Tuzo JamiiForums kama Mtandao ( Kampuni ) na Mmiliki ( Mwanzilishi ) wake Maxence Melo kwa Kubuni huu Mtandao ambao wengine umetusaidia sana kutujenga Kiakili ( Kifikra ) na Kutufanya tuzidi kuwa na Maarifa mengi ambayo hata ukiwa Vyuo Vikuu huwezi kamwe kuyapata.

Long Live JamiiForums na Ibarikiwe tu.
 
Sasa huyo Senzo aliisaidia nini Kaizer chiefs walipokuja hapa mbona walikoga bao 3 bila tena walitamani mpira uishe ndani ya dakika 60 tu.

Mbinu za mchezo ni nyingi hawezi kuzijua zote. Na tangu aondoke bado Simba amechukua ubingwa wa ligi kuu, kushiriki Champions league na sasa kufikia hatua ya robo fainali shirikisho Afrika.
 
Ukimaanisha kwamba...............
Binadamu mara nyingi tuna miaka michache ya kuishi hivyo ni vyema kuacha kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavyo. Hivyo lugha za matusi si ustaarabu aachane nazo, kwani hata akifa bado watu watamuelezea kwa mtizamo wa matusi yake.
 
Binadamu mara nyingi tuna miaka michache ya kuishi hivyo ni vyema kuacha kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavyo. Hivyo lugha za matusi si ustaarabu aachane nazo, kwani hata akifa bado watu watamuelezea kwa mtizamo wa matusi yake.
Barida....!!!!!
 
Back
Top Bottom