a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 4,014
- 4,600
Eneo kubwa la tahadhari katika ujumbe huu ni mtego wa kiroho wa kukwazika au kubeba kinyongo moyoni, ambao shetani anautumia kama silaha ya siri kuzuia baraka.
Maana ya "Scandalon": Neno la Kigiriki la kukwazika (offense) ni scandalon, ambalo linamaanisha kichocheo au kifyatulio cha mtego wa mnyama unaoshikilia chambo. Kubeba kinyongo ni kuingia mwenyewe kwenye mtego wa adui.
Kuzuia Ustawi na Upambanuzi: Kinyongo kinapooza uwezo wa mtu wa kusikia sauti ya Mungu na kinazuia upambanuzi wa kiroho. Hata kama mtu ana karama kubwa, hawezi kuvuka kutoka kipindi cha upweke/majaribio kwenda kwenye kipindi cha kudhihirika kwa baraka kama hajakatisha/hajaondoa kinyongo moyoni mwake.
Kujaribiwa kwa Imani:
Mungu anaruhusu majaribu kupitia watu au mazingira ili kusafisha na kuimarisha imani ya mwamini (1 Petro 1:6-7), na si kwa ajili ya kumharibu.
Mtego halisi sio yule aliyekukwaza, bali ni kile ambacho kinyongo hicho kinatengeneza ndani ya moyo wako
yani ule uovu ama maumivu ambayo adui yako amekutendea au amekukusudia ukupate,USIAMUE jinsi wewe utakavyoishi,utakavyopokea.
MFANO YOSEFU alitendewa mabaya na ndugu zake walimkusudia mabaya lakini ,moyo wa Yosefu haukuweka KINYONGO juu ya ndugu zake wale waliomtendea mabaya
Mwanzo 50:20
Nanyi kweli mlinikusudia mabaya ,bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.
kama Joseph angeweka kinyongo angelipa mabaya kwa ndugu zake kumbe Mungu aliwakusudia kuwaokoa.
Ni sawa na STEPHANO alipigwa mawe na miongoni mwq waliompiga mawe alikuwepo SAULO ambaye baadae alikuja kugeuka moyo na kuwa mtu maema na kuwa PAULO..kama Saulo angweka kinyongo na kuwalaani waliomkosea angelaani mtu ambaye amebeba kusudi la Mungu.
Yesu aliwasamehe wale waliomsulubisha waliomtundika msalabani ambao ni mimi na wewe kwa dhambi zetu
Kupitia kuwaombea wale waliokuwa wanamcheka AYUBU akapona uteka wake /ugonjwa wake.
Mt 5:44
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi
BE KIND to UNKIND people they need it the most.
Apostle Miz Mzakweh Tancredi