Mtei akosoa mgombea binafsi kuruhusiwa kuwania urais

Mawazo ya Mzee Mtei tunayaheshimu. Hata hivyo, afahamu kuwa asilimia kubwa ya wapiga kura siyo wanachama wa Chama chochote cha siasa. Kwa mantiki hiyo, hawahitaji sera za chama cha siasa. Wananchi wanachotaka ni maendeleo yao na nchi kwa ujumla!
 

Kimsingi kila Mtanzania na haki ya kutoa maoni. Hebu tuliangalie hili suala la serikali za majimbo, kama kuna mtu anaielewa vema falsafa naomba aweke wazi mawazo yake tuliokuwa hatuijui tuweze kuelewa faida na hasara zake. Kwa vile hiki ndiyo kipindi cha sisi kujenga au kubomoa, ni vema mambo yote yawekwe wazi mapema kabla KATIBA hii MPYA haijaanza kutumika.
 
Wrong!! rais anachaguliwa na wananchi na anawajibika kwao tu, na siyo kwa vyama vya siasa. Haya mambo ya kamati kuu za vyama hayana maana.

Toka lini? Sasa kama Haujui ITIKADI ya CHAMA Huyo MTU akkisema yeye ni Fascist au Segregationist alisahau kuwaambia Majuwaani sababu hana chama itikadi zake zinatoka kichwani mwake wewe bado utakaa akuchinje akubague sababu tu alikupa huo UONGO wake JUKWAANI?
 
Dis agree with him kuhusu kuunda mawaziri.
Tunataka mawaziri wasitokane na bunge wala vyama vya siasa...

Kwa mantiki hii mgombea binafsi ataweza kuunda serikali.
 
Wakati ule Mtikila ameshinda kesi yake ya kutaka Mgombea binafsi NA serikali kumbania, wewe Ritz NA ndugu zako akina Malaria sugu mlikuwa mstari WA mbele sana kumpinga mgombea binafsi. Leo hii, wamemkubali mmeamua kuwa Bender

a! Duh!

naona unalazimisha watu wakubaliane na Mtei , soma signature yangu "My loyalty is to reason,and as a reasonable person I reserve the right to change my mind when presented with new information that alters my perspective"


 

Acha uongo mkuu. Nikupe mfano mmoja tu. Marekani inao wagombea binafsi.
 

Mzee hapa napingana na wewe. Umesema fisadi alieiba rasilimali za umma na kuzificha nje ya nchi anawe kuzirudisha na kuzitumia kununulia kura na matokeo ya uchaguzi mkuu je fisadi huyo huyo ana shindwa vipi kutumia fedha zake kushinda ndani ya chama au kumnunua mtu ambae ni mgombea wa chama?

Kwa heshima na taadhima nasema your argument is invalid. Kama shida ni pesa za kifisadi kutumika kwenye chaguzi hata sasa kwenye mfumo usio na mgombea binafsi hilo laweza tokea.
 
hii issue ya kukatana majina dakika za mwisho itakuwa imeshapata muarobaini. Kata jina nachukua form mgombea binafsi. Vyama vya siasa vitakosa nguvu. pia ukinifukuza chama bado nitakuwa na ubunge mpaka kipindi changu kiishe sababu nawakilisha wananchi walionichagua
 
Wakati ule Mtikila ameshinda kesi yake ya kutaka Mgombea binafsi NA serikali kumbania, wewe Ritz NA ndugu zako akina Malaria sugu mlikuwa mstari WA mbele sana kumpinga mgombea binafsi. Leo hii, wamemkubali mmeamua kuwa Bender

a! Duh!

Ngoja nifukue ushahidi huo
 
 
Huyu Mzee yeye apumzike tu. Uzee ni busara lakini kuna kuteleza. Rais anawajibika kwa Wananchi wake na si Chama Cha Siasa!
 
mzee wangu mtei una khofu kubwa sana na kijana wako zitto manake una mbania sana kuwakilisha chamma chako katika ngazi ya juu sas ukimchezea tena atakukimbia na itakuwa anguko la ajabu la chama chako.
 

Mkuu, kwani Wananchi wakimtaka tatizo liko wapi???? Kuna tofauti gani ya kuruhusu mgombea binafsi ngazi za chini na kuacha katika ngazi ya Urais??

Hapa tunabishan mitazamo tu, lakini kila kitu kina faida yake na hasara yake. Ambazo katika hali ya kawaida, ni Wananchi ndo wataamua mfumo wanaoutaka.
 
Kwani fisadi huyo anashindwa vipi kuanzisha chama cha siasa akanunua kura? Kwani kununua kura mpaka awe mgombea binafsi?

Kama wewe uliweza kuanzisha CHADEMA, fisadi huyo unayemuogopa atashindwa vipi kuanzisha CCJ?
si ndo ushangae sasa,kwani ukigombea kupitia chama ndo huwezi kuwa fisadi?

Bunge litakua na mamlaka ya kudeal na rais na wabunge wakileta uzembe wananchi watakua na nguvu ya kuwatoa.
 
Tanzania bado sana mgombea kusimama mwnyewe kama mwenyewe bila kupitia chama na akashinda.We still have a long way to go in order to reach that level.
 
Kweli nimeamini siku hizi uzee ni kutokuwa na busara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…