Mtei akosoa mgombea binafsi kuruhusiwa kuwania urais

Mtei akosoa mgombea binafsi kuruhusiwa kuwania urais

I can read between the line kwa kauli ya Mzee Mtei.

Mzee Mtei, acha kufikiria chama kwa sasa. Kauli zako zilitakiwa ziwe niza mtazamo wa kitaifa.

Kauli kama hii haukupaswa kabisa kutoka kwa kiongozi na mwanzilishi wa chama cha Demokrasia na maendeleo. Badala ya kukuza demokrasia, unachofanya ni kupunguza.

Kama vyama vitaweka mgombea mzuri ambaye atajibu maswali ya kitaifa kwa wananchi, basi wananchi watampa kura.

Demokrasia haipatikani kwenye magenge ya vyama vya siasa peke yake.

Isije ikawa kauli hii imekuja kutokana na hofu ya kupunguziwa kura kwa mgombea fulani kwa sababu kuna mgombea binafsi atakuwa EMBEDDED kama duru za kisiasa zinavyoonyesha kuwa kuna kiongozi fulani ambaye uwezekano wake ni mkubwa kuwa Presidential independent candidate kwa vile chama chake hakionekani kumkubali.
 
kimtazamo wangu naona bora mgombea binafsi kwani waliokuwa kwenye vyama waliukuwa utumbo mtupu hakuna chochote kilichofanywa kwao kwani uozo mtupu bora ya kuwa na mgombea binafsi nadhani Tanzania itabadlika
 
lakini anachozungumza ni kweli bhana hakuna haki yoyote iliyotendeka kwenye serikali yetu kwani tume ilijaa dini moja tu wewe unadhani kuna usawa hapo ni propaganda tu
Haelewekagi huyo,mara tume ina waislamu wengi mara oooh mgombea binafsi awepo mara asiwepo, mladi ubinafsi tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Katiba ya Marekani inaruhusu mgombea binafsi; sawa.

Hebu taja wagombea binafsi ambao wamewahi kuwa Marais wa Marekani?
Kugombea na kushinda ni vitu viwili tofauti.

Huwezi hata kidogo kutumia kipimo kama hicho katika kujenga demokrasia kwenye jamii na taifa huru.
 
Katiba ya Marekani inaruhusu mgombea binafsi; sawa.

Hebu taja wagombea binafsi ambao wamewahi kuwa Marais wa Marekani?

Sasa hilo ni swala lingine kabisa. Kuweza kugombea haimaanishi kushinda. Maana kwa mantiki yako tusiwe na vyama vya upinzani kwa vile hakuna mgombea wa chama cha upinzani aliewahi kuwa raisi???
 
Katiba ikipita swala la kuwakilisha wananchi litakuwa ni mfuko wako tu. Ingawa bado sijaisoma Rasimu yote sijaona bado matumizi ya fedha za uchaguzi na auditing yake. Kuna matajiri wengi sana duniani wanauwezo kabisa wa kumsimika Raisi na wabunge wa kutosha kwa fedha zao na wakashinda kwa kivuli cha mgombea binafsi.

Lazima tuichambue hii Rasimu vizuri na kuhakikisha demokrasia yenye mipaka ipo. Naunga mkono 100% Mgombea binafsi ila katiba lazima iweke wazi matumizi ya fedha za kampeni na jinsi zinavyoweza kupatikana.

Lakini bado hata kwa kutumia vyama, kwenye chaguzi hizi zetu za kiafrika, bado kuna matajiri wanaweza kupenyeza watu kwenye uongozi through chama. Kwani Kikwete akiingia madarakani? Si zilitumika fedha kuwahonga wajumbe wa mkutano wa ccm? Fedha za akina Rostam!
 
..hoja ya mzee Mtei kuwa rais atokane na chama haina msingi sana.....maana katiba hutaka mgombea kutoka kwa watu na si vyama....Infact katiba ya nchi si ya vyama ......bali ya watu...na ndio maana kwenye katiba hamna chama chochote kinachotajwa....

Labda mzee anaogopa kukimbiwa/kutopata na wanachama anaodhani wanaweza kugombea urais kupitia chama chake?....au hofu kwa wana ccm weeengi kugombea urais kama wagombea binafsi kama mkakati wa ku dilute kura na kufanya Chama chake (CDM)kuwa na ugumu wa kufikisha idadi ya kura stahiki?....hawa wazee wanafikiri mbali.....
 
Acha uongo mkuu. Nikupe mfano mmoja tu. Marekani inao wagombea binafsi.

tofautisha marekani na tz.sisi tunaishi kwa blah blah wakati wenzetu wanaangalia facts.mfano mtu kama sitta uchaguzi uliopita(kama ingekuwepo katiba inayoruhusu mgombea binafsi) angejitoa ccm na kusimama yeye kulikuwa na possibility ya kushinda pamoja na ukweli kuwa alioongoza harakati za chuki binafsi(zilizomwongezea umaarufu) zilizoathiri uchumi wa nchi.outcomes zake zinafahamika hakuna haja ya kukumbushana.mtu kama huyo unaona kabisa anaongozwa na tamaa ya madaraka sasa mkimpa nchi sehemu kubwa ya muda wake madarakani atautumia kuwashughulikia wabaya wake wakati nchi inadoda.though nakubali kama kutakuwa na sheria nzuri za kuwasimamia na kuwawajibisha tunaweza kupata kiongozi mzuri kwa nchi yetu.
 
True That... Tutakuwa ni NCHI PEKEE DUNIANI yenye MGOMBEA BINAFSI na hii ni kwasababu ya VIONGOZI waliobaki NCHINI hawakuwa VIONGOZi walipewa nafasi kuzijaza tuuu kwasababu ya UNYENYEKEVU na SIO UELEWA wa SIASA...

Sasa we ARE GOING TO PAY DEARLY...

Nakumbuka kule Maraekani Lord Parrot(?) (Bilionnaire) alishawhi kugombea URAIS wa Marekani kama Mgombea binafsi! No Research No right to Speak
 
Sasa hilo ni swala lingine kabisa. Kuweza kugombea haimaanishi kushinda. Maana kwa mantiki yako tusiwe na vyama vya upinzani kwa vile hakuna mgombea wa chama cha upinzani aliewahi kuwa raisi???

Mkuu mimi sijakataa mgombea binafsi kuruhusiwa kwenye katiba mpya.

Lakini najiuliza kiuhalisia ni wapi mgombea binafsi amewahi kushinda?
 
Wrong!! rais anachaguliwa na wananchi na anawajibika kwao tu, na siyo kwa vyama vya siasa. Haya mambo ya kamati kuu za vyama hayana maana.
Samahanini. Nauliza hili kwa lengo la kujifunza. Hivi kuna nchi inayoongozwa na kiongozi ambaye alikuwa mgombea binafsi? Inaposemekana anawajibika kwa wananchi, maana yake ni nini? Akiboronga anawajibishwaje na hao wananchi?
 
Kwa mawazo yangu...tumekuwa tukipata wagombea uraisi kutoka vyama vyetu huku kukiwa na manung'uniko ndani ya vyama......kwa hili litapunguza hiyo hali na kufanya vyama vyetu viwe na demokrasia ya kweli katika kupata mgombea wake ili kuepuka kwa wagombea wengine kujitoa na kuamua kugombea binafsi ili mradi tu anakubalika......tulifikia mahala hadi tunajinadi kwa chama fulani hata tukisimamisha jiwe tunapata ushindi......sasa ni bora kuwa na mawe mengi......vyama visituchagulie viongozi....ambao wakiboronga mnawalinda ili muendelee kuwepo madarakani.......
 
tofautisha marekani na tz.sisi tunaishi kwa blah blah wakati wenzetu wanaangalia facts.mfano mtu kama sitta uchaguzi uliopita(kama ingekuwepo katiba inayoruhusu mgombea binafsi) angejitoa ccm na kusimama yeye kulikuwa na possibility ya kushinda pamoja na ukweli kuwa alioongoza harakati za chuki binafsi(zilizomwongezea umaarufu) zilizoathiri uchumi wa nchi.outcomes zake zinafahamika hakuna haja ya kukumbushana.mtu kama huyo unaona kabisa anaongozwa na tamaa ya madaraka sasa mkimpa nchi sehemu kubwa ya muda wake madarakani atautumia kuwashughulikia wabaya wake wakati nchi inadoda.though nakubali kama kutakuwa na sheria nzuri za kuwasimamia na kuwawajibisha tunaweza kupata kiongozi mzuri kwa nchi yetu.

Mkuu wewe unaongelea kitu kingine kabisa todauti na jibu nililo toa hapo juu. Mtu kasema Tanzania ingekua nchi ya kwanza kuwa na wagombea binafsi which ni uongo. Hicho ndicho nilicho jibu mimi. Hilo la faida au hasara ya mgombea binafsi ni tofauti na nilicho jibu mimi.
 
Mzee mtei anawasiwasi na kijana zitto manake jamaa akisimama kama yeye baada ya kumbania basi chadema wanaweza ambulia aibu.

Rasimu ya katiba mpya inasema mgombea wa uraisi awe na miaka zaidi ya 40, na asiwe na miaka chini ya 40
 
Mkuu,
Una hakika na ulichoandika hapa chini? Nchi kubwa na zenye demokrasia mfano USA na nchi zingine zina mgombea urais huru.

Rais inatakiwa awajibike kwa wananchi na sio kwa vyama.

Wapi UMESIKIA USA ina MGOMBEA BINAFSI - Katiba yao INAKATAZA sababu lazima Wananchi waelewa IDEOLOGY ya CHAMA saa nyingine hawachagui MTU wanachagua ITIKADI za CHAMA
 
Mkuu kabla haujaandika jaribu kwanza kufanya utafiti japo kidogo Tanzania siyo ya kwanza kuruhusu mgombea binafsi.

Nimeandika baada ya UTAFITI USA INDIA UK FRANCE KENYA zote hizo zina Demokrasia safi na hawana Mgombea Binafsi kwasababu wananchi hawachagui SURA ya MTU wanachagua ITIKADI za hicho CHAMA
 
Mawazo HAFIFU ya mzee Mtei yanachelewesha demokrasia ndani ya chadema.

Sasa anataka mawazo hayo HAFIFU yaingie kwenye katiba.

Katiba haitachukua mawazo HAFIFU. Taifa linahitaji mawazo BORA yanayoleta MAENDELEO.
 
Nimeandika baada ya UTAFITI USA INDIA UK FRANCE KENYA zote hizo zina Demokrasia safi na hawana Mgombea Binafsi kwasababu wananchi hawachagui SURA ya MTU wanachagua ITIKADI za hicho CHAMA

Nani kakwambia USA hawana mgombea binafsi?

Tatizo watu wengi mnafuatilia front runners tu!!!
 
Back
Top Bottom