Mtemi Mirambo VS Mtemi Mkwawa

sijawahi kusikia Historia ya mirambo, lakini mleta mada umepoteana ulipolisifu jeshi la Mirambo lenye askari elfu kumi wakati Mkwawa pia alikuwa na idadi kubwa ya askari
 
Kuna mtemi mmoja kutoka Afrika kusini jina nimemsahau alitaka aje kumpiga Mirambo aichukue himaya yake alipofika na alichotarajia kukuta sicho alichofikiri ikamlazimu kuomba aungane tu na Mirambo kwakuwa hakuwa namna.
Jeshi la Mirambo kwa mambo yao na sura ngumu waliaminika huvuta bangi kabla ya kuingia kazini. Kijana wa kiume ukiwa mvivu lilikuwa ni kosa linaloweza kukusababishia hata kunyongwa.


MAGUFULI4LIFE.
 
Mirambo badooo sana kumuwekea battle na mkwawa. Kwa wasiojua hadi leo kuna medan ya kivita aliitumia mkwawa kijj cha LUGALO kwenye battle na kamanda VON ZELEWSKY, tactic hii inatumiwa na kufundshwa pia na JWTZ.. hadii leo staitaji ni siri za jeshi..So miramboo hakuwaa genious kuliko mkwawa...big no . Japo naweza kukubali geographically mirambo alikuwaa na sehem kubwaa with lillte resistance.
 
Swali kwako bwana mwandishi/msimulizi...

Je ni wakati upi ambapo Waarabu walikuwa wakienda maeneo ya kuanzia Kigoma hadi Unyamwezini kujitwalia watumwa?

Ni kipindi cha Mirambo, Isike au mtemi mwingine tu?

Ikumbukwe watumwa wengi waliokijaza kisiwa cha Zanzibar wale waliouzwa masoko ya watumwa ya Bagamoyo na Kilwa Masoko walitokea Unyamwezini na maeneo ya Kigoma na Katavi ya sasa
 
Stori nzuri sana!
Mkuu tupe reference yo yote inayoeleza ukweli huu.Harafu uniweke sawa ugonjwa wa rovu ukoje!
 
Hapana, mtemi Milambo alifariki kwa kulishwa vitu na mjomba wake, waligombana. Alikatazwa na mama yake asiende kupigana na mjomba wake, hivyo uncle alimzidi uganga Milambo akajikuta kachukuliwa kwa njia za kishirikina na kula kichwa cha mbwa na baada ya hapo alipojigundua akasema Mjomba basi umeniweza, na ukawa mwisho wake.
 
Wazee wengi wanasema aliuawa kama ulivyo sema na wengine wanasema kuna muda Mirambo aliugua akashindwa kusimama kama kiongozi kwa ugonjwa ndipo ndugu wakaona wamuue tu ili kiti akalie ndugu mwenye nguvu ila haya hayajawekwa hata kwenye historia ya pale kwake ukienda kujifunza.


MAGUFULI4LIFE.
 
Ukirudia kusoma utajua snitch wa Mirambo chief Mkasiwa ndiye alikuwa anauza watu wake na ndiye aliye wakaribisha waarabu Tabora.


MAGUFULI4LIFE.
 
Dah kweli kabisa mkuu huyu jamaa alikua na sehem inaitwa sela magazi hapo mahala ilikua ni kumwaga damu
 
Tactic kubwa ya Mirambo ya kujifanya umezidiwa mapambano na kurudi nyuma ndiyo iliyotumika kumpiga Idd Amini pale darajani JWTZ walirudi nyuma kama wamezidiwa kumbe ndio zilikuwa hesabu zenyewe. Katika machief waliokuwa wajanja na wenye akili ya haraka Mirambo ndio mshika bendera.


MAGUFULI4LIFE.
 
Kwa mantiki hiyo kumbe mirambo alikua mwamba kwa sababu wakoloni hawakuhitaji mikataba na machifu ya kibiashara Ila walipora na kitu kingine kwenye himaya ya mtemi mirambo hawa jamaa hawakugusa kuchukua mtumwa yeyete Ila walipita na watumwa kutoka huko mbali na Kodi walitoa
 
Bado kidogo kila chief aliyejulikana anauza watu wake Mirambo hakumuacha salama alienda kumpiga na kutanua himaya ndio sababu ya Mirambo kutawala mpaka ziwa Victoria kurudi Kagera mpaka ziwa Tanganyika kote alifanikiwa kuunganisha na kuwa himaya yake. Hata kisa cha kuvuka ziwa Tanganyika kwenda kuipiga himaya ya Urundi ambayo ndio Burundi ya sasa ni baada ya chief wake kuwa anauza watu wake.
Bila kufa mapema Chief Mirambo huenda mpaka sasa Afrika mashariki ingekuwa nchi moja.
Kifupi Mirambo alikuwa mpingaji wa biashara ya watu.
Mzungu sio tu kulipa kodi kwa wananchi wa Mirambo, alikuwa akifanya fyoo mali zote zinachukuliwa na Mirambo.


MAGUFULI4LIFE.
 
Kuna chief mmoja wa Pimbwe yeye alichezea kichapo baada ya kusadikika aliwapokea wamisionari wawili. Ingawa wakati Mirambo anaenda kumpiga wamisionari hakuwakuta walikuwa wameshakikimbia kichwa cha Mirambo.


MAGUFULI4LIFE.
 
Stori nzuri sana!
Mkuu tupe reference yo yote inayoeleza ukweli huu.Harafu uniweke sawa ugonjwa wa rovu ukoje!
Reference kwakuwa historia yake haikuwekwa wazi inakuwa ngumu kidogo ila hii kidogo itakupa ishara.
Tabora kuna sekondari inaitwa Mirambo high school. Vijana wote wanaoenda kusoma pale huingiwa na ujasiri wa ajabu na misimamo ambayo hata kama haiko sawa wao hulazisha ifatwe hivyo hivyo. Sasa watu walishajua huwa ni nguvu ya jina na wazee huwa baada ya muda wanafanya yao wanayoyajua kutuliza nguvu ile. Inasemekana huwa wanafanya tambiko la kumtuliza mwenye jina.
Rovu ni ugonjwa wa uvimbe shingoni.


MAGUFULI4LIFE.
 
Historia inasema Mkwawa aliwashinda Wajerumani hadi wakaja mara ya pili kwa nguvu kubwa. Unaweza kutuambia kama kuna historia ya Mirambo kushinda jeshi la nje ya Afrika? Kama lipo au umaarufu wake ie alishinda vita zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…