DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa imemhukumu Bw. Badwin Atanazi Chundu (60), Mtendaji wa Kata ya Ikozi, kifungo cha miaka 60 jela pamoja na kurejesha zaidi ya Shilingi milioni 44 alizozitumia vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Rukwa, Bw. Chundu alitiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma, ambazo zilikuwa ni mapato ya ushuru wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Hukumu hiyo imetolewa chini ya vifungu vya sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329 (Marekebisho ya 2019), pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Kupangwa (Sura ya 200).
TAKUKURU Mkoani Rukwa imeeleza kuwa hukumu hiyo ni moja ya mafanikio ya mapambano dhidi ya rushwa na ufujaji mali za umma, na imetoa rai kwa watumishi wa umma kuacha vitendo vya kujinufaisha binafsi kwa kutumia fedha za serikali.
Chanzo: Vosfmtz