KERO Mtendaji wa Kijiji cha Ukingwaminzi - Katavi anatumia madaraka vibaya, anabagua watu

KERO Mtendaji wa Kijiji cha Ukingwaminzi - Katavi anatumia madaraka vibaya, anabagua watu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mtendaji wa Kijiji cha Ukingwaminzi, Kata ya Mwamapuli, Wilaya ya Mpimbwe, Mkoa wa Katavi, amekuwa akifanya maamuzi ya kibaguzi na ya upendeleo dhidi ya wananchi wa kijiji hicho wanapowasilisha shida zao, hasa zinazohusu migogoro.

Kuhusu ujenzi wa vibanda vya biashara pembezoni mwa barabara, amekuwa akiwazuia wananchi wa hali ya chini huku wale wenye uwezo wa kifedha akiwaacha waendelee, licha ya kudai kuwa maeneo hayo yako kwenye hifadhi ya barabara.

Pili, muda mwingi wa siku na saa za kazi amekuwa akifunga ofisi na kufanyia kazi nyumbani. Mara nyingi wananchi wanapomfuata nyumbani, hukataa kuwahudumia na kuwaacha warudi bila kupata huduma. Wanapomuhoji, huwajibu kwa dharau na kiburi kuwa hawajamuajiri wao.

Tatu, kwenye kesi mbalimbali, amekuwa akitoa maamuzi ya kutisha bila kusikiliza maelezo ya pande zote mbili zinazoshitakiana.

Tunaomba serikali itupazie sauti kwa kumuhoji mtendaji huyo, kwani wananchi wamevumilia vya kutosha. Ikiwezekana, awajibishwe kwa matendo yake yasiyo ya haki kwa wananchi, huku akiwa ndiye kiongozi tegemeo wa kutoa maamuzi ndani ya kijiji.
 
Back
Top Bottom