TANZIA Mtia nia wa Ubunge Moshi Vijijini, Dkt. Donald Kisanga afariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Dodoma

TANZIA Mtia nia wa Ubunge Moshi Vijijini, Dkt. Donald Kisanga afariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Dodoma

Hahaha nawafahamu wachache walioko jirani na hapa nilipo, mara kwa mara napata taarifa zao za hivi ndio maana ika comment vile sikuwa nazuia wasife mkuu.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji28]ukaona yaishe[emoji134][emoji134][emoji16]
 
Safari za Dar Dodoma hata kwa Vitz/ Passo sikuhizi watu wanaenda
-Pale Dodoma kuna hadi taxi za kwukuwahisha Dar kwa wabunge ambao wanatakaga kwenda Dar weekend bila magari yao wanaenda na Taxi(Premio, Corona nk) na madereva wa Kijiwe cha Dodoma Hotel wanapiga hela

-Halafu pia alikua mzoefu Mwezi uliopita alikuwepo kwenye mkutano mkuu na hapa juzi ndo alikwenda kumsindikiza JPM kuchukua fomu na alishafika akawa anasubiria mkutano wa UVCCM.

- Alipata ajali sehemu alitoka kula Kisasa mwisho nadhani wakati anarudi barabarani ndo lori likamzoa

Pia alikua anatumia Cruiser II mara nyingine
View attachment 1532927

Duh aisee, nimejaribu kufikiria ni ajali ya namna gani, tena Dodoma mjini nikashindwa kupata jibu.!
Mwenye taarifa anazikwa wapi jamani tufahamishane.
 
Inasikitisha sana. Japo kifo hakiangalii umri lakini inaumiza sana vijana wadogo wanapopoteza maisha mapema namna hii.

Huu ni msiba mkubwa kwa wanafamilia. Mungu wetu awajaze moyo wa unyenyekevu katika kuyapotea mapenzi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumzika salama comred
Pole kwa wafiwa na chama chake
 
انا لله وانا اليه راجعون

Kila nafc itaonja umauti

Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور
((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]

Tokea kuumbwa kwa Nabii Aadam عليه السلام hadi leo na mpaka siku ya Qiyaamah hakuna kiumbe kitakachobakia isipokuwa Mwenyewe Mola Mtukufu kama Anavyosema:
كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ
((Kila kitu kitaangamia isipokuwa Yeye)) [Al-Qaswas: 88]

Vile vile Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

((كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ))
((وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَام))

((Kila kilioko juu Yake kitatoweka))
((Na Atabakia Mwenyewe Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu)) [Ar-Rahmaan: 26-27]

Baada ya kupulizwa Swuur (baragumu) siku ya Qiyaamah viumbe vyote vitakufa kwa mpangilio Anaoutaka Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى. Kisha mwisho atabakia Malakul Mawt (Malaika mtoaji roho) na Allaah سبحانه وتعالى. Kisha Allaah سبحانه وتعالى Atamuamrisha Malakul Mawt ajitoe roho yake mwenyewe. Atakapokufa Malakul Mawt Atabakia Allaah سبحانه وتعالى Pekee wa Mwanzo na wa Mwisho, Al-Hayyul-Qayyuum (Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo). Allaah سبحانه وتعالى Siku hiyo Atazikusanya ardhi na mbingu katika Mikono Yake,

((وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ))

((Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume)) [Az-Zumar: 67]

Na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنه kwamba:

((يطوي السموات والأرض بيده، ثم يقول: أنا الملك، أنا الجبار، أنا المتكبر، أين ملوك الأرض؟ أين الجبارون؟ أين المتكبرون؟)) مسلم

((Allaah Atazikunja mbingu kwa Mikono Yake, kisha Atasema, Mimi ni Mfalme, Mimi ni Al-Jabbaar (Mwenye Kushurutisha), wako wapi wafalme wa dunia? Wako wapi majabbaar (wanaolazimisha), wako wapi wanaotakabari?)) [Muslim]

Hapo tena Atauliza mara tatu:
((لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ))
((Ufalme ni wa nani leo?)) [Ghaafir:16]

Hakutakuwa na mtu wa kujibu, basi Atajibu Mwenyewe,
((لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّار))

((Ni wa Allaah Mmoja Mtenda Nguvu)) [Ghaafir 16]

Na hapo tena ndipo kila mtu atakuta hesabu yake ya matendo aliyoyatenda duniani ikiwa ni mema au mabaya, hakuna atakayedhulumiwa hata chembe, kwani Allaah سبحانه وتعالى Atahukumu kwa uadilifu baina ya viumbe Vyake. Kila jema Atalilipa kwa mara kumi na kila ovu atahesabiwa mja kwa ovu moja.

((الْيَوْمَ تُجْزَى كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ))

((Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma. Hapana dhulma leo. Allaah ni Mwepesi wa kuhisabu)) [Ghaafir: 17]


Poleni sana wanafamilia.
 
Back
Top Bottom