Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mtia nia ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kinondoni, Joseph Boniface Mhonda, ametoa wito kwa wanachama na wagombea wenzake wa CCM kuwa watulivu na kuheshimu taratibu za chama, wakati huu wa mchakato wa ndani wa chama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza katika mahojiano mafupi na wanahabari, Mhonda ambaye ni Mjumbe wa zamani wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi na mmiliki wa QS Mhonda J Apex Group of Companies Ltd, amesema mchakato huu unapaswa kuendeshwa kwa nidhamu, mshikamano na uvumilivu akieleza kuwa “Chama kwanza, mtu baadaye”.
Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu 2025
Mhonda ambaye amewahi kushika nafasi ya pili katika kura za maoni za CCM mara tatu mfululizo (2015, 2017, 2020), ni miongoni mwa wagombea wanaopewa nafasi kubwa kutokana na uzoefu wake katika siasa, maendeleo ya jamii na taaluma ya ujenzi.