Mtifuano: Alikiba na Ruby kisa jina la mbwa mpya wa Alikiba

Mtifuano: Alikiba na Ruby kisa jina la mbwa mpya wa Alikiba

Majina siku hizi yana hati miliki?
Mbona mijibwa chungu nzima inaitwa Tom hatujasikia wenye jina wakilalamika
With all due respect young lady it's just misunderstanding Kiba hawezi kukutukana intensionaly

Kweli wana vipaji lakini wajaribu hata kupata elimu kidogo ya kuwawezesha kupanua uwezo wao wa kufikiri,kupambanua mambo, na kufahamu mengine nje ya mazingira yanayowazunguka!! Kulalamika mbwa kuitwa Ruby ni kituko unless amwombe Kiba abadili jina la mbwa wake!!
 
One week before huyo binti alikutana na diamond na kusema ilikuwa business meeting..! Sasa baada ya siku kadhaa anakuja na barua ndeefu ya malalamiko kwa alikiba, kwa maono ya kwaida unaweza kuhisi kuwa kuna influence ya hii kitu kutokea kutoka upande wa Pili, sasa badala ya kulimaliza na Ali mwenyewe kalibebelea kupeleka insta, kilichomkuta huko hawezi kuludia tena, kuna msanii alishawahi kuulizwa juu ya diamond na alikiba, akasema kwa msanii wa bongo ukitaka kupata hali mbaya basi waseme vibaya hawa wasanii wawili yani diamond na alikiba...! Sasa binti kaona balaa lake
 
Kusema ukweli king kiba amekosea mara nyingi watu hawatoi majina kwa wanyama ambayo yanakonnection na watu wanaowafahamu tayari Rubby na King walishakutana iweje atoe jina hilo au tayari Rubby alishakuwa maarufu ni sawa umpe mbwa wako jina linafanana na mtu mnaefahamiana huyo mtu akijua atajisikiaje kifupi King akiba akutumia busara ,jina King linahitaji busara kama za mfalme suleiman
 
Ukweli Kiba inabidi ajirekebishe niliangalia interview yake na Spora nimeanza kupata perception nyingine juu yake, abadilike kwa kweli
 
Jiwe (madini) yenye thamani rangi yake nyekundu

Nipe mrejesho, mlienda kule Tabata na Kaboom?

Maana jamaa hachelewi kujifanya eti yuko bize.

Kama hamkwenda nipe jibu fasta nijipange kukupeleka maana mimi ndo nilipamwelekeza.
 
Halafu maskini wala hakuna mtifuano wowote, karuby kamelalamika wee kakimlalamia kaka kiba halafu kiba akakaomba radhi yakaisha. ...loh wenye kuyabeba wakayabeba yakanakshiwa kila aina ya maneno kisha yakarushwa halafu yakadakwa na wapenda umbea

Ndo wabongo tulivyo. Wenyewe wameshasameheana kitambo. Ila kuna watu watayakuza na kuongea mambo mengine ambayo sio kabisa

Tena unakuta washabiki tunalalamika kwa wasameheane wakati sisi bado tunataka kuona ligi?
 
RUBY N JINA TUU KAMA MAJINA MENGNE...KWAN MM NKIMUITA MBWA WANGU john! Kuna shida apo?? NADHAN N UTOTO TUU
 
Ali Kiba mbwa wake mpya ameamua kumuita jina la ruby na kupelekea watu wa karibu na kiba na mashabiki zake(teamkiba) kumuita binti na chipukizi wa bongo flave mwenye sauti nzuri Ruby kushindwa kuvumilia matusi hayo, kupitia instagram RUBY ameandika...

Well well well
Kabla ya yote naombeni sana mashabiki zangu, mniwie radhi kwa nnacho kiandikia katika ujumbe huu binafsi mimi sijapendezewa kabisa na alichokisema kaka yangu @officialalikibakwenye kipindi cha @thesporahshow kilichorushwa kupitia @cloudstv kaka yangu alikiba mimi ni mdogo sana kwako si kwa umri wa kimuziki, sikutegemea na sijapendezwa na kauli yako yakunifananisha mimi na MBWA mimi ni binaadam na ni mdogo wako kama alivyo@zabibu92kiba sidhani kama ungeweza kumwita huyo mbwa wako zabibu au abdul, mimi sina ukaribu wowote na wewe lakini kama mtu niliyemkuta kwenye industry na uliyenitangulia kuliona jua na mpaka uliponifwata kuniambia una- appreciate kazi yangu nakuniomba nifanye nyimbo na mdogo wako @officialbdukiba na nikakubali yote hayo yalifanikiwa kutokana na love niliyokuwa nayo kwako kama kaka yangu,hujawahi hata siku moja kunitamkia kwamba unambwa wako anaitwa Ruby, kwa sababu mimi na wewe tumesha kutana nakuongea si chini ya mara moja, hujawahi kusema hilo kwangu, ila umekuwa ukiniambia tu naimba vizurii, je ulisahau nini kaka yangu hadi kushindwa kuniambia muhusika wa jina la mbwa wako mpya,mimi nimeona ni kejeli na dharau kubwa na hazisaidii katika maisha zaidi ni kujishushia heshima yako haipendezi kwa mtu kama wewe ambae pia unaangaliwa na watu wengi kama kioo cha jamii,nategemea kuona mfano mzuri kutoka kwako nikiwa kama mdogo wako lakini umenitia giza machoni @officialalikiba kakaangu kwakweli nimekwazika sana kwasababu mimi ndo kwanza naanza game naanza kazi ya kuendeleza nchi hii na afrika kwa dunia nzima kwenye upande wasanaa ambao wewe umeshaanza muda ,lakini nimestaajabu unanifananisha na mbwa ,cha ajabu zaidi hata watu wako wa karibu @rehemavisuallab @zabibu92kiba hawaitamki wala kuileta katika jamii kwa usahihi wa mbwa kweli ,Naamini Mungu hamtupi mja wake, chozi la mnyonge haliendi bure, Me namuachia Mungu''
Hata hivyo kuzima mtifuano huo alikiba amemuomba msamaha binti huyo kupitia uongozi wake


Kwa maoni yangu hii in kutafuta cheap popularity tu.mfano mbwa anaitwa tom na wewe unaitwa to hapo kuna shidaaa????imekuondolea nini wewe?mbona majina mengi ya kiafrika yana maana ya miti,wanyama,mizimu etc hujalalamika?mf.mapunda,ngonyani etc etc,huko ni kufsnanishwa na wanyama?au tu kutafuta cheap popularity?ruby ni wewe peke yako tu?????

Tatizo elimu tu
 
Kiba alikosea bhanaa ifike mahali tuangalie kitu gani alihojiwa na nin alijibu, yeye aliulizwa km ni balozi wa wanyama nataraji utakuwa hata na mnyama yeyote unaefuga, kiba akajibu nafuga mbwa alipoulizwa anaitwaje akacheka km dk 1 then akajibu Ruby Sporah akamuuliza kwanin unacheka ndipo aliposema Ruby ni msanii wa bongo fleva majibu yake yalionesha kuwa jina la Ruby amempa mbwa kutokana na yy anavyomfaham na kumchukulia ruby vile anavyoona yy binafsi kama kiba.
 
Back
Top Bottom