Sijaisoma wala sikushirikishwa katika utungaji wa sera hii mpya ya elimu. Lakini nilichokielewa ni;
1. Elimu ya msingi ( basic education) ambayo ni lazima kwa kila mtoto ni miaka 11 drs la 1 hadi 7 miaka 7 na kdt cha 1 hadi cha 4 ni miaka 4
2. Elimu ya kuwango hiki ni ya lazima na bure kwa maana serikali itagharamikia kila kitu vitendea kazi vyote km vitabu, chaki, vifaa vya maabara nk vitapelekwa kwa wingi kwenye mashule yote ya serikali.
3. Kwamba, sasa hakutakuwa na mtihani wa drs la saba uliokuwa unatumika km chujio la kupata wenye uwezo kwenda ngazi inayofuata ya elimu....sekondari, bali kupitia sera hii mpya kutakuwa na mitihani ya mara kwa mara kuwatambua wanafunzi dhaifu ili walimu wapate kuwasaidia lengo likiwa ni kila mtoto kumaliza elimu ya msingi!!.
4. Kwamba, sera hii inatambua Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya kufundishia katika ngazi zote za elimu lakini lugha zingine km kiingereza, kichina, kifaransa na kiarabu zitakuwa kama lugha muhimu zitakazofundishwa!.....HII MIMI NIMEIPENDA NA NAIUNGA MKONO KWA 100%!!
5. Kwamba kupitia sera hii mpya, mtihani wa mchujo utakuwa ule wa kidato cha nne ambao utawapata wanafunzi watakaoendelea kidato cha tano na sita!
.........tuendelee kuidadavua kwa kadiri ulivyo elewa