Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Unaweza ukaondoa mtihani kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu lakini ni je unapata nini mwisho wa siku. Kiukweli mtihani unasaidia kusoma kwa bidii.

Miaka ya nyuma tulikuwa na mtihani wa darasa la nne na bila kufaulu mtoto alikuwa haendi la tano. Wakati huo haikuwa rahisi kwa asiyejua kusoma na kuandika kuvuka hatua hii.

Leo hii baada ya kuondoa mtihani wa darasa la nne, tunashuhudia mtoto anafika darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika vivyo hivyo kwa mfumo huu tutegemee wasiojua kusoma na kuandika hadi kidato cha nne.
 
Wakifanya hivyo, watoto wa wenye hela watasoma English medium. Hapo sasa mtoto wa kapuku ataishia kuwa karani. kutumwa tumwa chai. Nan atamuajiri mtu asiyetema yai?
 
Are we serious?? Kwamba miaka kumi na moja ndio iwe ya Compulsory education? Serikali ina mpango gani na walimu asee, pamoja na mtihani wa Darasa la saba kuwepo,

kumekuwepo na ongezeko la vilaza secondary hali inayowapa waalimu wakati mgumu wa kutumia Nguvu nyingi kufundisha na mishahara yao yenyewe ndo hiyo. Mr president hapa Umeteleza
 
Angesema lugha ya kufundishia ni kiingereza kuanzia shule za awali ningeunga mkono, lakini kwa hili hapana.

"lazima ujue kuandika na kuongea kiingereza" nafasi nyingi za kazi hili ni sharti lao kuu,
 
Sijaisoma wala sikushirikishwa katika utungaji wa sera hii mpya ya elimu. Lakini nilichokielewa ni;
1. Elimu ya msingi ( basic education) ambayo ni lazima kwa kila mtoto ni miaka 11 drs la 1 hadi 7 miaka 7 na kdt cha 1 hadi cha 4 ni miaka 4

2. Elimu ya kuwango hiki ni ya lazima na bure kwa maana serikali itagharamikia kila kitu vitendea kazi vyote km vitabu, chaki, vifaa vya maabara nk vitapelekwa kwa wingi kwenye mashule yote ya serikali.

3. Kwamba, sasa hakutakuwa na mtihani wa drs la saba uliokuwa unatumika km chujio la kupata wenye uwezo kwenda ngazi inayofuata ya elimu....sekondari, bali kupitia sera hii mpya kutakuwa na mitihani ya mara kwa mara kuwatambua wanafunzi dhaifu ili walimu wapate kuwasaidia lengo likiwa ni kila mtoto kumaliza elimu ya msingi!!.

4. Kwamba, sera hii inatambua Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya kufundishia katika ngazi zote za elimu lakini lugha zingine km kiingereza, kichina, kifaransa na kiarabu zitakuwa kama lugha muhimu zitakazofundishwa!.....HII MIMI NIMEIPENDA NA NAIUNGA MKONO KWA 100%!!

5. Kwamba kupitia sera hii mpya, mtihani wa mchujo utakuwa ule wa kidato cha nne ambao utawapata wanafunzi watakaoendelea kidato cha tano na sita!

.........tuendelee kuidadavua kwa kadiri ulivyo elewa
 
Wakati nikiyaangalia haya maamuzi ya viongozi huwa najiuliza kuwa huwa wanatumia kiungo gani cha mwili kufikiria......maana maamuzi yao mengi ni kama mtu aliyetoka usingizini..........
 
Prof. Mchome amepatwa na nini? He is not thinking straight. Unaondoa filter ya kuchuja makapi, yet unatarajia kuongeza idadi ya watanzania walioelimika na wenye ujuzi.

How? Matokeo yake tutakuwa na watu wengi wamemaliza form IV na hawajui kusoma. Bila mtihani Wa darasa la saba, umeondoa incentive moja muhimu kwa walimu na wanafunzi kujifunza kwa bidii.

Je, lengo ni kuwa na vijana wengi waliomaliza form IV au tunataka vijana wengi walioelimika? Kama mtihani Wa darasa la saba hauna maana, ni nini kinafanya mitihani ya form IV, VI na vyuoni kuwa na maana?
 
Wakifanya hivyo, watoto wa wenye hela watasoma English medium. Hapo sasa mtoto wa kapuku ataishia kuwa karani. kutumwa tumwa chai. Nan atamuajiri mtu asiyetema yai?

Sera ya elimu itakuwa moja tu nchi nzima, shule za English medium zitaanzishwa kwa sera ipi mkuu? Au mimi ndiyo sijaelewa, hebu tuelewashane.
 
Ni vizuri kujipa mda tukatest approach hii then matokeo take yatatusaidia kujua kama tulukuwa sahihi ama tulipotea,kwa vile ina transitional period sioni tatizo as long yanayohitajika yatakuwa accessible mda itakapozinduliwa rasmi katika vitendo
 
hii Sera hapana.kuna mazuri ila mabovu mengi zaidi
 
Sijaisoma wala sikushirikishwa katika utungaji wa sera hii mpya ya elimu. Lakini nilichokielewa ni;
1. Elimu ya msingi ( basic education) ambayo ni lazima kwa kila mtoto ni miaka 11 drs la 1 hadi 7 miaka 7 na kdt cha 1 hadi cha 4 ni miaka 4

2. Elimu ya kuwango hiki ni ya lazima na bure kwa maana serikali itagharamikia kila kitu vitendea kazi vyote km vitabu, chaki, vifaa vya maabara nk vitapelekwa kwa wingi kwenye mashule yote ya serikali.

3. Kwamba, sasa hakutakuwa na mtihani wa drs la saba uliokuwa unatumika km chujio la kupata wenye uwezo kwenda ngazi inayofuata ya elimu....sekondari, bali kupitia sera hii mpya kutakuwa na mitihani ya mara kwa mara kuwatambua wanafunzi dhaifu ili walimu wapate kuwasaidia lengo likiwa ni kila mtoto kumaliza elimu ya msingi!!.

4. Kwamba, sera hii inatambua Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya kufundishia katika ngazi zote za elimu lakini lugha zingine km kiingereza, kichina, kifaransa na kiarabu zitakuwa kama lugha muhimu zitakazofundishwa!.....HII MIMI NIMEIPENDA NA NAIUNGA MKONO KWA 100%!!

5. Kwamba kupitia sera hii mpya, mtihani wa mchujo utakuwa ule wa kidato cha nne ambao utawapata wanafunzi watakaoendelea kidato cha tano na sita!

.........tuendelee kuidadavua kwa kadiri ulivyo elewa
 
Kwanza tukubali kiswahili kigumu kuliko kiingereza, hasa cha kishuleni (science), pia tunaongelea projects na international collaboration sijui kiswahili hadi chuo kama tutafika.

It means tujiandae kuwekeza pesa nyingi kusomesha watoto wetu English medium au Uganda au Kenya. Tukifikiri kwa undani hao wote walioandika hii sera watoto wao watasoma hizi shule zetu?
 
sere nzuri ya wao kuendelelea kututawala maana watoto wao watasoma hizo shule kama faiza na santi meri sisi wa kwetu za kata

ina maana wao wataendelea kututawala maana sisi tutakuwa hatuna elimu...

ntakula nao sahani moja
 
Sipati picha itakuwaje kama sasahivi english ipo na watu hawajui vizuri hicho kingereza, sasa itakapokuwa kiswahili hadi chuo itakuwaje?
 
Back
Top Bottom