Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Hawa watu ni wapumbavu sana, hivi unaweza kutengeneza Policy bila kuwa na strategic Plan?
 
Sasa kwenye kazi wanahitaji watu wajue kiingereza na hapa tumekitoa duh!
 
Mikataba ya nje lazima iwe inaandikwa kwa lugha ya Kiswahili hasa kwa ile mikataba ya mambo ambayo tuna nguvu nayo. Kampuni ya General Motors ikienda kufanya kazi China, haiwezi kulazimisha mikataba ya kuingia kule iandikwe kiingereza.

Inaandikwa kichina na inakuwa jukumu la General Motors kutafuta wafasiri wa Kichina kwenda kiingereza. Kunapotokea mgongano wa kisheria katika maneno - tafsiri ya kichina inakuwa ya mwisho.

Hapa kwetu tukifanya hivyo itakuwa ni kazi kwa wageni wanaokuja Tanzania kujifunza kiswahili - si kazi ya watanzania kujifunza lugha za wageni.

Nchi zote zinazojitambua zinafanya hivyo huko kwao na sioni wachina wakishindwa kuajiriwa General motors ya China eti sababu hawawezi kuongea lugha ya wanaomiliki Kampuni. Tena kwa sisi waomba misaada ndo kabisaaa - sababu tunaomba kwa wengi. Yaani tunaomba msaada kwa wajapan halafu mkataba umeandikwa kiingereza!!!!! Inatia kinyaa.

Nchi zote zilizosimama duniani hazijiendeshi hivi tunavyoenda sisi na hapo ndo pa kuanzia. Mkataba wa Tanzania na Accacia Mining ni lazima uandikwe kiswahili na utamke kuwa kukiwa na ubishani wa kisheria tafsiri ya kiswahili itachukua mkondo.

Wawekezaji bado watakuja tu kwani hawawekezi Tanzania pekee na huko kwingine masharti ndo yako hivyo. Mikataba iliyoandikwa kiswahili itaeleweka vizuri zaidi kwa watu wetu kuliko mikataba iliyoandikwa kwa lugha za Kigeni
 
Nilifikiri elimu ya msingi iwe mpaka darasa la tano, then unakuwa na wale wanaoenda michepuo ya vocational na wale wanaoendelea na pure shule hivyo hivyo mpaka secondary, na iwe compulsory.

I think compulsory education iwe mpaka mtoto atakapotimiza umri wa miaka 15/16.

Baada ya hapo, achague kama anataka kuendelea na A Levels, vocational training, kuingia kitaa, etc.
 
ni ushauri unaopokelewa bila kupimwa kwa sababu watunga sera wetu hawana muda na uwezo, lakini pamoja na bunge letu kuwa 'ruber stamp', naamini kwa mswada wa aina hii wino kwenye huo mhuri utakauka!
 
Sasa kwenye kazi wanahitaji watu wajue kiingereza na hapa tumekitoa duh!

Siku tukitangaza hii ni nchi ya KISWAHILI serikali ikawa inafanya shughuli zake kiswahili, hawa wageni walioko nchini kwa nini wasiendeshe ofisi zao kiswahili? Hapa ni kitu kidogo tu.

Ni serikali yetu kutambua tu. Hata kama kampuni za nje zinazofanya kazi hapa zitaendelea kutumia kiingereza kwenye ofisi zao, wakitoka nje watalazimika kutumia kiswahili kwa hiyo pole pole watabadirisha tu.

Tukishatamka kuwa nchi hii mawasiliano rasmi yatatumia kiswahili ... baaasi. Utaona mwenyewe pole pole mambo yakibadirika .... ndani ya miaka mitano tu.

Hata hivyo wasi wasi wako wa ajira bado ni wasi wasi tu kwani lugha kama kiingereza itaendelea kufundishwa tu na watu bado watakuwa na uwezo wa kuongea kiingereza.
 
Majanga,

Najiuliza tu ma-housegirl... mimba nk miaka saba tu shughuli sasa unaweka mpaka form four.., saidia fundi watapatikana wapi? Mi mawazo yangu ni kuwa na wasomi haswa na kuwa vocational skilled labour force haswa.

Hivi ni shule gani za msingi cum secondari zitakazoweza kuwafundisha elimu ya ufundi haswaaa. Vifaa watavipata wapi?Bunsen burner tu wameshindwa kununua je wataweza kununua lathe machine?

Nilifikiri elimu ya msingi iwe mpaka darasa la tano, then unakuwa na wale wanaoenda michepuo ya vocational na wale wanaoendelea na pure shule hivyo hivyo mpaka secondary, na iwe compulsory.

Tatizo letu sasa tuna wasomi wavaa tai wasiojua kufunga tai. Graduates weeengiii lakini weupeeee , matokeo yake wachina wanakuja na nyundo za kunyoosha magari na wanapiga hela ya hatariii.

Dah, yani mi hata sielewi dunia watakayoishi watoto wetu.

Nakuunga mkono kwa asilimia zote, Hata mi nilikuwa nafikiria kupunguza miaka ya shule ya msingi ni mingi mno na sekondari masomo yake mengi ni kama marudio ya darasa la tano mpaka la saba ila sema yanafundishwa kwa kiingereza tu nyongeza ni kidogo sana, Nilidhani wataleta mfumo ambao utaondoa wanafunzi kuariri mitihani na kutupatia wataalam wa kweri
 
DSC09471.jpg
 
Mkuu unadhani sisi tutaendelea kuwa masikinihadi lini? umeshaambiwa it will take decades just wait and see. Tanzania ya wasomi waswahili inawezekana.
 
Jana mheshimiwa Rais wa Tanzania alizindua Sera mpya ya Elimu ambapo kati ya mengi yaliyomo ndani ya sera hiyo ni kufutwa kwa mtihani wa Darasa la Saba na Elimu ya Msingi kuongezwa hadi Kidato cha Nne.

Nchi la ma.pumba.vu kuanzia magogoni mpaka Kigoma, Mtwara mpaka Bukoba! Kila mmoja anayeshika madaraka anakuja na mambo yake! Huyu jamaa anaondoka kesho kutwa kwa nini asimwachie mrithi wake hivyo vingine! Anajuaje anayekuja atakuwa na akili fupi kama ya kwake? Eti elimu ya Msingi mpaka kidato cha NNE?

Hebu ngoja nipate muda na Mimi niisome vizuri hii sera mbona kama siamini hiki kinachojadiliwa hapa!! Ina maana shule zote za Kata zitakuwa za Msingi? Kama siyo hivyo hizi za Msingi sasa hivi zina miundo mbinu ya kubeba wanafunzi Wa madarasa 12?

Au hapa tena wanataka kuanza kuchangisha wazazi kwa ajili ya uboreshaji shule za msingi? Natamani Lowasa angekuwa mzima Wa bukheri Wa afya achukue hii nchi ili asafishe huu uozo tunaoachiwa na Mzee Wa vigodoro!! Hili nalo tumeiga wapi? Maana sisi ni Wa maigizo tu kila nyanja!!
 
Ya J. Mungai yanarudi tena!!!!

Bora ya Mungai na Prof. Maghembe aiseee! Huu upanga wa kuliua taifa umeandaliwa na kupitishwa na Mkuu wa Kaya, tena kwa mbwembwe nyingi.

Anyway...miezi yake inahesabika, na Bunge lake linahesabika. Imani yangu, utawal ujao hautoweza kuvumilia hauvundo huu, hivyo utatupwa jalala la nyaraka, kama zilivyotupwa nyaraka nyingine.

Naitafuta sana hiyo nyaraka ili nijionee mwenyewe. Je nitavumilia haya mpaka lini?
 
Huu ni mwanzo mwema kwa nchi yetu. Kiingereza kimetufanya watumwa katika nchi yetu. Futa kiingereza kwanza katika mfumo wa uendeshaji wa serikali. Machapisho yote ya kiserikali yawe yanatoka katika Lugha ya Kiswahili.

Andika sheria zote za nchi kwa Lugha ya kiswahili na mahakama zetu ziendeshwe kiswahili - Huu ujinga wa kiingereza utaisha na wote watajifunza kiswahili na kuwa wasomi wa ukweli badala ya wasomi wa kukalili.

Ni aibu kuwa nchi baada ya miaka 50 ya uhuru tunatumia lugha ya mkoloni kuendesha nchi - ni aibu kubwa. Kule South Africa lugha ya ki-Afrikaans - lugha ya watu wasiozidi milioni 5 inatumika hadi kutoa PHD ya uhandisi, udaktari, n.k.

Lakini wataalamu waliosoma kwa lugha hiyo bado wako bora kimataifa. Hapa Tanzania mtanzania anaona haiwezekani kusoma PHD kwa kiswahili - kifupi kama huwezi kuandika chapisho la kupata PHD kwa kiswahili huna PHD bali umenakiri PHD.

Sisi kila tukisema lugha ibadirishwe watu wanakuja na madai oooh, uongozi utachukuliwa na waliosoma kiingereza!! Haya ni madahi mufilisi na ya Kisiasa tu. Uongozi wa serikali inayoendeshwa kiswahili utahitaji Kiingereza cha kufanyia nini?

Tujifunze kwa wenzetu. Lugha za kimataifa ziko nyingi, tuchague muhimu tuzifundishe, ila watu wetu wajifunze masomo yote ya msingi kwa Lugha zao. Mfano lugha za kufundisha iwe Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, Kichina na Kihindi.

Kazi ya kufasiri vitabu muhimu kutoka lugha mbali mbali kuja Kiswahili haiwezi kugharimu zaidi ya Sh. Billioni 200. Hizi fedha tunazo tena hatuhitaji kuomba senti tano. Huu utumwa wa kujitakia tuachane nao. Naunga mkono hoja.

Ndoto za alinacha!!
 
Hali hii inatisha! Elimu siyo jambo la kukurupuka hivi! Research ya kubadili yote hayo wameifanya lini na wamemshirikisha nani? Kumbe Lema hakukosea kusema wanawe hawatanusa vishule vya BRN

Nilidhani ni mimi na tundu lissu pekee, kumbe mpaka lema, alishasema! wengi tu hawasomeshi watoto wao shule hizi, ila wapo kimya!
 
Mbona zamani wazee wetu wamemaliza darasa la NNE au middle school wakiwa wanaweza kuzungumza vizuri kiingereza? Tusikwepe majukumu, ni rahisi sana kufufua ari na uwezo wa kufundisha na kutumia Kiingereza badala ya kuhangaika kutafsiri mambo kwa Kiswahili ambacho wala hakitakuwa Kiswahili hiki tunachofikiria.

Fundisha vizuri Kiingereza basi, sasa watoto wanafeli kwa sababu wakifundishwa Kiingereza hawakielewi au au sababu hakuna msingi wa kufundisha kiingereza kwa ufasaha? Tanzania tunafanya mzaha wa ajabu kabisa, nakwambia kama tumeshindwa kufundisha kiingereza wakati ndio lugha ya kufundishia mpaka university vipi ikiwa somo la la kawaida? Ndo basi tena kiingereza bye bye.
 
Hivi sera hii ilifuata taratibu zote zitumikazo kutunga sera?
 
Mkuu unadhani sisi tutaendelea kuwa masikinihadi lini? umeshaambiwa it will take decades just wait and see. Tanzania ya wasomi waswahili inawezekana.

Hii sera hata mhudumu wa ndege, mfagiaji, mhudumu wa ndani haimwandai. Nchi ya Kusadikika, je wewe ni binadamu yake. Abunuasi? DRC wameacha Kifaransa, Sudan wameacha Kiarabu, Rwanda wameingiza Kiingereza, ...... Nchi ina wasomi wazuri, wasomi legelege. WATANZANIA NDIO WAVUMILIVU KULIKO WATU WOTE DUNIANI. NAONA GIZA NENE.
 
Duh!

Kwa hiyo form 5 na 6 inakuwaje? Kwenye kiswahili, binafsi siungi mkono! Hatuna vitendea kazi BADO vya kufundishia kiswahili mpaka chuo. China, Korea, Uk, USA walifanikiwa kwenye lugha zao mama kama lugha za kufundishia sababu walikuwa na rasilimali ya kutosha, na kikubwa uwezo wa kifedha.

Ila ngoja tuone, tuwe positive!
Binafsi naona ni jaribio la kushughulika na mkakati ulioshindwa.Huwezi kujaribu kuiga China Urusi nk,huku ukiwa masikini kiasi hicho.Hao wanafunzi utakao waburuza toka msingi mpaka form four bila mchujo wowote lazima utegemee kuongeza umbumbu nchini
 
Tehe Tehe???? , hamutaki lugha ya kizalendo, aisee lugha ya mababu mwaikataa.... Kwanza na hizi English medium wazikataze kuongea ongea umombo kila dakika bhana, watoto Wadogo hawana uzalendo wa lugha yao kabisa, every time dad??? Ala... Kwanza kwa hii lugha ya kizalendo huko darasani mtaelewa sasa, ebo???
 
Hii ni kulizika taifa. Kuna nini nyuma ya pazia?

Watoto wao watasoma Kenya au nchi nyingine ambapo lugha ya kufundishia ni English kisha watachukua nafasi muhimu serikalini na watakuwa watawala wetu. Chezea ccm wewe!
 
Back
Top Bottom