Nilifikiri elimu ya msingi iwe mpaka darasa la tano, then unakuwa na wale wanaoenda michepuo ya vocational na wale wanaoendelea na pure shule hivyo hivyo mpaka secondary, na iwe compulsory.
Sasa kwenye kazi wanahitaji watu wajue kiingereza na hapa tumekitoa duh!
Majanga,
Najiuliza tu ma-housegirl... mimba nk miaka saba tu shughuli sasa unaweka mpaka form four.., saidia fundi watapatikana wapi? Mi mawazo yangu ni kuwa na wasomi haswa na kuwa vocational skilled labour force haswa.
Hivi ni shule gani za msingi cum secondari zitakazoweza kuwafundisha elimu ya ufundi haswaaa. Vifaa watavipata wapi?Bunsen burner tu wameshindwa kununua je wataweza kununua lathe machine?
Nilifikiri elimu ya msingi iwe mpaka darasa la tano, then unakuwa na wale wanaoenda michepuo ya vocational na wale wanaoendelea na pure shule hivyo hivyo mpaka secondary, na iwe compulsory.
Tatizo letu sasa tuna wasomi wavaa tai wasiojua kufunga tai. Graduates weeengiii lakini weupeeee , matokeo yake wachina wanakuja na nyundo za kunyoosha magari na wanapiga hela ya hatariii.
Dah, yani mi hata sielewi dunia watakayoishi watoto wetu.
Jana mheshimiwa Rais wa Tanzania alizindua Sera mpya ya Elimu ambapo kati ya mengi yaliyomo ndani ya sera hiyo ni kufutwa kwa mtihani wa Darasa la Saba na Elimu ya Msingi kuongezwa hadi Kidato cha Nne.
Ya J. Mungai yanarudi tena!!!!
Huu ni mwanzo mwema kwa nchi yetu. Kiingereza kimetufanya watumwa katika nchi yetu. Futa kiingereza kwanza katika mfumo wa uendeshaji wa serikali. Machapisho yote ya kiserikali yawe yanatoka katika Lugha ya Kiswahili.
Andika sheria zote za nchi kwa Lugha ya kiswahili na mahakama zetu ziendeshwe kiswahili - Huu ujinga wa kiingereza utaisha na wote watajifunza kiswahili na kuwa wasomi wa ukweli badala ya wasomi wa kukalili.
Ni aibu kuwa nchi baada ya miaka 50 ya uhuru tunatumia lugha ya mkoloni kuendesha nchi - ni aibu kubwa. Kule South Africa lugha ya ki-Afrikaans - lugha ya watu wasiozidi milioni 5 inatumika hadi kutoa PHD ya uhandisi, udaktari, n.k.
Lakini wataalamu waliosoma kwa lugha hiyo bado wako bora kimataifa. Hapa Tanzania mtanzania anaona haiwezekani kusoma PHD kwa kiswahili - kifupi kama huwezi kuandika chapisho la kupata PHD kwa kiswahili huna PHD bali umenakiri PHD.
Sisi kila tukisema lugha ibadirishwe watu wanakuja na madai oooh, uongozi utachukuliwa na waliosoma kiingereza!! Haya ni madahi mufilisi na ya Kisiasa tu. Uongozi wa serikali inayoendeshwa kiswahili utahitaji Kiingereza cha kufanyia nini?
Tujifunze kwa wenzetu. Lugha za kimataifa ziko nyingi, tuchague muhimu tuzifundishe, ila watu wetu wajifunze masomo yote ya msingi kwa Lugha zao. Mfano lugha za kufundisha iwe Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, Kichina na Kihindi.
Kazi ya kufasiri vitabu muhimu kutoka lugha mbali mbali kuja Kiswahili haiwezi kugharimu zaidi ya Sh. Billioni 200. Hizi fedha tunazo tena hatuhitaji kuomba senti tano. Huu utumwa wa kujitakia tuachane nao. Naunga mkono hoja.
Hali hii inatisha! Elimu siyo jambo la kukurupuka hivi! Research ya kubadili yote hayo wameifanya lini na wamemshirikisha nani? Kumbe Lema hakukosea kusema wanawe hawatanusa vishule vya BRN
Mkuu unadhani sisi tutaendelea kuwa masikinihadi lini? umeshaambiwa it will take decades just wait and see. Tanzania ya wasomi waswahili inawezekana.
Binafsi naona ni jaribio la kushughulika na mkakati ulioshindwa.Huwezi kujaribu kuiga China Urusi nk,huku ukiwa masikini kiasi hicho.Hao wanafunzi utakao waburuza toka msingi mpaka form four bila mchujo wowote lazima utegemee kuongeza umbumbu nchiniDuh!
Kwa hiyo form 5 na 6 inakuwaje? Kwenye kiswahili, binafsi siungi mkono! Hatuna vitendea kazi BADO vya kufundishia kiswahili mpaka chuo. China, Korea, Uk, USA walifanikiwa kwenye lugha zao mama kama lugha za kufundishia sababu walikuwa na rasilimali ya kutosha, na kikubwa uwezo wa kifedha.
Ila ngoja tuone, tuwe positive!
Hii ni kulizika taifa. Kuna nini nyuma ya pazia?