Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Nashukuru kwa ufafanuzi wako mkuu, hofu yangu ni hizi shule za kata, kama primary ni hadi darasa la 10 (Ngumu kuitaja) ko hizi za kata zitakuwa Advance zote?

Nini intention ya serikal hasa? Wanataka niamini kwamba Elimu tuliyo nayo ni bora sana kiasi kwamba Wanataka tuwe bora zaidi? Je jamii imehusishwa? Au ni Order from the Top? Are we after skills or certificates?

Mkuu. Kusema primary maana yake ni elimu yenye kumjengea msingi mtoto. Ilkikuwa na maana kuwa ni ya lazima kwa kuwa inamuaandaa kijana wholistically (kumkuza ktk nyanja zote) kwamba ahitimpo std7 aweze kujitegemea ktk nyanja mbalimbali za kiuchumi.

Kutokana na mahitaji ya dunia, kukua kwa teknolojia, na kuibuka kwa mambo mtambuka , Elimu hii ya darasa la saba imeonekana haieezi kuzikabili changamoto hizo.

Hivyo serikali imrona elimu inayoweza kumjenga mtoto kutokana na changamoto jajwa hapo juy, ni kuiextend mpaka kidato cha nne.

Kimsingi jamii imehusishwa. Kelele za kina hakiElimu, wazazi, wanataaluma kuwa elimu yetu ni mbovu kutokana na dunia ya sas, serikali imejaribu kutatua tatizo hilo. Maana ya elimu ya msingi ni nini?

.1. Ni lazima kwa kila kijana kama ilivyokuwa waki tuliopo.

2. Ni elimu itakayo mjenga mwanafunzi amalizapo aweze kupata maarifa atakayo yatumia kujipatia kipato nje au ndani ya mfumo rasmi.

3. Inatakiwa iwe practical oriented.
anyway tuishie hapa mkuu
 
Miujiza mingi hutokea Tanzania tu. Mfano rais kusamehe wezi. Mfano rais kukataa ripoti ya cag kuwa pesa za escrow ni za umma. Haya ya elimu ni km ulevi uleule wa xixiemu
 
Kwa mfumo uliokuwepo, ilikua ni rahisi kukubaliwa na vyuo vya nje ya nchi kwa elimu ya juu, nchi nyingi hasa zinazofuata mfumo wa uingereza zilikua zinatambua na kuwapokea wanafunzi kwa elimu ya juu.

Endapo sera pendekezwa itapitishwa na kuanza kutumika, tumeangalia intaathiri vipi huo muingiliano wa elimu na mifumo ya nchi nyingine? Au kwa vile waleta sera watoto wao hauta wa athiri?
 
Walichofanya ni kukopi mfumo wa UK ambapo hakuna mitihani kuanzia primary mpaka secondary form four (but then private sector zao zinazotoa viongozi wa taifa leo na vipanga kwenye nchi ya madaraja; do things differently, mpaka fimbo wanachapa zingine).

Ukirudi kwenye public sector wanafunzi wanapimwa kwa uelewa at each level, ukifika muda wa kufanya mtihani wa form 4 wanafunzi wanakuwa wamewekewa level ya mtihani kutokana na uwezo wao,

kuna mitihani mingine aina A+ hata upate sahihi maswali yote. Sijui kama ni exactly in the end lakini it looks that way, ndio ma-Phd wetu nyenzo si wanafunzi tu pia kwa ma-Prof wao maana hapa kama sio kukosa creativity sijui tuite nini.

Eitherway tuna matatizo makubwa sana kwakuwa kuna ma-Professor ambao tumeshawasikia wakilalama kuhusu haya mambo ya elimu na mitaala huko walipo kwa sasa watakuwa vichwa vinawauma kwa kukosa kuwepo kwenye hii system isiyo eleweka kwa sasa.

Hoja kubwa ya Professor mmoja niliowahi kumsikia kutoka UDSM kitengo cha mafunzo ya elimu ni mitaala inayoendana na changamoto za taifa hili kukidhi skills za wakati tulipo (ina maana si vibaya mitaala ikiwa inafanyiwa review after two to three year).

According to the Prof serikari kwa sasa aija harmonize elimu na uhalisia wa mazingira yetu ya kijamii na uchumi kukidhi changamoto. Mfano kuna faida gani ya kufundisha wanafunzi zaidi ya miatano sociology wakati ajira zenyewe hakuna ni waste of resources; both financial maana wanalipiwa na human capital kwa sababu wakimaliza shule wengi hawana ajira.

Kwa madai yake serikari lazima ijue tunahitaji nini kwenye elimu kwa sasa kwa faida za kuchochea uchumi, mahitaji ya wafanyakazi wa serikari na sector binafsi na wanafunzi walengwe huko. Kama ni degree za uchumi au biashara kwanini nyingi zisilenge kwenye fursa za kilimo kama biashara na mambo mengi yenye ku-reason kutokana na uhalisia wetu wa mambo. Kipi kingemsaidia mwanafunzi kwa leo sociology baada ya kumaliza shule au elimu inayo ona fursa kwenye kilimo kilimo na biashara?

Kuna watu ukiwasikiliza kwakweli wanaona mbali sana, hata ukisoma riport za CAG unajiuliza hawa watu ndio pekee walioilewa F8 auditing module au vipi.

Iweje wakiwa nje wanaona wakiwa ndani wanageuka vipofu, kwa sasa Utoh ni mmoja kati ya watu wanaojua matatizo ya administration ya serikari kuliko watu wengi serikarini mchango wake sijui kama umetumika na watunga sera za elimu hili kufundisha wanafunzi sahihi.

Tuna ombwe la uongozi kwa sasa na maarifa; JK kaifungua serikari tuione kama ilivyo mahala tulipo ni kwa sababu ya watendaji sanasana maafisa wa serikari are unqualified or poor expreinced; lakini wapo wenye uwezo wa kutubadilishia mambo na wenye maoni ya za namna sahihi kwenye kutuongoza na wasomi wenye mawazo mbadala ya kutengenza vijana wenye elimu ya leo na kesho kwa faida ya Tanzania.

Sasa kizungu chenyewe kasheshe, wewe tena ukakifute utegemee wataalamu watakaoweza mudu jargon za lugha kwa miaka mitano ya elimu ya mwisho, hata sijui huwa wanafikiria nini.
 
Sasa hivi hakuna kusoma nje. Hakuna vyuo vikuu vinasomesha watu kwa kiswahili duniani. Itakuwa ni vvuo vikuu vya kata ambavyo ni vya hapa hapa tu.

Watakaokuwa na hakika na uwezo wa kusoma nje ya nchi, ni watoto wa matajiri na watawala ambao hawatasoma kwenye huu msaragambo!.

Tanzania Kwisha habari yake.


Kwa mfumo uliokuwepo, ilikua ni rahisi kukubaliwa na vyuo vya nje ya nchi kwa elimu ya juu, nchi nyingi hasa zinazofuata mfumo wa uingereza zilikua zinatambua na kuwapokea wanafunzi kwa elimu ya juu.

Endapo sera pendekezwa itapitishwa na kuanza kutumika, tumeangalia intaathiri vipi huo muingiliano wa elimu na mifumo ya nchi nyingine? Au kwa vile waleta sera watoto wao hauta wa athiri?
 
Mie sio sehemu ya maamuzi haya, but ni mdau kidogo naweza kuchangia.
1. Form 5 na 6 utakuwrpo kama kawaida. kilichobadirika ni mfumo tu yani kutoka 2yrs for kindergaten, 7yrs kwa primary edn na 4yrs olevel, 2yrs kwa Alevel na 3+ for tertiary edn (2-7-4-2-3+ structure) kwenda (2-10-2-3+ structure)

2. Kufel nadhan kupo kama mtihani wa darasa la saba ukifail na f2 unarudia,

3. Shule ulizozitaja zitafundisha wanafunzi kama hao waliopo sasa. lazima wafanyiwe sreening kutokana na ufaulu wao.

4.Mfumo wa udahili hauwezi kuathirika kwa mabadiliko haya. watadahiliwa kwa sifa kama za sasa.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Tabby
Afadhali umenielewa mkuu. Kwa hiyo hapo mtu ukitaka kumponya mwanao inabidi umsomeshe nje kuanzia chekechea!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu chichimizi nashukuru kwa masahihisho.

Natumia kamchina, nipo mbali na ushahidi wa andiko hilo, hopeful keshi nitakubandikia hapa.
 
Malalika
Mfumo huu naona umekaa vizuri. Cha msingi mtaala uundwe katika msingi wa kumjengea mwanafunzi uwezo wa kujitegemea mara atakapohitimu.
 
Last edited by a moderator:
Mfumo huu naona umekaa vizuri. Cha msingi mtaala uundwe katika msingi wa kumjengea mwanafunzi uwezo wa kujitegemea mara atakapohitimu.

Hilo ulilosema ndio la Msingi kabisa kuliko yote.
 
Malalika

Practical oriented education depends on curriculum mkuu, kipindi cha ujamaa (education for self reliance) Elimu yetu ilikuwa bora kuliko hiki cha kwenu BRN.

Nipe mcahanganuo wa Curriculum na Syllabus zenu are transitions? If yes, we're is the Education and Inequality emerged from? And why?

Tatizo sio kuongeza kufumua bila kujua jinsi ya kurudishia, inch jamaa amefikisha pasipo na anataka kuipoteza kabisaa
 
Last edited by a moderator:
Wadau nashauri tuisomeni kwanza Sera yenyewe,coz Sera ni km dira au guide inayokuongoza wakati wa kupanga utekelezaji,tuisome na tusubiri mikakati watakayo kuja nayo kuitekeleza hiyo sera. Japokuwa hofu yangu sijui km kale kamchezo ka kupanga vizuri na kutokutekeleza kameisha.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako mkuu, hofu yangu ni hizi shule za kata, kama primary ni hadi darasa la 10 (Ngumu kuitaja) ko hizi za kata zitakuwa Advance zote?

Nini intention ya serikal hasa? Wanataka niamini kwamba Elimu tuliyo nayo ni bora sana kiasi kwamba Wanataka tuwe bora zaidi? Je jamii imehusishwa? Au ni Order from the Top? Are we after skills or certificates?
lengo ni kuvuruga akili za wadanganyika.
 
MALALIKA

Hakuna kituvkinachoitwa shahada katika ualimu bali ni shahada ya elimu.

Then tunaomba muongozo wako wenyekuonesha kwamba mwalimu wa diploma anatakiwa kufundisha form one na two.
Then shahada afundishe three hadi six.

Tupatie ushahidi wa kudhibitisha kauli hiyo

usiwe mvivu. tafuta mwenyewe sera ya elimu ya 2006 na Education act. maelezo uliyopewa ni sahihi.
 
Nahisi nipo usingizini na nimekosa cha kuongea ila 2015 watanzania tufanye maamuzi magumu sana tusiangalie sura na rangi tunahitaji mabadiliko
 
Back
Top Bottom