Mtihani wa geography wafutwa!!

Mtihani wa geography wafutwa!!

Ni kitu kimoja kibaya sana na ambacho nilimweleza Dr Mapunda nilipouona kwa mara ya kwanza mtihani uliovuja 1987.Elimu ni namba moja na bila elimu taifa halipo.Taifa bila elimu ni sawa na upofu.Hutaenda popote mpaka ushikwe mkono.
Wakubwa ni kwamba pepa zinavuja kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu, na hii kitu haijaanza leo. Kilichobadilika ni teknolojia ya habari tu, kwa hiyo hata wasio kwenye mtihani wanapata habari. Zamani hizi habari ziliishia huko mashuleni, na wale ambao hawajafanya mtihani walitunza siri ili hiyo "channel" ya pepa iendelee kudumu zamu yao ya kufanya mtihani ikifika nao waitumie. Mitihani ya kuvuja ilikuwa na majina mengi kama "nondo", "kirungu", kule chuo kikuu mlimani waliita "desa", Muhimbili waliita "mwezi" nk.

Wavujishaji wakuu wa mitihani wako katika makundi kadhaa:
1. Wafanyakazi wasio waaminifu wanaotaka kujipatia fedha kwa kuuza mitihani. Hawa wako katika sections mbalimbali katika process ile ya kuandaa mitihani kuanzia uchapaji, kurudufu, kufungasha, kusafirisha nk. Na hawa ni ngazi zote, shule ya msingi hadi university. Uzuri ni kwamba hawa ni rahisi kuwadhibiti kwa kuziba mianya yote na kuweka kanuni za usalama zinazozingatiwa na zinazoji-monitor zenyewe.
2. Kundi la pili ni la wamiliki wa mashule na wakuu wa mashule wanaotaka kujenga sifa kuwa shule zao ni bora. Hawa hununua mitihani kwa gharama yoyote na kuifundisha mashuleni, na wala huwa hawaoni aibu kuwaambia wazazi waongeze michango ya "special tuition" kwa ajili ya watoto wenye mitihani (form 2, 4, 6). Kinachowawezesha hawa kufanikisha hii ni kupenyeza vigogo wa baraza la mitihani kwenye payroll za shule zao, kwa hiyo hizi paper zinatoka kwa wakuu wa Baraza la Mitihani, wale wenye dhamana ya mwisho kabisa ya kuaminiwa (actually wale wanaodhibiti wizi wa mitihani ndio wanaopelekea hawa jamaa hizo pepa). Mitihani ya namna hii inapovuja si rahisi kuonekana mizimamizima maana wahusika huwa wanakabidhi maswali kwa waalimu wa masomo, ambao wanayafundisha darasani kama "revision" za kawaida, kwa hiyo si rahisi kuwastukia. Tatizo linatokea wanapomkabidhi mwalimu paper nzima na yeye ana tamaa ya pesa, anauuza kwa dalali (au madalali) ambao wanaanza kuutembeza kama njugu, hapo ndio "soo" linabumburuka!
3. Kundi la tatu ni wazazi wenye influence huko baraza la mitihani ambao wanaiba mitihani hiyo kwa ajili ya watoto wao. Hawa pia ni vigogo, na huipata kutoka kwa vigogo wa baraza. Anapofikisha mtihani nyumbani anamkabidhi mwanae anamwambia "ushindwe mwenyewe sasa!" Ikitokea mtoto hajiamini, anatafuta rafiki (au marafiki) anaoamini ni "kipanga" katika kila somo ili wamfundishe (siri imeanza kutoka hapo). Wakimaliza kufundishana, wanakumbuka "unajua tunaweza kutengeneza hela hapa?" Wanaanza biashara kuuzia wenzao.

Udhibiti wa mitihani unatakiwa uanze kwanza na vigogo wa baraza la mitihani, maana hawa wengine wa chini wanaumiza vichwa kulinda mitihani ambayo ilishavuja kabla hawajakabidhiwa!

(BTW hii ndio ilikuwa proposal yangu ya awali kwa ajili ya tasnifu yangu ya masomo ya uzamivu, lakini kutokana na "siasa" zilizomo ndani yake niliiacha maana uwezekano wa kuifanikisha ulikuwa mdogo sana. Changamoto kwa anayeipenda aichukue, awe jasiri!)
 
Huko baraza la mitihani hamna kitengo maalumu knichomonitor utolewaji wa mitihani?Swali lingine la kuuliza jee ni baraza ama mashule yenye headmaster wasroho wa fedha?
He!we kevo,hicho kitengo huko NECTA kikidhibiti watoto na watoto wa watoto wao wafaulu vipi?na mashemeji zao je?Hata 'madedimasta' pia wale wapi wakati mishahara yenyewe ya ubabaishaji.Tanzania kila kitu ubabaishaji.Hata wale ambao wamefaulu vizuri na wangepaswa kwenda nje ili warudi na utaalamu wamejazana pale UDSM na Mzumbe.Nafasi zao wale watoto wa wakubwa walishapewa hata kabla matokeo kutoka.It doesnt matter what you know but Whom you know
 
Ieleweke kwamba siikatai elimu yetu hata kidogo.But system inatuua and we real need experts.Juzi nilikuwa pale kuna mwanafunzi finalist fourth year hata kujieleza kwa kingereza hawezi! Na akinyimwa ajira,malalamiko.SOMETHING MUST BE DONE
 
Mzee wa Gumzo; hizi habari zilitolewa na nani; maana ni habari ambayo baada ya kazi niliitegemea badala yake ni kitu tofauti kabisa; kama mtu huna taarifa za maana kwanini udanganye umma huu wote; hii sijapenda andika kitu ambacho una uhakika nao; Mzee wa gumzo kili kuwa ulidanganya jana kuhusu hii habari sasa usamehewe
 
Back
Top Bottom