Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
BAADA ya kurudiwa kwa mtihani wa Hisabati wa kidato cha nne, mtihani huo ulivuja tena na ushahidi wake ni kwamba wanafunzi wawili wa kidato cha nne wanashikiliwa polisi mkoani Dar es Salaam kwa kukutwa na majibu ya mtihani huo ndanin chumba cha mtihani.
Waliokamatwa na polisi ni Hidaya Issa (19), aliekuwa na namba S.844/078 na Salima Ally(18) aliyekuwa na namba S.884/079 wakiwa ni wanafunzi wa shule ya sekondari ya seminari ya Thagalaini iliyopo Mbagala Chalambe,Dar es Salaam.
Walikamatwa Octoba 27, 2008 saa 4:20 asubuhi siku ambayo mtihani huo wa hesabu ulifanyika na walikamatwa na msimamizi wa kituo hicho Leila Hamadi(50) wakiwa na majibu ya mtihani huo.