Mtihani Wa Kenya Kidato Cha Nne - Ungepata Maki Ngapi?

Mtihani Wa Kenya Kidato Cha Nne - Ungepata Maki Ngapi?

MwendaOmo

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2013
Posts
774
Reaction score
723
Nina shahada ya Kiswahili ya UDSM lakini huu mtihani ni changamoto kwangu, MwendaOmo!
 
Last edited by a moderator:
Sasa utakuwa nifanye mtihani wa Kenya ilihali sijasoma Kenya, kumbuka syllabus ya Kenya ni tofauti na ya Tanzania.
 
Sasa utakuwa nifanye mtihani wa Kenya ilihali sijasoma Kenya, kumbuka syllabus ya Kenya ni tofauti na ya Tanzania.

Ni mtihani wa Kiswahili ndungu..wajua waTZ wamebobea Katika Kiswahili. Nina uhakika ukipewa Mtihani wa Marekani wa Hisabati utaweza fanya (Ikiwa hiyo ndio area yako.)
 
Hizi ni baadhi ya Mitihani ya Kenya Kidato cha Nne. Jee, Kwa maoni yako ni rahisi kushinda uliyofanya na ungeweza pata Maki ngapi?

Ni Mtihani wa 2013 wala sio 2014. Kwa kuwa wengi hapa JF ni waswahili, Tuanze na Kiswahili Paper 1 ni Insha, Paper 2 ni Lugha, na Paper 3 ni Fasihi

Kiswahili ni lugha yangu ya kila siku ila hiki kiswahili cha kwenye huu mtihani anakiweza Bakita tu.
 
Last edited by a moderator:
INAFANANA NA HII
Tar 1/11/2014 Wanafunzi Wa Mwaka Wa Kwanza Wote Wa SUA tumefanya mtihani wa kiingereza
(utaratibu uliowekwa na chuo kama ukifeli utafundshwa hadi ufauru,ukifauru husomi hilo somo) cha kushangaza kati ya wanafunzi waliofeli yumo mzungu ila sidhani kama anatoka uingereza.
 
mimi nimeipenda kwanza wanavyotenganisha, inamupa mwanafunzi muda wa kutosha na kufikiri katika jambo moja

lakini huku kwetu vitu vyote wanaviweka katika mtihani mmoja.
 
Hebu ipachike hapa tukainoe. SUA ni?
 
mimi nimeipenda kwanza wanavyotenganisha, inamupa mwanafunzi muda wa kutosha na kufikiri katika jambo moja

lakini huku kwetu vitu vyote wanaviweka katika mtihani mmoja.

DUH! Fasihi, Lugha na Insha yote pamoja? Yanachukua masaa mangapi? Hata mtihani wa darasa la nane hatuchnganyi Insha na Lugha
 
Hapo zamani bongo mitihani ilikuwa na hadhi kama hii kwani ulikuwa unaletewa habari ambayo unaisoma mwanzo mwisho uielewi iwe ya kiswahili ama ya kiingereza lakini baada ya ujio wa BIG RESULT NOW watoto wanapwewa maswali rahisi sijapata ona
 
kiukweli tz tunafanya masihara na lugha yetu,nawasiwasi hata hao baraza la mitihani la Taifa la Tz ukiwa huu mtihani watashindwa kuujibu au hawatakua na uhakika kama ni mtihani wa form 4,rudisheni elimu yet mahali pake,HAKI ELIMU mna kazi kubwa sana kuikosoa,kuilimisha na kuihabarisha mnlaka husika juu ya kudorora kwa elimu yetu.
 
Si mtihani mgumu sana isipokuwa unapima viwango vya juu kama uwezo wa kuchambua na kuchanganua (analysis) n.k. Mtihani haumlengi mzungumzaji wa Kiswahili bali msomi na mtaalamu wa kiswahili.
 
Ikumbukwe pia huko Kenya mhitimu wa kidato cha 4 huingia chuo kikuu moja kwa moja. kwa hivi ni vizuri kulinganisha mtihani huu na ule wa kdato cha 6 tz
 
Kuna yeyote anayeweza kupata soft copy ya mitihani ya TZ hapa? Nngependa kuona Kiingereza, Kiswahili, ya kidato cha nne, na mitihani yote ya darasa la saba.
 
Back
Top Bottom