Wakuu,
Labda tujiridhishe kidogo, kuna njia nyingi wakati wa kusahihisha mitihani zinazosaidia kujua wanafunzi ambao wamefaidika na kuvuja kwa huo mtihani. Kikawaida inatakiwa
wasahishaji waweze kuondoa effects za kuvuja kwa mtihani.
Mara nyingi wanaofaidika na kuvuja kwa mitihani ni wale wanafunzi wenye uwezo mkubwa; aliye nacho huongezewa. Wale wa chini, kuna njia za kuhisi na hivyo kuwashughulikia.
Mimi wakati nafanya mtihani wa form six, paper mbili zilivuja, ambazo hata mimi niliziona. Physics ikaangukia kuwa sio kweli, tulipofungua paper, watu wakaanza kupumua kwa nguvu zote. Ni kwamba watu wakaponzeka. Paper nyingine ilikuwa Chemistry, hii ilitoka kama ilivyovuja.
Matokeo yalipotoka kwa shule husika ilikuwa ni reflection ya uwezo wa watu. Kuna watu walichukua F hata kwenye Chemistry. Siamini hao watu walipata F maana baada ya kuona paper hata kama wali panic bado wangetoka japo na D.
Kwa sisi tuliosoma shule za shamba na kisha kusoma A-level shule za Dar, hilo lilikuwa jambo la kusikitisha sana. Lakini cha kufurahisha, hiyo miaka pamoja na kuvuja mitihani mjini, bado sisi watu wa kule shamba kwenye O-level bado tulikuwa tunatesa.
Ushauri ni kukaa chini na kusoma bila kufikiria kuna watu wanaweza kupata mtihani.