Nimeisoma thread hii imenikumbusha mbali kweli. Kuvuja huku kwa mitihani sio leo wala jana, ni long time tu. Imenikumbusha jinsi pepa zilivyokuwa zinakuja camp yetu kushushwa. Kuna wale waliokuwa waandaaji wa mapicnic, mabitozi, masista du, wao class hazipandi kabisaa wanasubiri mpaka time time, wanatafuta pepa then wanatuletea kuzishusha. I can say 90% of the time zilikuwa za kweli, walikokuwa wanazipata sijui na tulikuwa na "Dont ask dont tell" policy. Hatuulizi zimetoka wapi na wao hawasemi, lakini ndio hivyo tena pepa zinashushwa, na wengi wao walikuwa ni watoto wa vigogo.
Hadi siku moja mdingi akanitilia shaka, akaniuliza mbona kipindi cha mitihani kunakuwa na mishemishe nyingi? Mbona trafic inakuwa kubwa hapa? As you already know, niliruka futi saba wa sabini nikakanusha. So my point ni kuwa uzembe upo, umasikini upo, uvivu upo na vyote hivi vinachangia pepa kuwepo mtaani kabla ya wakati wake.