Ndio maana nawashangaa sana wakenya wenzangu, ambao tayari wameshatoa mashati kabisa. Wakiashiria wazi kwamba watafunga mabao upande wa pili, yaani kwenye goli la waliovalia mashati. 😄
Naamini kwamba chaguo la mgombea-mwenza, kutoka kwa wagombea urais wote, ni jambo ambalo linafaa kutazamwa kwa umakini mkubwa. Watu hawajajifunza, kutoka kwa mengi tuliyoyaona kwenye utawala huu wa rais UK. Ugomvi, malumbano, maigizo, 'makasiriko', yote tumeyashuhudia, kati ya rais na naibu wake.
Katiba ya Kenya 2010 ilituletea NAIBU rais, umakamu, ukimya na unyenyekevu wa ovyo ukaishia hapo. Sasa hivi kiti hicho kina hadhi, ushawishi, mamlaka sawa na ya 'co-president'. Tunangoja, ni wazi kwamba atakayeteleza kwenye hili ndoto yake ya kuwa rais itapata pigo kubwa kupindukia. Tena punde tu atakapomtangaza rasmi mgombea-mwenza wake.