Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
KAZI KWELI KWELI
Mtikila Adai Kakobe ni Nabii wa Uongo, Amtaka Akae Kimya
Mchungaji Mtikila Saturday, April 18, 2009 4:43 AM
Mchungaji Mtikila ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha DP amemtaka Askofu wa Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe kutulia kimya kwani Kakobe anajulikana ni nabii wa uongo na mengi yanayomhusu yeye na kanisa lake yanajulikana
Mtikila aliyasema hayo alipotakiwa kujibu hoja ya mwandishi mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa.
Swali, Wewe na Kakobe wote ni wachungaji wa kondoo wa Mungu inakuweje mkapingana maana yeye hivi karibuni alisema DECI ni ya shetani na wewe unasema kuwa ni sehemu ya ukombozi wa mtanzania je hili likoje
JIBU, Kakobe yeye anajulikana maana anaposema DECI inashirikiana na mashetani wa kuzimu je yeye ameshawahi kufika huko, lakini hatushangai kwa Kakobe kwani hata waumini wake wanajua anavyowaongoza kwa maana inafikia hata kuwalazimisha wavue heleni za Dhahabu wampe yeye kama sadaka pia hupita nyumba hadi nyumba kuorodhesha mali za waumini ili wamtolee yeye, Yote haya si mambo mageni kwa Kakobe.
Pia ni nabii wa uongo Maana alitabiri kuwa Mrema atachua Urais lakini hakuchukua ,pia kipindi kingine alisema Mrema asipokuwa Rais anaacha kazi ya Uaskofu je ameacha?.
Mtikila aliyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa habari juu ya Taasisis ya DECI ambayo imekuwa gumzo katika jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Deci imeweza kujizolea umarufu mkubwa kwa kuwajaza mapesa watanzania wenye kipato kidogo kwa kutumia kauli mbiu isemayo Panda Mbegu Vuna mbegu ambapo ukipanda Shilingi 200,000. unavuna 500.000 kila baada ya miezi 4.
Hivi karibuni serikali ilitoa tamko kwa wananchi kuwa Deci haina vibali na inaendesha shughuli zake kama upatu jambo ambalo linaweza kuwasababishia hasara.
Na Kaimanzila, Dar
Mtumie Rafiki Yako

Last edited by a moderator: