Mtikila Adai Kakobe ni Nabii wa Uongo, Amtaka Akae Kimya !!!


Pdidy,
Kwanza nakili nimeokolewa na Bwana Yesu mwenyewe.
Na mimi nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa.
Mungu atusaide kujua haya.
Amen.
 
wengi walimjua Kakobe na habaro walizo nazo ni zile ziliandikwa na magazeti ya Shigongo wakati ana bifu naye,. Lakini leo hapa JF tumeona Magazeti ya Shigongo yalivyoleta madhara kwa watu mbali mbali, Je, Tuzidi kuamini zile habari za Kakobe kuwavua wanawake dhahabu? Mimi nasema hata mahakama mtu hutoa ushahidi wa lile alilowahi kuioona au kusikia yeye mwenyewe, sio kuambiwa! Sasa watu ambao hamjawahi kuwakaribu na Kanisa la Kakobe mnayajuaje yanayoteokea huko Ndani? Mimi sio Mfuasi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, lakini nakiri kuwa niemshiriki ibada mara nyingi sana kwenye kanisa hili, sio Dar tu hata Mikoani,. Naweza kushuhudia yale niliyoyaona, na kamwe sitashuhudia lile ambalo sikuliona kwa macho yangu, tujiangalie sana, Kuwaonyoshea mikono watumishi wa MUNGU kwa tuhuma zisizo za kweli Biblia Imakataza!!!
 
Mkuu naifaham ARK FOUNDATION aFRIKA, halijawahi kuanzishwa wala kuhudumiwa na Mtikila. Jamaa makao makuu yapo marekani na wanatoha huduma kwa marginalized children hasa wale ambao wameathiriwa kwa namna moja au nyingine na UKIMWI. nilishawahi kuwa volunteer wa shirika lile ila wakiwa wanatoa huduma za kijamii wala hawabagui watu kwa udini wao. Mara ya mwisho walikuwepo nyuma ya ubalozi wa USA na walikuwa wanajiandaa kuhamia kigamboni na wanalo tawi kule Kibamba ambapo pia wameanzisha shule ya vidudu.
Niliwahi kuongea na mkrugenzi mkazi wa ArkFoundation Ms Rhoi Kaima alisema anamfaham Mtikila na hawana hamu naye maana aliwaingiza mkenge kutokea marekani.
 
Japo ninamuunga mkono Rev Mtikila la kusema kuwa Kobe-mdogo ni mzushi na anawalakini katika dili lake la kutumia biblia, hata hivyo si-muungi mkono kuhusu DECI. Nadhani Rev anataka ku-support hii DECI kwa kuwa imebuniwa na wachungaji wenzake, lakini kitaalamu hana hoja sana ya kuisemea DECI. Hivi, kweli Mungu anaweza kuwaletea watu "kamali" kwa jina la DECI. Maana hata kamali pia unapanda na kuvuna, na wakati mwingine mbegu haioti kabisa.
 
Lakini kakobe anavyoubiri (TV) kuna "flow of Logic" ukilinganisha na wenzie wengi, anajitayarisha na kutoa kitu sahihi. Lakini baadhi ya Shuhuda za wauminini wake ni utata / usanii mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…