Mtikila aibua mapya tume ya katiba

Nami namkubali sana Rev Mtikila ana akili zilizo juu sana ya wastani ya wanasiasa wengi sana EA.,ilikuwa namsubiria aje atupe changamoto zake za katiba mpya!pia jamaa anajisomea sana na ana upeo mkubwa sana!basi tu system inamsumbua akipate wasaa wa kung'aa
 
Safi sana hasa kwa hao viti maalum wanakula ela ya bure kabisa!
 
Uzuri wa Mtikila ni miongoni mwa viongozi wachache wa dini ambao wanapokuwa katika majukwaa ya kitaifa wanaangalia TAIFA KWANZA badala ya dini yangu; wanaangalia WATANZANIA KWANZA badala ya waumini wangu; wanaangalia UZALENDO KWANZA badala ya udini.

Pamoja na udogo wa dhehebu analoliongoza, pamoja na uchanga wa kanisa ambalo yeye ni kiongozi; kanisa ambalo mizizi yake ni mifupi mno; haiendi hadi Ulaya au Uarabuni kama madhebu mengine ambayo hayaishi kulialia kinafiki wakiwa na ajenda zao za siri bado Mtikila hajitambulishi kama kiongozi wa dini yanapokuja masuala ya kitaifa.

Nchi hii tunaye adui mmoja tu wa taifa letu na Mtikila ni miongoni mwa viongozi wachache wa dini wasiokuwa wanafiki na wanaomjua vilivyo adui wa taifa letu. Laiti viongozi wetu wa dini wangekuwa kama Mtikila.
 
maoni mazuri kama haya maccm hawayataki kuyasikia na yatachuja tu maccm
 
Japo ni kawaida kuwa sheria inapokuja mpya huwezi kuitumia sheria hiyo kuwashtaki wale waliotenda makosa kabla ya hiyo sheria lakini kwenye hili katiba itamke wazi kuwa, 'hata wale Marais waliotangulia kama katika vipindi vyao walitenda makosa ya jinai wataweza kushtakiwa.

Mimi ningependa jambo moja liongezwe kwenye katiba ili kuondoa uonevu na kupunguza rushwa katika jeshi la polisi kuhusiana na makosa ya jinai. Mtu yeyote aruhusiwe kufungua kesi ya jinai dhidi ya mtu au chombo chochote, siyo lazima iwe ni jeshi la polisi tu. Polisi wameitumia nafasi hii vibaya kiasi cha kuamua nani wamshtaki na nani wasimshtaki kwa makosa gani.

Naunga mkono hoja zote na hasa hili la kuondoa kinga baada ya urais kumalizika. Hii itawafanya wahusika kuwa na adabu wawapo madarakani!
 

Excellent point! Na upelelezi uendeshweje? Na Polisi hao hao au kuwe na vyombo vingine huru (au hata watu binafsi) vyenye mamlaka kikatiba kufanya hivyo? Tatizo la msingi linaanzia kwenye upelelezi na ndipo hoja za kipuuzi kama kukosekana ushahidi, kubambikiwa kesi, n.k. yalipoota mizizi.
 
mchungaji mtikila ana points kweli .... Ni baadhi ya mawazo niliyochangia kupitia kwenye mtandao wa tume .... Tusubiri tuone vituko tu ni nini kitapita!
 
Ana hoja, Tume izingatie maoni ya huyu kamanda.
 
Mchungaji mtikila amekua na uwezo wa kuleta msisimko wa kizalendo katika namna anavyotoa mawazo yake. Kinachonisikitisha ni hali yake ya kukosa "consistance" katika uwepo wake kama kiongozi wa kisiasa. Anapoteapotea na kukurupuka na hoja. Ni vigumu kumchukulia kama kiongozi makini wa kisiasa. Hoja zake za leo zinamashiko.
 
Mtikila nae jembe sana.
Ana fikra zilizonyooka kama Zitto kabwe.
 
Wananchi wametoa na wanaendelea kutoa maoni mazuri tu,wasiwasi wangu je tume na serikali tawala itayakubali?
Kwakuwa mengi ni kisu kikali kwa watawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…