Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
taifa linahitaji viongozi bora na siyo kustarehesha jinsia".
Naunga mkono hoja zote na hasa hili la kuondoa kinga baada ya urais kumalizika. Hii itawafanya wahusika kuwa na adabu wawapo madarakani!
Japo ni kawaida kuwa sheria inapokuja mpya huwezi kuitumia sheria hiyo kuwashtaki wale waliotenda makosa kabla ya hiyo sheria lakini kwenye hili katiba itamke wazi kuwa, 'hata wale Marais waliotangulia kama katika vipindi vyao walitenda makosa ya jinai wataweza kushtakiwa.
Mimi ningependa jambo moja liongezwe kwenye katiba ili kuondoa uonevu na kupunguza rushwa katika jeshi la polisi kuhusiana na makosa ya jinai. Mtu yeyote aruhusiwe kufungua kesi ya jinai dhidi ya mtu au chombo chochote, siyo lazima iwe ni jeshi la polisi tu. Polisi wameitumia nafasi hii vibaya kiasi cha kuamua nani wamshtaki na nani wasimshtaki kwa makosa gani.
Mtikila nae jembe sana.View attachment 78955 MAKUNDI maalumu jana
yaliendelea kutoa maoni yao
kwenye mchakato wa Katiba
Mpya, huku DP kikipendekeza
Rais aapishwe baada ya siku 90
tangu kumalizika kwa Uchaguzi
Mkuu.
Mbali na maoni hayo
yaliyowasilishwa na Mwenyekiti
wa chama hicho, Mchungaji
Christopher Mtikila, makundi
mengine; wakulima, wafugaji,
wanahabari na Mtandao wa
Jinsia Tanzania (TGNP) nayo
yalijitokeza kutoa moyoni.
Mtikila alisema kipindi hicho
cha siku 90 kitatoa fursa kwa
watu wanaotaka kuwasilisha
pingamizi dhidi ya ushindi wa
Rais mteule kufanya hivyo, kabla
ya kuapishwa.
Alisema pingamizi linaweza
kufanyiwa kazi kwa kipindi
hicho cha miezi mitatu ili
kuhakikisha kuwa taifa linapata
kiongozi halali mwenye ridhaa
ya wananchi.
Pia tunataka kinga ya Rais
ikome pale anapomaliza muda
wake wa uongozi, kama alifanya
makosa yoyote ya jinai aweze
kushtakiwa ili kujenga nidhamu
ya uongozi katika ofisi ya
umma. Utaratibu wa
kumwondoa madarakani
uimarishwe asisubiriwe hadi
amalize muda wake wa
uongozi.
Alisema kuwa Katiba ya nchi
inapaswa kuwa mali ya
wananchi wenyewe ili watawala
wasijihusishe katika kuwaundia
wananchi Katiba kama ilivyo
kwa mchakato unaoendelea sasa
wa kupata Katiba Mpya.
Kumekuwa na hoja ya kuwapo
kwa Serikali ya Tanganyika, hilo
ni jambo muhimu na watu
kutoka Tanganyika ni lazima
wawe na Serikali yao ndani ya
mipaka ya ardhi yao kupitia
Katiba Mpya, alisisitiza
Mchungaji Mtikila.
Aliongeza kuwa nafasi za
wabunge wa viti maalumu
bungeni ziondolewe ili viti hivyo
vishindaniwe kidemokrasia.
Alisema wanawake wanatakiwa
waelimishwe na kupikwa ili
wahimili ushindani katika
medani za kisiasa. Alisema kuwa
taifa linahitaji viongozi bora na
siyo kustarehesha jinsia.