Mwanakijiji,
Mzee wangu umezungumza mengi sana kuhusu Lowassa na hakuna mtu alochoka kusoma malalamiko yako. Sii peke yako hapa JF kila siku tunarusha madongo na kukemeana tunapotaka kutoka ktk msitari.. huo ndio uhuru wa maoni, hata siku moja tusije fikiria uhuru wa maoni una include matusi toka kwa kiongozi mwingine wa chama.
Mzee Mkandara, kwenye suala la maoni ninaamini kuwa watu wana uhuru mkubwa ikiwemo kuita watu majina ya kejeli na hata ya dhihaka. Katiba inapolinda watu kuwa au kutoa uhuru wa maoni haisemi maoni hayo ni ya namna gani.
Linapokuja suala la matusi nchi nyingi duniani zinazosheria ambazo zinatakaza obsenities, na hapa mara nyingi mahakama zinahangaika kusema what is obsene.
katika Lugha ya Kiswahili vivyo hivyo tunayo sheria inayokataza matusi hadharani lakin haiorodheshi matusi ni nini. Kumuita Rais Mjinga inawezekana kuwa ni tusi na kwa wengine inawezekana kuwa si tusi. Ujinga ni sifa ya kuashiria uwezo wa mtu kujua jambo fulani. Mtu mjinga hajui, na ujinga hutoka. Kumuita mtu ******** yaweza kuwa tusi na laweza kuwa sifa ya kuelezea kuwa mtu huyo hawezi kujua hata akijulishwa vipi. Lakini, mtu anapotoa matusi ya nguoni ambayo lengo lake ni kumdhalilisha mtu kwa matusi ya "mama" au ya viungo vya mwili, ni rahisi zaidi kuona wapi mtu anapotoka.
Uzuri ni kuwa katika Lugha ya Kiswahili matusi yako very clear hayana ile ambiguity ya maana. Kama mtu si hanithi, halafu mtu mwingine akamuita ni hanithi, hilo ni tusi. Lakini kama mtu ni hanithi halafu akaitwa hanithi, haliwezi kuwa tusi.
Now, kwa upande wa Mtikila naamini charges zinazoweza kustick and as a matter of fact should stick ni charges za uchochezi hasa kama aliyosema ndivyo alivyosema. Kumuita Rais Mhuni he can get away with that. Ila anaposema.
Rais Gaidi - amevuka mstari wa matusi na kufika mstari wa madai ambayo atatakiwa ayaoneshe ukweli wake. Tanzania tunayo ile sheria ya Dhidi ya Ugaidi, je Kikwete anastahili kuitwa Gaidi. Hakuna nchi ambayo iko tayari kuongozwa na Gaidi, hivyo lengo la Mtikila kusema Rais ni Gaidi ni kuwafanya wananchi waichukie serikali na indirectly watake kuiondoa kwani kama kweli tunaye Rais Gaidi ni jukumu la wananchi kumuondoa Rais huyo hata kwa nguvu! Ndio maana charges hizo ni more serious (and should be serious) kuliko za kumuita Rais Mjinga.
Na anaposema kuwa lengo la Waislamu ni "kuwachinja wakatoliki" ni madai mazito hayo kwani ni sawa na kile ambacho Marekani kinatenganisha uhuru wa maoni na maoni ya hatari. Wenyewe Marekani wanasema ni sawa na "kupiga kelele 'Moto, moto' kwenye ukumbi wa sinema uliojaa watu". Yeye anataka Wakatoliki wafanye nini kujihami, wakikaribishwa na Waislamu wasiende na wakiona waislamu wanatambe mtaani na upanga kwenda msituni wajifungie ndani!
Ni kwa sababu hiyo utaona kuwa simtetei Mtikila hata kidogo kwani ninaelewa vizuri sana maana ya uhuru wa maoni na mipaka iliyopo. Ndio maana utaona kuwa katika makala zangu zote ninawaelezea viongozi wa nchi kwa jinsi walivyojieleza wao wenyewe au kutokana na mambo waliyoyafanya. Sijawahi kumuita kiongozi yeyote jina lolote ambalo si la cheo chake au hata la utani (kwa mfano, ingawa wengi hapa wanapenda kumuita JK "Muungwana" miye siwezi, ninamuita Rais Kikwete). Siku akifanya mambo ya woga nitamuita mwoga, akifanya mambo ya kijinga nitamuita mjinga, hata Lowassa mara nyingi nasema ni "kiongozi mahiri, hodari, shujaa aliyetamba Bungeni" ambalo ni kweli!
Jibu la yote haya ni kwamba mahakama hizi hazitufai hata kidogo ila tunaweza kumtumia Mtaalam wa sheria hizi kama atahitajika...Na sidhani kama kuna nafasi hiyo.
Mkandara katika sehemu ya pili ya Makala yangu ninaelezea ni jinsi gani tunaweza kuanzisha mahakama ya Kadhi Tanzania Bara pasipo kuwa na hofu. Kama India wameruhusu kuwa nazo (japo hazitambuliki kisheria) na kama Waisraeli wameruhusu (na zinatambulika kisheria) nadhani Tanzania tunaweza kuwa nazo pia. Cha kushangaza Uturuki (nchi yenye waislamu wengi) haina mahakama za kadhi! Upande mwingine Indonesia taifa lenye Waislamu wengi zaidi duniani halina mahakama ya kadhi kama tunavyoifikiria sisi. So in essence there is a wide range of models of how we can establish Qadi courts without contravening the Constitution or other laws. Tatizo inawezekana tutahitaji wataalamu toka nje kutufikiria jinsi tunaweza kufanya hivi kwanini sisi wenyewe hatuwezi kufikiri vya kutosha na ni waoga kulifikiria jambo hili na kulipatia utatizo wa Kitanzania.