Mtikila amshutumu rais, polisi, usalama

Mtikila amshutumu rais, polisi, usalama

Status
Not open for further replies.

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Joined
Apr 21, 2008
Posts
197
Reaction score
5
Katika hatua nyingine ya mlolongo wa matukio ya kushangaza kumhusu Mtikila,Mchungaji huyo amekanusha waraka uliosomwa ITV kuwa haukuwa wake.

Hata hivyo chakushangaza zaidi Mtikila amemtuhumu Rais Kikwete, jeshi la polisi na Usalama wa Taifa.Taarifa hiyo ya Mtikila haikuweza kurushwa hewani kutokana na maneno na kauli zake kutoweza kuvumilika masikioni na.

Binafsi nimeyasikia maneno ya Mtikila na haiwezi kuingia akilini kuwa Mtikila anaweza kuwa mzima wa akili.

kuna kila sababu ya kuamini kuwa Mtikila anatumia siasa kucheza na akili za watanzania kwa kuwa haiingii akilini kuwa anaweza kutoa shutuma nzito kwa maneno mabaya kiasi hicho kwa ongozi wa nchi na vyombo vya dola ambavyo awali alivitegemea kwa ulinzi.Amehamisha asira zake kutoka CHADEMA kwenda kwa serikali.

Hivoi bado tunamwamini Mtikila???
 
naomba uandike hapa hiyo taarifa ya mtikila, hata itv wanasema hawawezi kuisoma, hapa jf hatufungani na upande wowote tuipate live kabla hatujashauri apelekwe isanga psychatric insitute kule dodoma
 
Mtikila ni mwendawazimu na pia ni ndumilakuwili. Alistahili kudharauliwa na kutosikilizwa na umma wa Watanzania tangu pale alipoanikwa hadharani kwamba aliomba michuzi kwa fisadi Rostam.
 
Samahani mimi naomba kwama unaweza kutumia tafsida kutuelezea aliyoyasema huyo mwehu?na JK kaingiaje tena?Hizo tuhuma zimetolewa lini?

Kevo nahitaji muda kutafuta tafisida,
Lakini kwa ujumla amewatukana ITV,RAIS,POLISI NA USALAMA.
Amedai kuwa polisi na usalama wameshindwa kufanya kazi yao namatokeo yake ni halimbaya ya usalama huko Tarime ndiyo maana na yeye alipigwa mawe.

Amewatukana ITV kwa madai kuwa wanatumiwa na CHADEMA.Katika hali ya kustaajabisha Mtikila amechukua sheria mkononi kwa kuwaadhibu wale anaoona wako kinyume chake.Katika mTUSI YAKE Mtikila amejifananisha na mtume ambaye yupo katikati ya kundi la simba wala watu na kuwa siasa za Tanzania zimejaa unafiki na uongo.

Kwake kitendo anachodai cha kughushiwa saini yake amekiita kuwa kimepata baraka za polisi na usalama na kuwa hata Raisi wa Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania.Amemshutumu Rais kwa maneno makali kuwa utawala wake umejaa ubabashaji wa hali ya juu na kuwa nchi ipo ipo tu.

Kwa ujumla bado inakuwa ngumu kuweka matusi hadharani hapa
 
Ndio maana sitachoka kumwita kila kisu kwamba yeye ni political prostitute.anahitaji kukimbizwa milembe maana naona ana go nuts sasa!
 
Ndio maana sitachoka kumwita kila kisu kwamba yeye ni political prostitute.anahitaji kukimbizwa milembe maana naona ana go nuts sasa!

Naamini tukiendelea kumfikiria Mtikila tunampa chati.Let him continue with his dirty politics.Tufikirie kujenga taifa.
 
Kevo nahitaji muda kutafuta tafisida,
Lakini kwa ujumla amewatukana ITV,RAIS,POLISI NA USALAMA.
Amedai kuwa polisi na usalama wameshindwa kufanya kazi yao namatokeo yake ni halimbaya ya usalama huko Tarime ndiyo maana na yeye alipigwa mawe.

Amewatukana ITV kwa madai kuwa wanatumiwa na CHADEMA.Katika hali ya kustaajabisha Mtikila amechukua sheria mkononi kwa kuwaadhibu wale anaoona wako kinyume chake.Katika mTUSI YAKE Mtikila amejifananisha na mtume ambaye yupo katikati ya kundi la simba wala watu na kuwa siasa za Tanzania zimejaa unafiki na uongo.

Kwake kitendo anachodai cha kughushiwa saini yake amekiita kuwa kimepata baraka za polisi na usalama na kuwa hata Raisi wa Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania.Amemshutumu Rais kwa maneno makali kuwa utawala wake umejaa ubabashaji wa hali ya juu na kuwa nchi ipo ipo tu.

Kwa ujumla bado inakuwa ngumu kuweka matusi hadharani hapa

Mkuu,

Sijui hayo ya ITV kutumiwa na CHADEMA maana sina uhakika lakini mengine yote mbona kasema kweli tupu? Hata mimi naona nchi ipo ipo tu na JK ni mbabaishaji.

Labda kama kuna mengine.
 
kama anaona nchi inaongozwa na wababaishaji, sasa kwa nini hakuona altrnative ni kujaribu upinzani, badala yake akashiriki kuibomoa upinzani, hata kufikia mahali pa kuwataka wanatarime waichague ccm? pili mbona analamaba michuzi kwa hao wababaishaji? huyu hana ajenda ni vema akarudi kanisani akaenda kutubu huko kabla hajawahishwa milembe
 
Hivi huyu mtikila si ameomba ccm ishinde kuliko chadema?

Mchungaji wa shetani huyu, achaneni nae
 
Hivi huyu mtikila si ameomba ccm ishinde kuliko chadema?

Mchungaji wa shetani huyu, achaneni nae

Hapa ni zaidi ya shetani. Mtikila anafanya kazi ya watu na anawatumikia watu maalumu. Sasa ndio mujue habari ya Mwanahalisi ni ya kweli unapoona Mtikila anashindwa kujizuia na kumtukana Rais Kikwete. Wanaomtuma Mtikila (Makamba, Rostam, Manji, Lowassa etc) wahawako pamoja na Kikwete hata kidogo. Inawezekana vipi Makamba amsifie, amsaidie na kumtukuza Mtikila ambaye toka siku ya mwanzo anamtukana Rais na mwenyekiti wa CCM? Hamjiulizi? Siku alipozungumzia kifo cha Wangwe pale Tarime, mtikila alisema Kikwete analinda wauaji kama alivyomlinda Marehemu Ditopile na akamtukana pia Rais. Sasa hapo bado kuna watu wanashangaa habari ya MWanahalisi!!!!
 
Nilisema kwenye ile thread ya awali kuhusu Mtikila na manane yake kuwa kuna mambo mengi yanatokea nyuma ya pazia ambayo wengi hawayafahamu. Bado yanazidi kutokea lakini ukisikiliza na kuangalia kwa makini, unaweza kuanza kuunganisha nukta na kujua kilichokuwa kimepangwa, jinsi kilivyo-backfire. Kigumu kutabiri ni nini kitatokea kwa sababy spin doctors wana zaidi ya alternative mbili katika kila mpango wao.
bado, yataokea mwngi ambayo yazidi kutoa lues ya nini kilipangwa kitokeee Tarime. Mwenye kutaka kudadisi, atabaini
 
Hapa ni zaidi ya shetani. Mtikila anafanya kazi ya watu na anawatumikia watu maalumu. Sasa ndio mujue habari ya Mwanahalisi ni ya kweli unapoona Mtikila anashindwa kujizuia na kumtukana Rais Kikwete. Wanaomtuma Mtikila (Makamba, Rostam, Manji, Lowassa etc) wahawako pamoja na Kikwete hata kidogo. Inawezekana vipi Makamba amsifie, amsaidie na kumtukuza Mtikila ambaye toka siku ya mwanzo anamtukana Rais na mwenyekiti wa CCM? Hamjiulizi? Siku alipozungumzia kifo cha Wangwe pale Tarime, mtikila alisema Kikwete analinda wauaji kama alivyomlinda Marehemu Ditopile na akamtukana pia Rais. Sasa hapo bado kuna watu wanashangaa habari ya MWanahalisi!!!!

Mkuu Halisi,

Uzuri wa Mtikila hana rafiki. Ila sasa nimegundua pia hana adui maana alienda kukopa kwa Gabachori RA.

Nimeshangaa leo umemweka Mtikila kutumiwa na Manji wakati kila siku Manji anasema Mtikila anatumiwa na Mengi. Huenda Mtikila ni kama yule Mchungaji wa Obama, inapokuja ukweli haangalia adui wala rafiki, haangalii faida wala hasara, anapigilia msumari tu.
 
Mtanzania,

Hii mtazamo wako kuhusu Mtikila ni sahihi. Jamaa rafiki yake ni pesa kama itapatikana kwa Mengi au Manji yeye poa ugomvi wao haumhusu. Hii inathibitishwa na matukio ya huko nyuma. Siku zote amekuwa anaiita CCM cha cha Majambazi leo wamekuwa allied wake wazuri. Amekuwa kila siku na malumbano na jamaa wenye asili ya kiasia kiasi cha kuwaita magabachori, wezi na majina kibao, lakini nyuma ya pazia anaenda kuvuta kwa RA, Manji etc.

Tafsiri nyepesi ya kumjua huyu jamaa ni pesa, atafanya lolote lile kukidhi haja ya tumbo lake, na katika Tanzania ya leo isiyo isha dramas Richmond, IPTL, Rada, EPA, Buzwagi, Wangwe etc he is making most of it...
 
Tunaomba basi hiyo taarifa ya Mtikila ambayo imedaiwa haiwezekani kusomwa kwenye TV, tuisome hapa. Au hata hapa haifai? Mbona tumebandikiwa mengi tu hapa? Au haipo? Aliye nayo atuwekee tafadhali, nasi tuchambue kama kilichosemwa ni matusi au tu ni mambo (ya ukweli) yasiyowapendeza baadhi ya watu.
 
mkuu, mimi naona kujadili maneno ya kichaa kama mtikila nikupoteza muda.... huyu ni kichaa..sasa kichaa akipatia kitu kimoja haimaanishi amepona na kuwa na akili timamu atabakia kuwa ni kichaa ushahidi unaonesha hivyo
 
Baada ya Mtikila kupata kichapo Tarime, mimi ni miongoni mwa waliosema huyu jamaa sio mzima.
Nitaamini 100% kwa 100% kuwa Mtikila ni kichaa per se kama itathibitika ile taarifa ya kutubu pia ni yake lakini anaikanusha.
Ila ikithibitishwa imefojiwa mimi naomba niwe wa kwanza kumpa the benefits of doubti na hili nawathibitishia there is something fissy and there is more to it kuliko hizi kelele na matusi.

Mimi nilibahatika kuisikia taarifa yake ikisomwa live ITV. Amini usiamini ingawa ilisomwa kama sehemu ya taarifa ya habari, ilisomwa yote kama ilivyo kwa zaidi ya dakika 5z1 kitu ambacho hata taarifa ya ikulu haipati bahati kama hiyo.

Kwa wanaifutatilia ITV taarifa ile ya kitubio ilipewa umuhimu kama ule wa taarifa za Mengi wakati akimshutumu Manji ama taarifa za MOAT ambazo ni huyo huyo katika kivuli chake.

Kitubio hicho kinaashiria kilipelekwa ITV na mwenye mali na kulikuwa na mkono wa mtu. Ama alikuwa na ajenda fulani ama liko jambo.
Nafuatilia ili niwape picha kamili na kutengua kitendawili cha Mtikila kichaa, amechanganyikiwa tuu au ni mwendawazimu wa kisiasa
 
Kuna jamaa hapa alimwita Rev Mtikila ni Kahaba wa siasa...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom