Mtikila: Hili bunge la katiba limejaa wahuni na washenzi sijawahi kuona toka tupate uhuru

Mtikila: Hili bunge la katiba limejaa wahuni na washenzi sijawahi kuona toka tupate uhuru

malenga wetu

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
283
Reaction score
198
Mchungaji Mtikila leo huyu jamaa amekandia bunge lote la katiba na kusema anasikitka soon atalicha bunge hilo mana limechaguliwa kihuni.Nasema hivi wambieni kabsa nimesema hili ni bunge la kihuni limechaguliwa kihuni ndio maana unakutana na mambo ya kishenzi mnayoendelea kuyaona.

Nasema tangia uhuru sijapata kuona bunge la kihuni kama hili.Sitoshangaa maamuzi ya kihuni na kishenzi kutokea siku tunaagana pale nje.Huyo ni rev. Christopher Mtikila.

Source: BBC swahili
 
Mtikila ni zaidi ya CHADEMA!

Mtanisamehe kwani kwenye posho,hakuna tofauti ya wapinzani na chama tawala!
 
Mtikira anachosema ni kweli kabisa,hivi mtu kama Lusinde,kingunge,mwigulu na Maccm yote wanaingia bunge la katiba kwa upuuzi ambao wanauonyesha bungeni bado unaweza kuona katiba yenye akili? Mtikira uko sahihi kabisa.
 
mtikila juzi wewe ulisema chadema walijilipua mara baada ya kuhongwa na hao wahuni anawao wasema ni washenzi
 
MTIKILA huwa haeleweki, pia ni mtu anae penda sana kesi. Akikoswa kesi ama ya kushitaki au kushitakiwa huwa hana raha kama mlevi kukosa pombe. Kwa hili amekosea, unaposema wajumbe wa baraza la katiba ni wahuni na washenzi, unakuwa umemtukana pia rais alie wateua hawa watu.
 
Kama unamkubali Mtikila mwenye chama chenye usajili wa kudumu ingawa wanachama wote alionao hawafiki 150, basi unamatatizo makubwa.

Kama kawaida yenu vijana wa ccm kwa kurupuka bila hata kutumia akili, yeye kasema anamkubali mtikila na sio chama,, shiiit mbona mnakuwa na vichwa nazi jamani???. Hata kama ni wazito kuelewa ila sasa mnavuka mipaka ya wazito kuelewa..
 
Bunge la kutaka tu potsho kubwa badala ya kuangalia kilichowapeleka kujadili. Huyo mbunge aliyetoa hoja hafai kabisa kuwa mbunge wa nchi hii. Nasema kwa sababu yeye anataka kubomoa badala ya kujenga.Hizo 300000 kwa siku kwa mda wa siku 30 ni millionaire 18,000,000. Hii ni sawa na mshahara wa mtu wa sh.300,000 kwa mwezi kwa mda wa miaka 5. KAMA MSHAHARA WA MTU MMOJA KWA MIAKA MITANO ANAPEWA MBUNGE POSHO KWA MIEZI MIWILI TU AMBAYO NI MILIONI 90 KWA MWEZI HALAFU BADO ANALALAMIKA KUWA NI KIDOGO. JE, HUYU NI WA KUJENGA AMA KUBOMOA? HAFAI KUWA MBUNGE KABISA.
 
Namkumbuka huyu REV. MTIKILA katika miaka ya tisini alikuwa anadai KATIBA na TANGANYIKA irudishwe, watu wengi walidhania ni chizi kutokana na lugha yake. Leo yale mawazo yake ndiyo yanapiganiwa na wengi. Huyu jamaa huwa ni MTAIFA sana, ila bahati mbaya watu wengi hawamuelewi. nakumbuka alishaipeleka serikali mahakamani akidai mgombea binafsi, alivyoshinda ile kesi PINDA akampotezea. Leo hii tunapigania mgombea BINAFSI.
 
Kama wabunge wote wa bunge la katiba ni wahuni basi hata yeye ni mhuni na ndio maana amechaguliwa kujiunga na machizi wenzake
 
Kikwete ana kazi kweli kweli,ila mtikila anachosema kina ukweli ndan yake
 
Back
Top Bottom