Mtikisiko: Mauzo soko la hisa Dar yaporomoka tena

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,950
Mauzo soko la hisa Dar yaporomoka tena

Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ( DSE) yameendelea kushuka kwa wiki ya tatu mfululizo baada ya wiki iliyopita kuporomoka kwa asilimia 87.

dse+mauzo_1.jpg

Katika wiki hiyo iliyoishia Novemba 25, DSE imeeleza kuwa mauzo hayo yalishuka kutoka Sh4 bilioni hadi kufikia Sh500 milioni.

Kushuka huko kwa mauzo kulitokana na kuyumba kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa sokoni hapo kwa asilimia 85 kutoka hisa 671, 618 hadi 101, 809 wiki iliyopita.

Ripoti ya wiki ya mwenendo wa soko hilo iliyotolewa leo Jumatatu (Novemba 28, 2016) inaeleza kuwa kushuka huko kwa mauzo kunaweza kuhusianishwa na ongezeko la mauzo ya hati fungani zilizouzwa sokoni hapo wiki hiyo.
 
Hapo ata sielewagi chochote mwenye ujuzi wa mambo ya hisa anieleweshe
 
Watu walioweka hisa katika makampuni mbalimbali wanajitoa hivyo ununuzi wa hisa unapungua katika hilo soko la hisa
 
Kupanda na kushuka mauzo kwenye soko la hisa ni kitu cha kawaida kabisa hasa ikiwa makampuni yaliyopo kwenye hiyo Exchange yapo machache kama ilivyo kwa DSE.
 
Acha ujinga wewe. Kama huelewi mambo ya uchumi kaa kimya.
 
Kupanda na kushuka kwa mauzo kunamaanisha kiwango cha biashara sokoni kimeshuka na hivyo kuathiri upatikanaji wa mitaji kwa makampuni yaliyojiorodhesha na pia inawaathiri wamiliki wa hisa wanaouza hisa zao ili wapate pesa za kufanyia mambo mengine.

Kwa nchi zilizoendelea kushuka kwa kiwango kikubwa kama hiki ni kiashiria cha kuanguka kwa uchumi. Kwetu bado DSE sio kipimo sana kwa sababu makampuni yaliyopo sokoni ni machache lakini ukitazama kisekta hili linaweza kuwa pigo jingine kwa sekta ya fedha kwa kuwa kila Bank nchini ipo DSE.
 
Sarakasi ziliendelea tulikodoleana macho na kupewa moyo tafiti za ndani na za kimataifa zinaonesha hali kijiwen ni shwari 🙄
 
Acha ujinga wewe. Kama huelewi mambo ya uchumi kaa kimya.[/QUOTE

You need to learn to use the power of your arguments rather than attaching the person in order to drive your point home.

If you think I am stupid then tell me what you know about stock markets.
 
Kupanda na kushuka kwa mauzo kunamaanisha kiwango cha biashara sokoni kimeshuka na hivyo kuathiri upatikanaji wa mitaji kwa makampuni yaliyojiorodhesha na pia inawaathiri wamiliki wa hisa wanaouza hisa zao ili wapate pesa za kufanyia mambo mengine.

Kwa nchi zilizoendelea kushuka kwa kiwango kikubwa kama hiki ni kiashiria cha kuanguka kwa uchumi. Kwetu bado DSE sio kipimo sana kwa sababu makampuni yaliyopo sokoni ni machache lakini ukitazama kisekta hili linaweza kuwa pigo jingine kwa sekta ya fedha kwa kuwa kila Bank nchini ipo DSE.

Tatizo la wachangiaji na waanzishaji mijadala ni ufahamu mdogo wa masuala yanayojadiliwa. Katika suala hili kwa mfano, kushuka au kupanda kwa hisa zilizouzwa pale DSE hakuwezi kuwa kigezo cha kupima kupanda au kuporomoka kwa uchumi wa Tanzania.

Chukua kwa mfano mauzo yanafikia milioni 500. Hizo si chenji tu kwa mfanyabiashara mmoja? Ndiyo kiwe kipimo cha uchumi wa TZ? Ikiwa Johannesburg Stock Exchange imeshuka kwa hiyo asilimia 10 tu watu wanatetemeka kwani volume yao kwa siku ni kama Rand Billioni 14. Siyo Shillingi 500 million!

Mabenki mengi ya Tanzania hayapo DSE.KCB have cross-listed,NMB recently sold some bonds and although CRDB has sold some shares I don't think you can buy or sell those shares at DSE. All other banks, and they are many in Tz are private. I stand to be corrected.
 
ma Dr wetu wakiongozwa na Mpango wansema uchumi wetu unakua sijui ni vigezo gani vinatumika
 
Tatizo la wachangiaji na waanzishaji mijadala ni ufahamu mdogo wa masuala yanayojadiliwa. Katika suala hili kwa mfano, kushuka au kupanda kwa hisa zilizouzwa pale DSE hakuwezi kuwa kigezo cha kupima kupanda au kuporomoka kwa uchumi wa Tanzania.

Chukua kwa mfano mauzo yanafikia milioni 500. Hizo si chenji tu kwa mfanyabiashara mmoja? Ndiyo kiwe kipimo cha uchumi wa TZ? Ikiwa Johannesburg Stock Exchange imeshuka kwa hiyo asilimia 10 tu watu wanatetemeka kwani volume yao kwa siku ni kama Rand Billioni 14. Siyo Shillingi 500 million!

Mabenki mengi ya Tanzania hayapo DSE.KCB have cross-listed,NMB recently sold some bonds and although CRDB has sold some shares I don't think you can buy or sell those shares at DSE. All other banks, and they are many in Tz are private. I stand to be corrected.

Ni kweli kunaweza general indicator ila niliposema kwa financial sector ni signal mbaya I meant it, all big banks nchi hii ziko registered DSE na ndipo mitaji yao inapotoka. DSE imelist Tanzanian banks nane hii sio jambo dogo. Kwa maana nyingine hizo financial institutions nyingine ambazo hazipo mitaji yake inatokea nje kitu ambacho ni hatari kuliko watu tunavyochukulia.

Hoja kuhusu CRDB na NMB hawa hisa zao zinauzwa. Unaona hakuna effect kwao ila kuna effects kubwa kwa wawekezaji wa hisa katika makampuni hayo kwani iwapo wanataka kuuza hisa zao hakuna wa kununua.

Swala la milioni 500 ambalo unaliita la kawaida ni vema ungepitia records za nyuma za DSE kuhusu mauzo. Sijaangalia vema lakini katika kipindi kirefu probably toka 2010 hii inaweza kuwa the lowest sales volume.

Ukianalyse mambo hali ya soko sio ya kawaida ni mbaya sana.
 
Mauzo soko la hisa Dar yaporomoka tena

Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ( DSE) yameendelea kushuka kwa wiki ya tatu mfululizo baada ya wiki iliyopita kuporomoka kwa asilimia 87.

dse+mauzo_1.jpg

Katika wiki hiyo iliyoishia Novemba 25, DSE imeeleza kuwa mauzo hayo yalishuka kutoka Sh4 bilioni hadi kufikia Sh500 milioni.

Kushuka huko kwa mauzo kulitokana na kuyumba kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa sokoni hapo kwa asilimia 85 kutoka hisa 671, 618 hadi 101, 809 wiki iliyopita.

Ripoti ya wiki ya mwenendo wa soko hilo iliyotolewa leo Jumatatu (Novemba 28, 2016) inaeleza kuwa kushuka huko kwa mauzo kunaweza kuhusianishwa na ongezeko la mauzo ya hati fungani zilizouzwa sokoni hapo wiki hiyo.
Halafu tunaambiwa uchumi unakua. Okaaaay ngoja tuangalie uchumi unakua
 
Back
Top Bottom