Mtindo wa maisha, na makosa madogo madogo tunayofanya

Mtindo wa maisha, na makosa madogo madogo tunayofanya

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,951
Reaction score
19,766
Habari jamiiforum.

Hii ni Kwa watu wazima 40+

Mambo meengi tunafanya ila kuna makosa yanajitokeza bila kujua,tunajiaibisha bila kujua.
Mbaya zaidi tunaona ni kawaida.

Na ni ngumu mtu kukwambia ukweli

1.Vitu tunavyopost kwenye social network.

Kuna watu wanaweka status huko WhatsApp unashindwa kuelewa huyu anawaza nini kupost huku kitu

2.Kuvaa Earphones.

Yaani upo barabarani umevaa vitu masikioni eti unasikiliza muziki,
Yaani uhatarishe maisha yako Kwa jambo la kijinga.

3.Kutema mate ovyo.

Kuna mtu hata hawazi wenzie wanajisikiaje yeye ni kutema mate,mara ajichokonoe puani,halafu ni mtu mzima,inatia kinyaa sana

4.kuzungumzia vitu vichafu ikiwa wenzio wanakula.

Yaani mtu anazungumzia stori za kupasuka Kwa bomba la ma*I au kinyesi n.k huku mnakula . binafsi huwa siwezi kuendelea Kula.mbaya zaidi.unakuta unamuheshimu , kumwambia ni mtihani.

5.Mazoea mabaya na kuchukuliana poa.

Mfano umeagiza Nyamachoma mahali mara jamaa yako huyo from no where kachukua kipande ,bila kunawa ,akijiamini ni msafi.
Au unapaki usafiri mara kakupora funguo huyooo anaenda misele,no kuomba ni Kwamba anakumudu.

6.Kuazima simu labda upige lakini ukaanza kuscroll simu hiyo.

Mara uigeuze mara utake kujua ina uwezo upi,bro hizi pigo za watoto wadogo simu ni faragha ya mtu.

7.Kuvaa cheni na pete nyingi vidoleni.

At least hiyo cheni na hizo ring ziwe expensive na value ya juu kinyume na hapo, unazingua.rasta, tattoos na mitindo mingi imenipita kushoto sana

8.Kuvaa nguo fulani za vijana.

Nguo yenye maandishi,suruali iliyochanika chanika,zina umri wake ,jitafakari

9.Kutembea na redio barabarani.

Kuna radio ndogo zenye sauti kubwa Sana na makelele,ajabu kuna watu wazima anatembea nayo mtaani,na anaweza fika kijiweni asiizime,kiasi cha kuharibu mazungumzo ya watu wengine.

10.Ishi maisha unayopenda ikiwa tu huvunji Sheria za nchi.
 
Mtinndo wa maisha ya mtu hau-detremine umri mkuu ! Kuna kijana wa 25+ havai jeans , alafu kuna mtu wa 45+ anagonga cheni, sun glasses na jeans yake swaafi !

Ni namna unavyojiweka/jizoesha na jamii inayokuzunguka kwa ujumla !

Sijafikia huo umri uliotaja hapo, wala sijaukaribia lakini kuna vitu umetaja hapo sivitumii kabisa
 
Mtinndo wa maisha ya mtu hau-detremine umri mkuu ! Kuna kijana wa 25+ havai jeans , alafu kuna mtu wa 45+ anagonga cheni, sun glasses na jeans yake swaafi !

Ni namna unavyojiweka/jizoesha na jamii inayokuzunguka kwa ujumla !

Sijafikia huo umri uliotaja hapo, wala sijaukaribia lakini kuna vitu umetaja hapo sivitumii kabisa
Kwanza nikupongeze wewe ni mfano wa kuigwa ,nimetoa mfano hapo juu haswa Kwa watu wazima wanaobehave kama watoto
 
hiyo no 3 naifanyaga mara moja tu ile nikiwa nafanya usafi wa kinywa,, huku kwingine nishashindwa na huwa sipendi kuona mtu anatema tema huwa wananiudhi kweli
 
Back
Top Bottom