Jenifa Fidelis
New Member
- Jul 18, 2021
- 1
- 1
Nini maana ya tatizo la nguvu za kiume?
Hili ni tatizo linalohusisha hali tofauti kwa wanaume ambalo linaweza kuathiri njia ya mkojo na uzazi kwa mwanaume.
- wanaume wengi wamekuwa wakipata hofu na aibu kwa sababu tatizo hili linahusisha sehemu za siri.
Je ni Nini chanzo cha tatizo la kutosimamisha uume?(erectile dysfunction)
- hili ni tatizo ambalo mwanaume anakosa nguvu za kiume na uume kushindwa kusimama kwa ajili ya tendo la ndoa
Ni kwa namna gani mtindo wa maisha unasababisha tatizo la nguvu za kiuume?
-Tatizo la nguvu za kiume ni tatizo linalosababishwa na saikolojia na tatizo la mfumo wa mwili
- ili uume uweze kusimama ubongo unahitaji kutuma taarifa kwenye uume ili kuruhusu damu kujaa ambayo ndo husababisha uume kusimama. Zifuatazo ni sababu za kisaikolojia zinazopelekea tatizo,
1. Mawazo na hofu, mfano matatizo/ugomvi kwenye mahusiano, matatizo ya kifamilia n.k. Hupelekea ubongo kushindwa kupeleka taarifa kwenye uume
2. Uchovu
3. Kutojiamini kuhusu maumbile yako
Mwanaume anapokuwa na wasiwasi kuhusu uume wake na uwezo wa kumrithisha mwenzi wake hupelekea ofu kwenye ubongo unaosababisha uume kutosimama
4. Sonona(depression)
Hupelekea mfumo wa homoni za mwili kubadilika ambayo huweza kusababisha uume kutosimama au kukosa hamu ya tendo la ndoa
5. Unywaji wa pombe na matumiz ya dawa za kulevya, huathiri njia za fahamu ambapo hupelekea kuchoka na kuleta ugumu kwenye kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa.
6. Kutokulala. Mwili unahitaji kupumzika na akili pia, kutokulala hupelekea homoni(cortisol) kuwa juu ambayo pia hupunguza hamu ya tendo la ndoa na uume kusimama.
7. Kutokuwa na uaminifu kwenye mahusiano
Zifuatazo pia ni sababu za kimwili zinazopelekea tatizo
1. Unene
2. Shinikizo la damu
3. Matatizo ya moyo
4. Kuwa na mafuta mengi
5. Kupungua kwa homoni zinazohusika na mfumo wa uzazi kwa mwanaume
6. Kansa ya tezi dume/tezi dume kuwa kubwa
Je, wajua kuwa matatizo mengi ya kimwili yanayosababisha matatizo ya nguvu za kiuume yamekuwa yakisababishwa na MTINDO WA MAISHA?
Mfano:
1. Ulaji usiofaa, mfano:
-kula chakula kuzidi mahitaji ya mwili hivyo kunenepa
2. Kutofanya mazoezi
Kutokana na mtindo wa ulaji wa maisha ya sasa mazoezi ni muhimu kwa mwili mana hupunguza magonjwa yasiyoambukizwa ambayo pia kusababisha matatizo ya nguvu za kiuume mfano, kisukari, shinikizo la damu
- kufanya mazoezi hupunguza uzito uliozidi kupita kiasi.
Je, wajua tatizo la nguvu za kiuume linazuilika kwa kubadili mtindo wa maisha?
1. kuwa makini na mtindo wako wa ulaji kama kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi na sukari nyingi ambavyo hupelekea mishipa ya damu kuziba na kupelekea matatizo ya moyo na kisukari ambayo hupelekea matatizo ya nguvu za kiuume
2. Kuzuia kuwa na kuwa na uzito uliopitiliza
3. Kupunguza unywaji wa pombe sana
4. Mazoezi kila mara
5. Epuka matumizi ya dawa kiholela bila maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya.
JIPENDE LINDA AFYA YAKO, WEWE NI TAIFA LA KESHO.

- kula vyakula vya sukari, mafuta na chumvi zaidi ya mwili unavyohitaji
- kutokula mbogamboga na matunda
- kula nafaka zilizokobolewa

Upvote
1