Mtitu: Sababu ya kuamua kuzambaza filamu zangu mwenyewe badala ya kuuza Steps Entertainment

William Mtitu

Member
Joined
Nov 12, 2011
Posts
31
Reaction score
16
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiulizwa sababu ya kuamua kusambaza filamu zangu mwenyewe badala ya kuzipeleka kwa wasambazaji ambao nilikuwa nikifanya nao kazi kwa muda mrefu, yaani kampuni ya Steps Entertainment.

Najua maswali yamekuwa mengi kwa kuwa kuna watayarishaji wengi wa filamu nchini wanaohangaika usiku na mchana ili kupata mkataba wa kufanya kazi chini ya kampuni hiyo kwa kuwa Steps Entertainment ndiyo kampuni ya usambazaji inayolipa vizuri zaidi kuliko makampuni mengine yote kwa sasa.

Leo nimeamua nifunguke rasmi…

Kwanza nikiri kuwa maneno ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mhesimiwa Dr. Jakaya Kikwete aliyotamka siku aliyoiita Ikulu kamati ya mazishi ya marehemu Steven Kanumba ndiyo yamekuwa yakinisukuma sana hadi kufikia uamuzi huu mzito.

Kati ya waliounda kamati hiyo iliyoitwa Ikulu, mimi nilikuwa katibu, Mwenyekiti alikuwa Gabriel Mtitu au maarufu kama Mtitu Game, pia kulikuwa na wajumbe wengine kama Ruge Mutahaba, Asha Baraka, Jacob Steven ‘JB’ na Mzee Chilo. Baada ya kuongea mengi kuhusiana na msiba wa Kanumba na mazishi yake, mheshimiwa rais aliuliza ‘Hivi marehemu Kanumba kaacha filamu ngapi?”

Kwa aibu tulimjibu mheshimiwa rais kuwa marehemu Kanumba hajaacha hata filamu moja, zote ni za msambazaji wake na hata mbili ambazo zilikuwa hazijatoka yaani ‘Ndoa yangu’ na ‘Love & Power’ tayari zilikuwa ni za msambazaji kutokana na aina ya mkataba tunayoingia na msambazaji.

Mheshimiwa Rais alisikitika sana, akatuambia kuwa yeye hawezi kutumia nguvu kutukataza kuuza mali zetu lakini angependa kuona kuwa tunamiliki wenyewe filamu zetu na tutakapoona tumekwama tumwambie. Aliongeza kuwa kuuza haki zetu ni kama kuuza utu wetu. Maneno ya mheshimiwa Rais yalinichoma sana.

Mimi ni msanii wa kwanza kufanya kazi na kampuni hiyo kama mtayarishaji wa filamu na filamu yao ya kwanza kuisambaza ilikuwa ni ‘Jeraha la Ndoa’ ambayo niliitengeneza mimi. Na kwa kuthibitisha hilo, mwaka huu kampuni hiyo ya Steps ilitoa tuzo ya heshima kwa kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd kwa ajili hiyo.

Nasikitika kukiri kuwa filamu zote ambazo nilizitengeneza kisha zikasambazwa na kampuni ya Steps, siyo zangu tena. Kampuni hiyo imekuwa ikinunua haki zote za filamu wanazopelekewa kwa ajili ya kuzisambaza kwa hiyo baada tu ya kusaini mkataba wao unakuwa huwezi kufaidika tena na chochote kutokana na mauzo au faida nyingine zinazotokana na filamu yako.

Kwa aina ya mikataba ambayo wasanii na watayarishaji tunaingia na kampuni ya Steps Entertainment, sisi tumekuwa ni wasimamizi tu wafilamu za zao, yaani ni kama manyapara kwenye mashamba ya mkonge wakati kwa ukoloni. Ni waajiriwa tusio na mafao ya uzeeni.

Kwa taarifa tu ni kwamba filamu zote mnazoziona mitaani zikisambazwa na kampuni siyo za hayo makampuni yanayotajwa kutengeneza filamu hizo bali ni filamu za Steps Entertainment. Ndiyo maana hata ukienda kwenye Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) utakuta wasanii wakubwa hawamiliki kabisa filamu lakini kampuni ya Steps inamiliki filamu zaidi ya 400.

Kifupi ni kuwa hadithi ni zetu, sehemu za kuigizia ni zetu, tunaigiza sisi, tunarekodi na kuhariri sisi lakini filamu ni za Steps Entertainment na ndiyo maana hata kampuni ya marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba the Great’ imesambaratika baada ya kifo chake na mama yake akikabiliana na ugumu wa maisha lakini filamu za Kanumba bado zinatesa kwenye soko la filamu ndani na nje ya nchi.

Nawashangaa watu wanaomshutumu mama mzazi wa Kanumba kuwa amemaliza mali za mwanae na sasa anaishi kwa kufadhiliwa na Lulu, wangejua kilicho nyuma ya pazia wangemuonea huruma badala ya kumshutumu. Wakati Steps wanakiri kuwa filamu iliyowahi kuuza sana katika historia ya kampuni yao ni ‘Ndoa yangu’ ya Kanumba, hawasemi kuwa familia yake imenufaika vipi zaidi ya kupewa tuzo.

Pamoja na kununua haki zote za filamu, kampuni ya Steps hawatoi malipo ya filamu wanazozinunua kwa muda muafaka hivyo kutufanya tuendelee kuwa mafukara siku hadi siku. Hii ni sababu ya pili ya mimi kujitoa Steps, sitaki familia yangu ije kudhalilika baada ya kifo changu.

Fikiria unapeleka filamu yako Steps, mnaingia mkataba wa kuuziana, lakini hawakulipi mpaka wakati watakapoamua kuiingiza sokoni hivyo hata wakikaa mwaka bila kuiingiza utakaa mwaka mzima unasuburi pesa. Hivi kweli mwaka huo utakuwa unakula nini kama umeamua kuifanya sanaa kuwa kazi yako?

Cha kuchekesha hata wanapoamua kuiingiza sokoni hawakulipi mpaka baada ya wiki mbili au tatu baada ya filamu yako kuwa imeingia sokoni, utasema hapo wamekulipa au umejilipa mwenyewe baada ya kuwa imenunuliwa?

Mfano mwingine hai ni wa marehemu Said Juma Kilowoko (Sajuki) ambaye ni miongoni mwa wasanii maarufu na watayarishaji wa filamu. Marehemu Sajuki alilazimika kuzunguka na wasanii wenziye mikoani akiwa anamuwa taabani ili tu aweze kupata fedha za matibabu jambo ambalo naamini lilimzidishia matatizo ya kiafya.

Na kutokana na kuuza haki zetu zote ilibidi mkewe Sajuki, Wastara atengeneze ‘Mr & Mrs Sajuki’ ili aweze kupata fedha za kujikimu na kurekebisha mambo mbalimbali yaliyovurugika wakati akimuuguza mumewe. Kama tungekuwa hatulazimiki kuuza haki zetu zote, familia hiyo ingeweza japo kupeleka filamu zake kwenye vituo vya runinga barani Afrika ambako ni chanzo kingine cha mapato kwa msanii.

Baada ya kutafakari kwa kina niliamua kulipia leseni ya usambazaji wa filamu kupitia kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd ili niwe nasambaza filamu zangu nikitegemewa kupata sapoti kubwa kutoka kwa wasanii wenzangu hasa mastaa wakubwa lakini imekuwa kinyume chake. Kwa sasa naonekana adui mbele ya wenzangu.

Kupitia kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd, niliingiza sokoni filamu ya ‘Omega the Confusion’, na ndani ya masaa matano ya kwanza nilifanikiwa kurudisha gharama zangu zote na kupata faida kidogo. Toka hapo hadi sasa inaendelea kukimbia sokoni hivyo natengeneza faida tu na bado filamu ni yangu, naweza kuifanyia chochote kama kuipeleka kwenye runinga za kimataifa n.k

Nimalizie kwa kuweka wazi kuwa sina ugomvi wowote na kampuni ya Steps, mmiliki wake wala mtumishi yeyote wa kampuni hiyo. Pia sina chuki na yeyote kati ya wanaoendelea kufanya kazi chini ya kampuni hiyo. Kikubwa ni kuwa haya ni maisha na kila mmoja ana mtazamo wake katika kuyakabili na kujiletea mafanikio.
 
unyonyaji kila sehemu. ndio ubepari huo
ata serikali inanyonya raia wake ata kwenye line ya simu.
 
Kichwa cha habari na maudhui havijaendana, labda kwenye kichwa cha habari ungewataja steps kwani wanaonekana ndio habari yenyewe
 
Yani Shaaban bin Robert akifufuka leo atalia sana.

Katika kazi yake moja alikuwa analalamika sana (kwa stadi za staha zake) kuhusu watunzi kukosa haki zao, na jinsi alivyodhulumiwa. Akirudi leo atakuta mpira uko pale pale alipopaacha zaidi ya miaka hamsini iliyopita!
 
Mungu akupiganie uendele kusimama imara kama mnara
 
HIVI HIZI NAKALA NI ZA DVD sio?
au bado wanatoa mikanda ya vhs???
 
Mkuu ungebadilisha heading........Kha.......

Mbona part ya mma Kanumba ni ndogo sana
 
Kweli wajinga Ndio waliwao ....! kumbe Ndio maana...
 
Alikuwa wapi siku zote? all the best for him.
 
Kumbe,mbona wasanii wa kike wanafuja pesa au za ngada nn? mjomba wee komaa na kampun waache wazubae
 
Ni jambo jema na la maana kaza mwendo utafika kaka
 
vijana wa kibongo km tunmerogwa tumekuwa dhaifu sana hta kwny masuala yanayohusu haki zetu na hta anapotokea mtu kututetea tunaanza kumuona adui .....rejea inshu ya sugu na vinegar walikuwa wanawapigania wasanii wapate haki zao lkn cha ajabu wasanii hao hao ndyo walikuwa wakiwaponda wakina sugu huku wakimtetea ruge huku moyon wakijua kabsa madhambi anayowafanyia sasa ukija kwny hii inshu ya bongo movie ndyo utachoka kabsa kwa akil ya kawaida ungefikiria wasanii wote wangekuwa nyuma yha mtitu kumpa support kinyume chake wanatumiwa na mhindi kumhujum mtitu .......jb. ray ,cloud na wengineo achen kuridhika na vitu vidogo kuna uzee kumbuken angalien maisha anayoishi mzee small sa iv akil mtie kichwan:disapointed::disapointed::disapointed::disapointed:
 
Hóngera umepata shamba utalima utavuna utapalilia wajukuu watalikuta huo ndio mpango kwa wenye mawazo yaliyofunguka
 
yaani huyu Mtitu wa Game, Mungu ambariki, amwongezee baba wa watu sio siri,ana roho Mbaya na wala umkatai yeyote atakaye kutana nae,ana moyo wa upendo na huruma daima, MUNGU AMBARIKI NA AMTIE NGUVU DAIMA AENDELEE NA UPENDO NA KUJALI WASANII SIKU ZOTE. Mimi nnakumbuka alivyomtunza na kumuudumia ndugu yetu rafiki yetu mpendwa KIBABU.

Hatuna cha kukulipa Mr. Game ni Mungu tu aonae sirini ndie atakae kupa yale unayostaili. Mungu tu akupe moyo na akuongezee upendo wa kujali na kuwasaidia wasanii.

Marehemu Kanumba kama sio wewe, ni kweli asingesikika popote pale,
 
haya ya maajabu makubwa. msanii anatakiwa kufaidika na kila nakala ya kazi yake. ni makosa makubwa kuuza jumla hakimiliki ya kazi yako. nakutakia mafanikio Ndugu Mtitu endelea kuonesha njia!
 
kuna mtu anaitwa MR TURNER hapo Marekani,miaka ya 50,60,70,80na 90 wakati akifanya kama anavyofanya STEP leo walikuwa wanamcheka!leo hii ana movies zaidi ya laki moja na akuna yeyote yule anabishana nae DSTV wanaonyesha TUNNER CLASIC MOVIE na kebo TV nyingine duniani zaidi ya 100,awauziii ana wapa haki ya mwaka mmoja then wanarudi mezani anawapa bei wanasaini tena mwaka mwingine.......jama ni billionea na ata wajukuu wa wajuuu wa wajukuuu wake watakuwa billioneas....hivi ndivyo Step atakavyokuwa kama mimi na wawe atutoamka na kwasaidia hawa bandugu wa bongo movies.

the same na Bongo fleva kama awatoungana na kuanzisha kitu kama www.motown.com wataishia kuwa mateja kama banza stone pale sinza baar siitaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…