Mto Kongo na Maajabu yake

Mto Kongo na Maajabu yake

kutofautisha kuna Congo Kinshasa raisi ni Etiene Tshekedi na Congo Brazzaville raisi ni Denis Sasou Ngueso.
Infact waligawanywa tu na wakoloni shauri ya ukubwa ila hawa ni ndugu
Tukutupe Congo ipi mkuu?
 
Unakataa nini sasa? Na wewe umesoma jalalani nini? Mwandishi anakwambia alikuwa ni Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kuweza kufika mto Kongo! Usiwe limazwazwa mkuu!
Hapo No 6 ndio pekee nakataa mana huyo Mzungu alikuta watu hapo wakiishi ...Tofauti tu hawakuwa Wazungu
 
Congo Kinsasha kwenye utajiri
Haugopi Ebola Mzee Meko kwa maana inakadiriwa watu karibia 1000 tayari wameshakufa kwa sababu ya ugonjwa huo. Hali ni mbaya sana mkuu huko Congo kwa baadhi ya majimbo.
 
Unakataa nini sasa? Na wewe umesoma jalalani nini? Mwandishi anakwambia alikuwa ni Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kuweza kufika mto Kongo! Usiwe limazwazwa mkuu!
Msamehe mkuu, I hope kajifunza kitu next time atasoma between the lines.
 
Natural Wonders of the World
Forgotten Failures of African Exploration.jpg
 
Bandiko zuri mkuu, kwa kukazia tu uchumi wa Kongo zote mbili (Kinshasa) na (Brazzaville) unategemea sana uwepo wa mto Kongo. Wataaalamu wa mambo wanasema kwamba "River Congo is the only true highway in Congo ". Miundombinu ya barabara na reli ipo chini sana Congo, hivyo basi madini ya shaba na vito pamoja na mazao kama kahawa na sukari husafirishwa pitia mto Kongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
hivi nauliza mto Congo ni navigable?
 
ADUI mkubwa wa Afrika ni sisi Wafrika mkuu. Mabeberu huwa wanatafuta Vibaraka na kupenyeza rupia. Wabeligiji na Wafaransa wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuivuriga Congo. Achilia mbali Wizi mkubwa wa kutisha walioufanya huko.
Ukisoma Historia utaona ni jinsi gani Belgium na France zilivyokuwa zaidi ya Maharamia katika baadhi ya Nchi za Afrika.
Mkuu mkiweka kiongozi mzalendo wanamuua mabeberu kwa njia yeyote.
 
MTO KONGO
Afrika ni moja kati ya mabara ambalo limebarikiwa sana kuwa na vivutio vya aina mbalimbali. Moja kati ya vivutio hivyo ni Mto Kongo. Mto Kongo ni mto wa pili kwa urefu barani Afrika baada ya Mto Nile, lakini pia ni mto wa tisa kwa urefu duniani. Vyanzo vikuu vya Mto Kongo ni Milima na Nyanda za Juu za Bonde la Ufa la Afrika Mashariki (East Africa Rift Valley), Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) na Ziwa Mweru (ndio chanzo cha mto Lualaba).



MAAJABU YA MTO KONGO

  1. Mto wa pili kwa urefu barani Afrika baada ya Mto Nile.
  2. Mto wa pili duniani kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini baada ya Mto Amazon wa Amerika ya Kusini (South America).
  3. Mto Kongo ndio mto wenye kina kirefu zaidi duniani, unakadiriwa kuwa na kina zaidi ya 230 mita.
  4. Jina la Mto limetokana na ufalme wa Kongo (Ancient Congo Kingdom) wa hapo zamani, ufalme huo ulikuwepo maeneo ya karibu kuzunguka mdomo wa mto Kongo.
  5. Mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme (Hydroelectric plants) inakidiriwa siyo chini ya 40 ndani Mto Kongo ni mto ambao maji yake yananguvu sana kiasi kwamba unauwezo wa kutoa na kukidhi mahitaji ya umeme katika nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa).
  6. Katika mwaka 1482 Diego Cao ndio alikuwa Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kufika na kujionea Mto Kongo.
  7. Mto Kongo unakatisha katika mstari wa Ikweta (Equator) mara mbili.
  8. Nchi mbili za Afrika majina yake yametokana na uwepo wa Mto Kongo, ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo) na Jamhuri ya Kongo (The Republic of the Congo).
  9. Jina la Mto lilibadilishwa kutoka Mto Zaire na kuitwa Mto Kongo mwaka 1997 baada ya Nchi ya Zaire kubadilisha jina lake na kujiita Jamhuru ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo). The State of Zaire (1971-1997) ilipewa jina kutokana na Mto Zaire ambao hivi sasa unaitwa Mto Kongo baada ya kubadilishwa jina mwaka 1997.
  10. Unakadiriwa kuwa na visiwa vidogo vidogo zaida ya 4000 huku 50 kati ya hivyo vinakidiriwa kuwa na ukubwa zaidi ya (miles) 10 urefu.


  • Vyanzo (Sources) 👉 Lake Tanganyika, Lake Mweru and Highlands and Mountains of East African Rift Valley.
  • Urefu (Length) 👉 4700 km
  • Bonde (Basin Cover) 👉 4,014,500 km square.
  • Mdomo wa Mto (River Mouth) 👉 Atlantic Ocean
View attachment 1015993



Sasa maajabu yako wapi hapo wastage
 
Kama ni mto wa pili kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini duniani na mto wa tisa kwa ukubwa duniani iweje Nile iwe kubwa kuliko mto Kongo, je huo ukubwa unatazamwa katika sura ya upana au pamoja na kina chake?
Nile ni ndefu lakini nyembamba. Congo ni mto mpana na wenye kina kirefu zaidi
 
Kama ni mto wa pili kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini duniani na mto wa tisa kwa ukubwa duniani iweje Nile iwe kubwa kuliko mto Kongo, je huo ukubwa unatazamwa katika sura ya upana au pamoja na kina chake?
Nile ni mto mrefu zaidi duniani na siyo mto mkubwa zaidi duniani. Ukubwa wa mto unapimwa kwa discharge power ya maji yanayomwagwa baharini, kina na upana.
 
Back
Top Bottom