NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
kutofautisha kuna Congo Kinshasa raisi ni Etiene Tshekedi na Congo Brazzaville raisi ni Denis Sasou Ngueso.Hebu nisaidieni swali hili jamani Congo DRC ni tofauti na Congo Brazzaville??? Na maraisi wao ni tofauti??
Sent using Jamii Forums mobile app
upo sahihi kabisa, lazima tuijue Afrika yetu.Nile ni urefu, ila kwa upana hauwez fikia mto kongo
Tukutupe Congo ipi mkuu?kutofautisha kuna Congo Kinshasa raisi ni Etiene Tshekedi na Congo Brazzaville raisi ni Denis Sasou Ngueso.
Infact waligawanywa tu na wakoloni shauri ya ukubwa ila hawa ni ndugu
Congo Kinsasha kwenye utajiriTukutupe Congo ipi mkuu?
Hapo No 6 ndio pekee nakataa mana huyo Mzungu alikuta watu hapo wakiishi ...Tofauti tu hawakuwa Wazungu
Haugopi Ebola Mzee Meko kwa maana inakadiriwa watu karibia 1000 tayari wameshakufa kwa sababu ya ugonjwa huo. Hali ni mbaya sana mkuu huko Congo kwa baadhi ya majimbo.Congo Kinsasha kwenye utajiri
Msamehe mkuu, I hope kajifunza kitu next time atasoma between the lines.Unakataa nini sasa? Na wewe umesoma jalalani nini? Mwandishi anakwambia alikuwa ni Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kuweza kufika mto Kongo! Usiwe limazwazwa mkuu!
Ahsante sana Smart9111, karibu tena mkuu.
hivi nauliza mto Congo ni navigable?Bandiko zuri mkuu, kwa kukazia tu uchumi wa Kongo zote mbili (Kinshasa) na (Brazzaville) unategemea sana uwepo wa mto Kongo. Wataaalamu wa mambo wanasema kwamba "River Congo is the only true highway in Congo ". Miundombinu ya barabara na reli ipo chini sana Congo, hivyo basi madini ya shaba na vito pamoja na mazao kama kahawa na sukari husafirishwa pitia mto Kongo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mkiweka kiongozi mzalendo wanamuua mabeberu kwa njia yeyote.ADUI mkubwa wa Afrika ni sisi Wafrika mkuu. Mabeberu huwa wanatafuta Vibaraka na kupenyeza rupia. Wabeligiji na Wafaransa wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuivuriga Congo. Achilia mbali Wizi mkubwa wa kutisha walioufanya huko.
Ukisoma Historia utaona ni jinsi gani Belgium na France zilivyokuwa zaidi ya Maharamia katika baadhi ya Nchi za Afrika.
Watakuchosha hao.Sio maajabu bali ni namba 4, 6, na 9
Una sifa ya kuitwa ziwa basi tu maji yake yanatembeaKama una visiwa juu yake basi mto mkubwa sana
Tatizo hatuna utaratibu wa kuthamini vitu vyetu na kuweka rekodiHapo No 6 ndio pekee nakataa mana huyo Mzungu alikuta watu hapo wakiishi ...Tofauti tu hawakuwa Wazungu
Sasa maajabu yako wapi hapo wastageMTO KONGO
Afrika ni moja kati ya mabara ambalo limebarikiwa sana kuwa na vivutio vya aina mbalimbali. Moja kati ya vivutio hivyo ni Mto Kongo. Mto Kongo ni mto wa pili kwa urefu barani Afrika baada ya Mto Nile, lakini pia ni mto wa tisa kwa urefu duniani. Vyanzo vikuu vya Mto Kongo ni Milima na Nyanda za Juu za Bonde la Ufa la Afrika Mashariki (East Africa Rift Valley), Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) na Ziwa Mweru (ndio chanzo cha mto Lualaba).
MAAJABU YA MTO KONGO
- Mto wa pili kwa urefu barani Afrika baada ya Mto Nile.
- Mto wa pili duniani kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini baada ya Mto Amazon wa Amerika ya Kusini (South America).
- Mto Kongo ndio mto wenye kina kirefu zaidi duniani, unakadiriwa kuwa na kina zaidi ya 230 mita.
- Jina la Mto limetokana na ufalme wa Kongo (Ancient Congo Kingdom) wa hapo zamani, ufalme huo ulikuwepo maeneo ya karibu kuzunguka mdomo wa mto Kongo.
- Mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme (Hydroelectric plants) inakidiriwa siyo chini ya 40 ndani Mto Kongo ni mto ambao maji yake yananguvu sana kiasi kwamba unauwezo wa kutoa na kukidhi mahitaji ya umeme katika nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa).
- Katika mwaka 1482 Diego Cao ndio alikuwa Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kufika na kujionea Mto Kongo.
- Mto Kongo unakatisha katika mstari wa Ikweta (Equator) mara mbili.
- Nchi mbili za Afrika majina yake yametokana na uwepo wa Mto Kongo, ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo) na Jamhuri ya Kongo (The Republic of the Congo).
- Jina la Mto lilibadilishwa kutoka Mto Zaire na kuitwa Mto Kongo mwaka 1997 baada ya Nchi ya Zaire kubadilisha jina lake na kujiita Jamhuru ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo). The State of Zaire (1971-1997) ilipewa jina kutokana na Mto Zaire ambao hivi sasa unaitwa Mto Kongo baada ya kubadilishwa jina mwaka 1997.
- Unakadiriwa kuwa na visiwa vidogo vidogo zaida ya 4000 huku 50 kati ya hivyo vinakidiriwa kuwa na ukubwa zaidi ya (miles) 10 urefu.
View attachment 1015993
- Vyanzo (Sources) π Lake Tanganyika, Lake Mweru and Highlands and Mountains of East African Rift Valley.
- Urefu (Length) π 4700 km
- Bonde (Basin Cover) π 4,014,500 km square.
- Mdomo wa Mto (River Mouth) π Atlantic Ocean
Nile ni ndefu lakini nyembamba. Congo ni mto mpana na wenye kina kirefu zaidiKama ni mto wa pili kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini duniani na mto wa tisa kwa ukubwa duniani iweje Nile iwe kubwa kuliko mto Kongo, je huo ukubwa unatazamwa katika sura ya upana au pamoja na kina chake?
Ndio ni tofautiHebu nisaidieni swali hili jamani Congo DRC ni tofauti na Congo Brazzaville??? Na maraisi wao ni tofauti??
Sent using Jamii Forums mobile app
Nile ni mto mrefu zaidi duniani na siyo mto mkubwa zaidi duniani. Ukubwa wa mto unapimwa kwa discharge power ya maji yanayomwagwa baharini, kina na upana.Kama ni mto wa pili kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini duniani na mto wa tisa kwa ukubwa duniani iweje Nile iwe kubwa kuliko mto Kongo, je huo ukubwa unatazamwa katika sura ya upana au pamoja na kina chake?