Mtokeo ya kidato cha nne ni hujuma dhidi ya shule za kata.

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
961
Reaction score
533
Serikali imefanya jitihada kubwa ya kuanzisha shule za sekondari za kata nchi nzima ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi vijana wanapata fursa ya kusoma ili taifa liwe na wasomi wengi hatimaye liweze kupiga hatua za haraka za maendeleo.

Lakini kwa bahati mbaya sana kuna hujuma ya dhahiri zinazofanyika ili kuzihujumu shule hizi.Nadhani kwa wenye akili wataweza kuibaini hili.Wahusika wakuu ni baraza la mitihani kwa kutokuwa na gradi maalum ya viwango vya ufaulu.

Naiomba serikali ilichunguze mwenendo wa hili baraza la taifa linaangamiza taifa,kuna mchezo wa kukomoana hapa.Ufeliji huu ni aibu kwa serikali.Kwenye hii tume iliyoundwa na Pinda ikigundua kuna watu wanacheza na maisha ya vijana wetu kupitia elimu wanyongwe tu,hawa ni wahujumu nchi.
 


Kaka naona hujui unachoongea.NECTA kutoa mtihani wa aina moja kupima mtaala wa aina moja unaofundishwa katika shule zote za taifa hili. Huwezi kuwa na aina tofauti za utahini baina ya shule na shule kwa kuwa huwezi kuwa na vyeti vyenye thamani tofauti baina ya shule na shule. Hivyo, ni wajibu wa serikali kuimarisha miundombinu ya shule zote, vifaa na walimu wa kutosha ili vijana wetu kwenye shule za kata wasome ipasavyo, period!!
 
Mtoa hoja mwenyewe anajiita "kichwa mbovu", nadhani hamna haja ya kuendelea na hii mada--jamaa anajijua!
 
Mtoa hoja mwenyewe anajiita "kichwa mbovu", nadhani hamna haja ya kuendelea na hii mada--jamaa anajijua!
Ni vema kujadili hoja iliyowekwa jamvini siyo kuwa na hatred attacks kwa mtoa mada. NECTA tunafahamu kuna matatizo, anayepinga...basi anahusika nao na kufaidia na mfumo uliopo nECTA. tunajua mbinu wanzozitumia private schools mpaka zinafaulisha sana! Wanaiba mtihani (Hii SIYO SIRI) from the Corrupted NECTA under Dr Ndalichako. Tuongelee matatizo sio tufunike kombe mwanaharamu apite.
Wanafunzi wanaongia vyuo vikuu mostly walifaulu vizuri na grade za juu huku O'level na A'level lakini ni mambo ya aibu unakuta wanafunzi hawawezi hata kuandika kingereza kinachoeleweka. Mtu hujiuliza hawa walifaulu vizuri...kwa nini hawawezi kuandika kingereza? Pitapita zetu...tumebaini kuwa kuna wizi mwingi sana wa mitihani unaofanya na most of these private school(organized). Yaani hawa huchanga pesa nyingi kila wakati wa mitihani na kwenda kuchukua mitihani pale NECTA, ndo maana shule nyingi za aina hiyo wanatoka na ufaulu mzuri lakini substance hakuna. HUTAKI KUAMIN HILI UNAACHA.. kwa hiyo tujadili matatizo. mtoa hoja anasema hii ni hujuma ya shule za kata... I can support that with some of the current evidences we have in our database! Hivi juzi Green Acres wanasema kunamwanafuzi hakufanya mtihani lakini ana div 3(pt 24) na ana number ya kufanyia mtihani.... imekuwaje.. kwani NECTA wasijibu tumuma hiyo? Tujadili hoja na sio kufumbia macho matatizo! Namna hii tunaweza pata ufumbuzi wa matatizo ya nchi hii .....
 
Kinyumbe chake ndio ukweli.
Na hii ni kwa nia ya kuficha Aibu ya shule za kata, na ukimuuliza kawambwa atakuambia mbona hata Seminary na shule binafsi wamefeli?
Hii yote ni katika kuonyesha kuwa tatizo sio shule za kata tu lakini hata huko private kwenye walimu bora na vifaa hakuna tofauti na kata kusiko na walimu wala library au maabara.

Na ukitaka kujiuliza basi shangaa hili la kuwa mpaka sasa walimu wengi wakuu wanataka mitihani isahihishwe upya na hoja yao inatokana na kwamba kuna wanafunzi karibia 10 mpaka sasa wamwefaulu lakini hawakufanya mitihani, je wamefaulu vipi hawa? Kama sio baraza wamepika matokeo?
 
::
Mlitaka NECTA itoe matokeo ya kuwafurahisha wakati wote,,huko ni taaluma sio siasa.
Daktari mzuri haogopi kukuchoma sindano japo utaumia ila upone.Sio kufaulisha tu ifike mahali tuwe na Taifa la Mabwege
=
 


Mkuu kwani walifeli ni kutoka shule za Kata pekee? Je shule za Private ambazo nazo wameangukia pua inakuwaje hapo?
 

Kiongozi, kwa mtazamo wako tatizo ni watunga mitihani na wasahihishaji. huko mashuleni kuko shwari? Tatizo ni mfumo mzima wa elimu na siyo vipandevipande. Mnafikiri leo hii Dr. Ndalichako akiondolewa ndoo mambo yatakuwa shawari la hasha. Serikali inapobabaika hata kuonesha mtaala. Tatizo ni kubwa hata pa kuanzia hapajulikani labda kuunda tume ya kitaalam ya kuchunguza mfumo mzima na sio vipandevipande
 

SHULE = MADARASA + MDAWATI NA MAKABATI + WALIMU BORA + MAABARA + MAKTABA + VIWANJA VYA MICHEZO + NYUMBA ZA WALIMU. Sasa kabla ya kuishambulia NECTA angalia ni shule ngapi zimekidhi kuwa na hayo mahitaji ambayo Wizara ya Elimu inatakiwa ihakikishe yanakuwepo kabla shule haijasajiliwa.
 
Inasemekana wanafunzi walifelishwa makusudi ili kupunguza kero ya mikopo kwa wanaoingia Vyuo Vikuu.
 
Ndugu rejea hoja za ule mgomo wa walimu, pia tafuta muda uzitembelee hizo shule za kata usisubiri tume ya pinda ikujibu, pia hata afisa elimu wa mkoa hana mitaala ya elimu unategemea nini, kwa mtu yeyote ambaye ni muungwana hawezi shangaa haya maotokeo hata mara moja, ila yangekuwa tofauti mimi ningekuwa miongoni mwa watu wakushangaa tena. Leo unakuta mwanafunzi hajibu kitu au anaandika mashairi ya mapenzi unataka NECTA wafanye nini mkuu
 
Inasemekana wanafunzi walifelishwa makusudi ili kupunguza kero ya mikopo kwa wanaoingia Vyuo Vikuu.
Usiwe mwepesi wa kuamini kila kitu mkuu vitu vingine vikowazi kabisa kama kweli unaifutilia elimu yetu kwa sasa, inamaana iliwaambia wasijibu maswali au wachore katuni?
 
Hivi hadi zanaki na azania ni shule za kataeee
maana mimi sioni tofauti..........................
 

Kama kuna wanaoihujumu elimu basi ni serikali kupitia raisi aliyewapa wizara watu wasioiweza hata chembe
 
Mi ninajiuliza swali 1 tu ambalo mpaka sasa halijajibiwa, Inakuwaje mwanafunzi hajafanya mtihani kabisa na alifukuzwa shule na hata siku ya mtihan no# yake ya mtihan ilikuwa wazi lakin baada ya matokeo kutoka unakuta mtu huyo akapata matokeo tnea mzauri tu amefahulu kwa div 3-24 tena na comb imebalance ?

Nisaidien kujibu swali hilo tu alafu nyie wote mnaoitetea NECTA ndio muendelee na hoja zenu mfu.
 

Tanzania wivu ndo unatusumbua kusema private schools znaiba mitihan tayar ushageneralize zote na binafsi nimemalizia private na huo mtihan unaoibiwa cjauona!Kama umeshafanya utafiti ni bora ukaenda Necta ukawapa hiyo ripoti yako na co kulalamikia vitu vya kuhisi.
 

me nadhan necta wameelezea vizur tu kama hujawaelewa tatizo ni lako
 
::
Mlitaka NECTA itoe matokeo ya kuwafurahisha wakati wote,,huko ni taaluma sio siasa.
Daktari mzuri haogopi kukuchoma sindano japo utaumia ila upone.Sio kufaulisha tu ifike mahali tuwe na Taifa la Mabwege
=

mtihani wowote ule lazima ugawanywe katika mfumo ambao kitaalamu unaitwa table of specification (KCAASE). kwa kifupi lazima kuwe na maswali mepesi sana (1/4), maswali ya kati ambayo siyo magumu sana wa rahisi sana (1/2) na maswali mengine magumu sana (1/4). maswali magumu sana yatajibiwa kwa usahihi na watoto wenye akili sana na wanaojituma katika masomo. lengo la mtihani siyo maswali yawe magumu yote ili kuwafelishs watoto. wanaosema pana uwezekano maswali ni magumu sana ili wanafunzi waliopo ktk shule za kata wafeli, wanaweza kuwa sahihi. japo za binafsi zimefelisha lkn siyo kwa kiwango kikubwa sn.

sababu za watoto kufeli kwa asilimia kubwa ni nyingi lkn maswali magumu nadhani ni moja wapo
 
Wakati mwingine ni bora ukabaki msomaji wa thread za wengine kuliko na wewe kutaka uonekane umeanzisha thread ya kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…