Mtoni kwa Azizi Ally; Brazil ndogo iliyojaa vipaji

Huyo ally mzuri ndo yule aliyekuwa anacheza na zuchu nyimbo ya cheche ila sio video halisi ya nyimbo?

Nilionaga zuchu kamtag ally mzuri kwenye clip hiyo anambambia zuchu. Je ndo huyo?
yah ndio huyo ni dance mzuri sana kipaji kutoka azizi ally
 
Brazil? Utakua huijui Brazil
brazil kiufupi ni ichi kutoka bara la america ya kusini inajulikana sana ulimwenguni kwa vipaji lukuki vya mpira wa miguu na ndio mabingwa waliochukua komba la dunia mara nyingi kuliko nchi yoyote ulimwenguni na baadhi ya wanasoka nguli ndani ya brazil ni
1;KING PELE
2;RONALDO DE LIMA
3;RONALDINHO GAUCHO
4;GARINCHA
5;KAKA
6;RIVALDO nilikua namuhusudu sana huyu jamaa
na wengine kibao mpaka sasa kizazi hiki cha kina
NEYMAH JR, VINICIOUS JR,RODRIGO
na wengine lukuki
 
NIMESOMA MTONI KWA MAMA MARY 1989-95. Enzi za mwl baraka alikuwa kilema au ana mguu bandia. Mwl mkuu mchera. Tukicheza mpira wa kitenesi bwaloni. Shule binafsi, lkn darasa la kwanza na la pili, tulikuwa tunakunywa chai ya bure ya shule. Nimesoma na jamaa zangu wakina masudi, (alikuwa mweupe kaenda hewani, mwili nyumba) dada yake sijui anaitwa tatu kama sijamsahau sawasawa. Mashauri omari, feruzi, shimbi, antoni kagwa. Hawa mnondwa, salumu mohamedi. Lintu na devis watoto wa maghorofani bank club. Ramadhani, amekuwa mteja namuonaga anapiga debe stendi ya kwenda mjini. Mwanangu enoki mndolwa, na dada yake rozi mndolwa. Temeke kota. God alikuwa anakaa mtaa wa mkuranga b, juma kumba kumba. Bashiri. Joji mtoto wa mwalimu mama joji. Huyu mwalimu alikuwa anatuuzia pipi za tofi sh 5. Au unakopeshwa kwa lazima. Fimbo zake zilikuwa zinauma balaa. Tobiasi matiasi. Selemani sefu, huyu jamaa mapumziko ya saa 6 anatoka shule anaenda msikitini, halaf saa 7:15 anarudi darasani. Walikuwa na hoteli inaitwa kichangani pale kituoni mtongani. Hassani mgaza. Wilyam nyambwa. Sasa hv ni askari. Levokatus daudi. Mwanangu eliasi mtoto yatima kule kurasini nyumba za yatima. Athumani halifa mtoto wa tmk veterinary. Mwalami na saidi mbotoni. Masista fulani wakuitwa hadija na pili. Nilikuwa naishi tmk mwisho mtaa himo. Jirani na Pile bar mtaa wa mji mwema na kitomondo na bulyaga. Kitomondo hotel timu za soka zilikuwa zinakuja hapo. Watoto tunabeba mabegi ya wachezaji na kuenda nao taifa. Nikikosa mabegi ya wachezaji, natafuta kilema mwenye baiskel, namsukuma kuingia naye uwanjani. Nikimkosa kilema naruka ukuta kule taifa b. Au nasubiri fungulia mbwa. Natega shule a k a beira, napanda uda au icarusi, naenda feri kupaa samaki. Nachimba shimo halaf nalikalia. Mwenye samaki akijipindua natumbukiza samaki kwny shimo nafukia. Baadae nawauza. Timu yetu pale mtaani ikiitwa leads united. Wachezaji wenzangu wakina rama, haji, saidi mabuga, nuhu, hamza, alex, sekela, maulidi, mafulu, mwechiwa na kaka yake sijui anaitwa hasani, alikuwa hana miguu kamilifu, anatembelea mikono na miguu yake midogo tu imeishia mapajani. Tulikuwa na nyumba pale ilipo stendi ya kwa azizi ali kwenda mbagala, sasa hivi. Ilikuwa na bekali ya wasomali. Kwa mzee LUHIZO. Sasa hv imevunjwa kupisha upanuzi wa barabara. Tuliwahi kuishi mtongani mtaa wa mashine ya barafu. Nyumba ya mzigua sharifu jirani na familia ya mzee mkomwa. Baba mdogo NURU MKOMWA, mfalme katika biashara ya mafuta, mwili nyumba, white kaenda hewani. Timu ya mtongani wapinzani wao sifa politan. Upinzani wake simba na yanga wanasubiri. Temeke mwisho wapinzani wetu tandika mabatini. Hizo timu ni kama paraguay na uruguay. Mechi zetu zilikuwa haziishi. Mtoni kichangani tuna mji wetu, jirani na nyumba ilipoanzishwa band ya mchiriku TOPAZ. Nimesoma madrasa pale kwa jaalina, karibu na majaribio bar. Achana na mtoni kwa kindande kwa mwanangu fulani msela mavi MUSA A K A MUSCO. Sijui bd yupo hai? Baba alikuwa na genge mbagala zakhem, namkumbuka braza minyato, mzee bedui. Timu ya hapo zakhem fc, kama nipo sawa ndipo ilipozaliwa mbagala market. Wapinzani wetu watoto wa rangi 3 au kizuiani. Kwa tanzania nzima TEMEKE ndiyo chuo cha soka. Ndimu inayopigwa TEMEKE ni burudani tosha.
 
habarini wanajamvi ,naanza kwa salaam nyote humu naimani mpo njema.

Katika majina yaliotajwa ya wazee waliosaidia ukombozi wa nchi hii basi jina AZIZI ALLY utolikosa kwa mchango mkubwa walioleta kulikomboa Taifa letu pedwa.

Basi mimi ni mzaliwa wa TEMEKE sehemu iliyojaa waswahili wa kila aina makabila mbalimbali bila kusahau utofauti wa dini mbalimbali moja ya kata ya TEMEKE kuna mtoni kwa azizi ally sehemu aliyoishi mkombozi huyo mwenye historia kubwa hapa kuna nyumba nyingi zilizofungamana tunaita uswahilini ama kwa hakika ni uswahilini kweli kila aina ya biashara utaikuta na kila aina ya watu utawakuta ,vituko ,wizi, michezo na elimu bila kusahau burudani mbalimbali.

Ama kwa hakika mtoni kwa azizi ally ni mzuri leo nitaongelea michezo mbalimbali haswa mchezo pedwa uku ni mpira wa miguu ambapo tangu miaka ya 90 kumukua na wimbi la vipaji katika kiwanja cha SIFA AU UWANJA WA SIFA MTONI hapa kuna magwiji wa soka wengi waliopo ligi kuu tangu miaka hiyo pamoja na vipaji lukuki mpaka kuitwa brazil ndogo aisee hapa tumekosa mwendelezo tu lakini si vipaji mpira unapigwa hasa

Kuna miaka kulikua na taasisi ya EMIMA ambayo ilichukua vipaji mpaka kupeleka ulaya na uko vilifanya maajabu makubwa sana japo taasisi baadae ilipotea jamani mtoni imebalikiwa sana vipaji vya mpira wa miguu kuna magwiji wengi sana bila kusahau mtoni kuna vipaji vingine kama vile ;

1- MPIRA WA MIGUU

2-MUSIC

3-DANCE

4-KUIGIZA

5-SIASA
NK
KARIBUNI MTONI KWA AZIZI ALLY
Ongeza na Vibaka
 
Kumbe ni mtoni kwa azizi ally wewe ushawahi kufika kidimbwi??ukaone watu walivyo na kipaji cha kuchezea chupa??
 
NIMESOMA MTONI KWA MAMA MARY 1989-95. Enzi za mwl baraka alikuwa kilema au ana mguu bandia. Mwl mkuu mchera. Tukicheza mpira wa kitenesi bwaloni. Shule binafsi, lkn darasa la kwanza na la pili, tulikuwa tunakunywa chai ya bure ya shule. Nimesoma na jamaa zangu wakina masudi, (alikuwa mweupe kaenda hewani, mwili nyumba) dada yake sijui anaitwa tatu kama sijamsahau sawasawa. Mashauri omari, feruzi, shimbi, antoni kagwa. Hawa mnondwa, salumu mohamedi. Lintu na devis watoto wa maghorofani bank club. Ramadhani, amekuwa mteja namuonaga anapiga debe stendi ya kwenda mjini. Mwanangu enoki mndolwa, na dada yake rozi mndolwa. Temeke kota. God alikuwa anakaa mtaa wa mkuranga b, juma kumba kumba. Bashiri. Joji mtoto wa mwalimu mama joji. Huyu mwalimu alikuwa anatuuzia pipi za tofi sh 5. Au unakopeshwa kwa lazima. Fimbo zake zilikuwa zinauma balaa. Tobiasi matiasi. Selemani sefu, huyu jamaa mapumziko ya saa 6 anatoka shule anaenda msikitini, halaf saa 7:15 anarudi darasani. Walikuwa na hoteli inaitwa kichangani pale kituoni mtongani. Hassani mgaza. Wilyam nyambwa. Sasa hv ni askari. Levokatus daudi. Mwanangu eliasi mtoto yatima kule kurasini nyumba za yatima. Athumani halifa mtoto wa tmk veterinary. Mwalami na saidi mbotoni. Masista fulani wakuitwa hadija na pili. Nilikuwa naishi tmk mwisho mtaa himo. Jirani na Pile bar mtaa wa mji mwema na kitomondo na bulyaga. Kitomondo hotel timu za soka zilikuwa zinakuja hapo. Watoto tunabeba mabegi ya wachezaji na kuenda nao taifa. Nikikosa mabegi ya wachezaji, natafuta kilema mwenye baiskel, namsukuma kuingia naye uwanjani. Nikimkosa kilema naruka ukuta kule taifa b. Au nasubiri fungulia mbwa. Natega shule a k a beira, napanda uda au icarusi, naenda feri kupaa samaki. Nachimba shimo halaf nalikalia. Mwenye samaki akijipindua natumbukiza samaki kwny shimo nafukia. Baadae nawauza. Timu yetu pale mtaani ikiitwa leads united. Wachezaji wenzangu wakina rama, haji, saidi mabuga, nuhu, hamza, alex, sekela, maulidi, mafulu, mwechiwa na kaka yake sijui anaitwa hasani, alikuwa hana miguu kamilifu, anatembelea mikono na miguu yake midogo tu imeishia mapajani. Tulikuwa na nyumba pale ilipo stendi ya kwa azizi ali kwenda mbagala, sasa hivi. Ilikuwa na bekali ya wasomali. Kwa mzee LUHIZO. Sasa hv imevunjwa kupisha upanuzi wa barabara. Tuliwahi kuishi mtongani mtaa wa mashine ya barafu. Nyumba ya mzigua sharifu jirani na familia ya mzee mkomwa. Baba mdogo NURU MKOMWA, mfalme katika biashara ya mafuta, mwili nyumba, white kaenda hewani. Timu ya mtongani wapinzani wao sifa politan. Upinzani wake simba na yanga wanasubiri. Temeke mwisho wapinzani wetu tandika mabatini. Hizo timu ni kama paraguay na uruguay. Mechi zetu zilikuwa haziishi. Mtoni kichangani tuna mji wetu, jirani na nyumba ilipoanzishwa band ya mchiriku TOPAZ. Nimesoma madrasa pale kwa jaalina, karibu na majaribio bar. Achana na mtoni kwa kindande kwa mwanangu fulani msela mavi MUSA A K A MUSCO. Sijui bd yupo hai? Baba alikuwa na genge mbagala zakhem, namkumbuka braza minyato, mzee bedui. Timu ya hapo zakhem fc, kama nipo sawa ndipo ilipozaliwa mbagala market. Wapinzani wetu watoto wa rangi 3 au kizuiani. Kwa tanzania nzima TEMEKE ndiyo chuo cha soka. Ndimu inayopigwa TEMEKE ni burudani tosha.
nakubaliana na wewe mkuu TEMEKE chuo cha soka na vipaji lukuki
 
Back
Top Bottom