Mtori special kwa Aspirini

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mahitaji:
  • Nyama ya ng'ombe
  • Ndizi mbichi
  • Kitunguu maji
  • Mafuta ya kupikia
  • Blue band / Tanbond
  • Chumvi kiasi
Namna ya Kupika
  • Katakata nyama na kisha iweke kwenye sufuria yenye maji kidogo na chumvi kiasi
  • Chemsha nyama mpaka iive
  • Epua nyama yako na uiweke pembeni

    • Menya maganda ya ndizi
    • Katakata ndizi katika vipande vidogo kisha vioshe
    • Weka ndizi kwenye sufuria lenye maji kiasi na chumvi
    • Katakata vitunguu maji na viongeze kwenye sufuria lenye ndizi

  • Chemsha ndizi
  • Mara kwa mara geuza ndizi na mwiko ili kuhakikisha zote zinaiva.
  • Epua ndizi zako, na kisha punguza maji uliyochemshia kwenye chombo safi
  • Pondaponda ndizi huku ukiongeza maji uliyoyatenga ili kulainisha mchanganyiko
  • Ongeza margarine
  • huku ukiendelea kuponda



  • Ndizi zinapokua laini kabisa weka nyama uliyochemsha kwenye mchanganyiko wa ndizi
  • Ongeza maji uliyochemshia nyama na koroga mpaka mchanganyiko huo uchanganyike vyema


Asprin karibu mume wangu.
 
Hadi nimeona wivu.[emoji134]
Kule kwetu ndo msosi wetu wa asili huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…