Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mahitaji:
Asprin karibu mume wangu.
- Nyama ya ng'ombe
- Ndizi mbichi
- Kitunguu maji
- Mafuta ya kupikia
- Blue band / Tanbond
- Chumvi kiasi
- Katakata nyama na kisha iweke kwenye sufuria yenye maji kidogo na chumvi kiasi
- Chemsha nyama mpaka iive
- Epua nyama yako na uiweke pembeni
-
- Menya maganda ya ndizi
- Katakata ndizi katika vipande vidogo kisha vioshe
- Weka ndizi kwenye sufuria lenye maji kiasi na chumvi
- Katakata vitunguu maji na viongeze kwenye sufuria lenye ndizi
- Chemsha ndizi
- Mara kwa mara geuza ndizi na mwiko ili kuhakikisha zote zinaiva.
- Epua ndizi zako, na kisha punguza maji uliyochemshia kwenye chombo safi
- Pondaponda ndizi huku ukiongeza maji uliyoyatenga ili kulainisha mchanganyiko
- Ongeza margarine
- huku ukiendelea kuponda
- Ndizi zinapokua laini kabisa weka nyama uliyochemsha kwenye mchanganyiko wa ndizi
- Ongeza maji uliyochemshia nyama na koroga mpaka mchanganyiko huo uchanganyike vyema
Asprin karibu mume wangu.