Mtori wanazi

Mtori wanazi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Mtori ni moja ya vyakula ambavyo nafurahia sana kula ninapokwenda kijijini kumsalimia bibi yangu kule uchagani.

Naamini wote tunajua kua mtori ni moja ya vyakula vya asili vya wachaga,kwakawaida wachaga hupika mtori kwa kutumia ndizi na nyama tu pasipo kuongeza vionjo vingine, wao hupika na nyama nyingi sana na sehemu ya nyama hiyo lazima iwe nyama yenye mafuta mengi.
Mtori wa nazi

Tofauti na Mtori unaopikwa kiasili,mtori huu wa nazi nimeupa vionjo mbalimbali ili kupata ladha mpya na virutubisho vingi.


Mahitaji


  • Ndizi mbichi 5 (tumia ndizi bukoba)
  • Nyama ya ng'ombe ½ Kilo (
  • Vitunguu maji 2
  • Karoti 1kubwa
  • Nazi 1 (Nazi ya azam au nazi yaunga)
  • Blue banda kijiko 1 cha chai
  • Chumvi kwa ladha upendayo

Si lazima kutumia vipimo hivi,kua huru kukadiria vipimo kutokana na kiasi cha mtori unaotaka kupika.


Njia


1.chemsha nyama adi ikaribie kuiva ,iwe na supu nyingi.


2.Katika sufuria lingine,weka ndizi ,vitunguu na karoti.kisha mimina nyama juu yake na supu yote.chemsha adi ndizi ziive nakua laini,pia zibaki na supu kiasi


  • Pika ndizi kwenye moto wa wastani ili ziive nakulainika haraka,moto mkali utaunguza ndizi na hazitaiva haraka
  • Kama supu ya nyama nikidogo ongeza maji kiasi ili kuivisha ndizi na nyama

3.Zikiiva,toa nyama yote kwenye sufuria kisha weka pembeni.Acha ndizi zipoe kidogo



4.katika jagi lakusaigia matunda (blender) weka ndizi na supu yake kisha ongeza nazi na usage kwa pamoja adi uwe mtori laini


  • Badala yakusaga mtori kwenye blender unaweza kupika kiasili kwa kupekecha mtori kwa kutumia pekecho kama unalo.

5.Weka mtori kwenye sufuria kisha weka nyama,blue band na chumvi, bandika jikoni ,chemsha k kwa muda mfupi katika moto wa wastani uku ukikoroga.Mpaka hapo mtori tayari


  • Mtori ukiwa mzito sana ongeza supu iliyobaki au maji adi kupata uzito upendao

KILA KIONJO UONGEZACHO HUKIPA CHAKULA LADHA MPYA
 
Hebu nipikie kaka angu nije kula naskia tu mtori mtori sijui mlenda walau na mie nile

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom