Mtoto (6) mwingine aliyepotea juzi, amekutwa kafariki kwenye jumba bovu. Je, ni kwanini Rais asitangaze hali ya hatari (State of emegency)

Tanzania si nchi ya kuoneana huruma Tena....usiongee kilaini hivyo Kama vile hujasoma alichoandika
Nimesoma alichoandika lakini hicho nilichoandika sio kuoneana huruma bali ni Uwajibikaji. Aliitegemea Polisi tu? Kwa nini yeye binafsi hajasema alifanya nini (kujiongeza) hadi siku tatu zimepita na hatimaye ndo imekuwa hivyo?
Hatuongei kilaini-laini ila mzazi naye aseme yaliyojiri kwa upande wake.
 
Sawa mkuu
 
Haya mambo ya kupotea kufa na kutolewa viungo vya mwili mbona yanaongezeka sana kila siku?

Kwanini?
 
Ndugu ni kweli unaweza kusema wazazi kuna uzembe wanafanya kwenye kufanya maauzi ya wapi watoto wao wacheze na waende
Lakini unakumbuka yule mtoto albino ilikuwaje?, ukiachana na wazazi kutokuwa na umakini kwenye malezi ya watoto wao sasa ivi janga la watoto kutekwa limekuwa kwa kasi sana jambo ambalo limefanya watu kuongeza umakini kwenye malezi
NOTE:kwenye malezi ya watoto tunahitaji MUNGU atusaidie tu
maana jamii zinazotuzunguka zimeharibika mnoo...
 
Yule mtoto Albino, unafahamu kwamba mama yake alikabwa na kuporwa mtoto wake kinguvu?
 
Haya mambo ya kupotea kufa na kutolewa viungo vya mwili mbona yanaongezeka sana kila siku?

Kwanini?
Zinaweza kuwepo sababu nyingi zikiwemo:-
1. Husda baina ya familia -kwa chuki kubwa na ukatili wa kisasi, mtoto anadhulumiwa uhai wake kama adhabu mojawapo kwa hiyo familia halafu wahusika wanapoteza malengo kwa kunyofoa viungo ili ionekane ni Ushirikina kumbe sivyo.
2. Imani za kishirikina.
3. Ubakaji na Ulawiti - mtoto anakufa kwa kukosa hewa (suffocation) kutokana na kufumbwa pua na mdomo ili asipige kelele. Akifa, wahusika wanapoteza ushahidi ionekane vingine.
4. Madawa ya kulevya esp. bhangi.
 
Hivi sio huu uchaguzi kweli?! Imani za kishenzy!!!
 
Yule mtoto Albino, unafahamu kwamba mama yake alikabwa na kuporwa mtoto wake kinguvu?
Hilo la mtoto kunyakuliwa mikononi kwa mzazi, hiyo sifahamu. Lakini kwa Albino naamini mara nyingi huo ni Ushirikina wa kutafuta Utajiri. Hapo ujue Mganga wa kienyeji anahusika.
 
Omba lisikukute, haya mambo ya kupotea watoto unaweza Dhani watu (wazazi) ni wazembe sanaaa, mtoto anakuja kupotea kwenye mazingira ambayo Wala hukutegemea kabisa, ww hujui kumbe Kuna mtu au watu wanakulia mingo tu almost wiki Hadi mwezi...vijana mtaani wamejikatia tamaa, kazi za maana hawana wanaona Kuna watu wanatumbua tu, wakiangalia social media wenzao wako vizuri mwisho anaingiwa na roho mbaya ya ubakaji, ulawiti na mauaji ya makundi na ubaya ni kwamba AKILI ILISHAHARIBIKA hivyo njia ya kumnasua haipo. Hili ni janga kubwa mnooooo.

Ogopa sana njaa + ukosefu wa akili timamu.
 
Serikali ya CCM na policcm huwezi kuwaona kwenye matukio kama haya ila kwenye mikusanyiko ya Chadema hakuna Kiongozi wa polisi ambaye hatoonekana kwenye kuwathibiti.
 
Umaskini ni laana, mtu maskini ni mzigo kwa taifa.
 
Hayo yote uliotaja yapo tunayafahamu
swali kwanini yanaongezeka kwa kasi?

Halafu bangi fafanua inahusike hapo?.
 
Serikali ya CCM na policcm huwezi kuwaona kwenye matukio kama haya ila kwenye mikusanyiko ya Chadema hakuna Kiongozi wa polisi ambaye hatoonekana kwenye kuwathibiti.
Hii imekaa mno kisiasa aisee kwani lililo mbele yetu ni Suala la kudhulumiwa Uhai mtoto mdogo 6 yrs. Anyway, sikupingi kwani huo ni mtazamo wako na ninauheshimu.
 
Hii imekaa mno kisiasa aisee kwani lililo mbele yetu ni Suala la kudhulumiwa Uhai mtoto mdogo 6 yrs. Anyway, sikupingi kwani huo ni mtazamo wako na ninauheshimu.
Huelewa wako ni mdogo pole sana unachotakiwa kujua ni kwamba wanaotakiwa kuwajibika hapo ni polisi kwa kuwatafuta wauaji ila Cha kusikitisha ni kwamba uwezo huo hawana wao wanachoweza ni kukimbizana na wafuasi wa chadema tu, Kuna matukio tele ya watoto kutekwa na ya watu wengine kuteswa mpaka kufa ila serikali ya CCM inakuambia hizo habari zinakuzwa haziko ktk uhalisia sasa usichofahamu ni kipi hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…