Mtoto afariki dunia baada ya kugongeshwa kichwa kwenye gogo na mtu anayesadikiwa kuwa ni mgonjwa wa akili

Mtoto afariki dunia baada ya kugongeshwa kichwa kwenye gogo na mtu anayesadikiwa kuwa ni mgonjwa wa akili

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
MTOTO Agnes Kiraba (3), mkazi wa Kijiji cha Mtakuja Kata ya Kirado wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini baada ya kugongeshwa kichwa kwenye gogo na mtu anayesadikiwa kuwa ni mgonjwa wa akili.

Mtoto huyo alipatwa na mauti katika Hospitali ya Wilaya ya Mkasi Januari 3, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Justine Masejo, tukio hilo lilitoke majira ya saa 1.30 za asubuhi kijijini humo.

Alisema kuwa Agnes alikuwa anacheza nje ya nyumba yao pamoja na watoto wenzake, ndipo alipopita mtu huyo na kumkamata mtoto huyo na kumgongesha kwenye gogo.

Baada ya kitendo hicho, wazazi wa Agnes walimkimbiza katika kituo cha afya Kirando kwa ajili ya matibabu, lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya hali iliyo walazimu kumpa rufani na kumpeleka katika Hospitali ya Wilaya.

Kamanda Masejo alieleza kuwa Agnes alipofikishwa katika hospitali hiyo alianza kupewa matibabu, lakini alifariki dunia muda mfupi baadaye kutokana na kulalamika maumivu makali ya kichwa.

Kamanda Masejo alisema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi, na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
 
Back
Top Bottom