Ndugu zangu na wapenzi wa nyumba hii ya MMU,
Jana nilisoma hadithi ya kusikitisha kwenye gazeti la Mwananchi. Hadithi hii kutoka Songea (Na Joyce Joliga) inaeleza kisa cha mtu na mama yake ambao wameishi pamoja kama mume na mke kwa zaidi ya miaka 10.
Mama huyo, Condranda Ngonyani (70 yrs old) alisema hivi..."Naomba mnisamehe, ila niwe mkweli, huyu mwanangu ndiye alikuwa mume wangu kwa zaidi ya miaka kumi. Ila kwa sasa namruhusu atafute mke. Mimi sitaki tenana nimeshachoka kwani umri wangu umekwenda na huyu jamaa ana nguvu sana". Ila kwa maelezo zaidi, ni kwamba alimependa sana huyo kijana wake na alikuwa anamfurahisha na kumridhisha sana kimapenzi.
Naye kijana Joseph anakiri kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama yake toka 2002 baada ya baba yao kufariki. Alisema kuwa wakati wanaanza uhusiano na mama yake alikuwa na mke. Hata hivyo, mke wake alivyofahamu mambo hayo aliachana naye ingawa hakutoa siri hiyo kwa watu wengine,
Mambo hayo yalifumuka baada ya mama mmoja aitwaye Flora Ndembo kuanika upuuzi huo hadharani. Hali hiyo ilivuta umati wa watu ambao walianza kuwazomea hadi wakaomba radhi.
Je hawa ni wazima kichwani (mentally sound)?? Kama si wazima, inawezekanaje wagonjwa wawili wakakutana kirahisi na namna hiyo? Kama kweli ni wazima, hii inawezekanaje katika hali ya kawaida?
Babu DC!!