Mtoto akikupiga chabo

Mtoto akikupiga chabo

Wana JF;

Mtoto anapozaliwa, akili yake inauwezo mkubwa wa grasp mambo ya msingi kuliko wakati wowote. Mfano kumtambua mama, harufu yake, sauti yake, mazingira yake nk.

Inasadikiwa na Wanasaikolojia kuwa mambo mengi ambayo ni basic yanaanza kujijenga katika akili ya mtoto katika umri wa hadi mwaka moja. "Controller" ya the way we think and perceive things inajengwa katika tender age na hii controller inapatikana katika front lobe ya brain ya mwanadamu. Hatimaye hii controller ndiyo inayojenga patterns za tabia ya mtu.

Wakati katika umri huyo mtoto hawezi kumwambia mtu wakati anapiga chabo, definetely kama itakuwa routine ya nyie kufanya mbele yake akiwaona, itakuja kujengeka pia akilini mwake and will grow with it . . . . then u know what will be next.
 
.....ahhh!! Kumbe mtoto wa miezi 3 hadi 6 anajua eeehhh! Mie nilijua hajui chochote....nikienda kuoga huwa naenda naye, namuweka kwenye swing na mie naendelea na mambo yangu.....kumbe huwa kananipiga chabo tu, aisee inabidi niache.
 
Miezi sita anaona achilia mbali ile kuona kwa hisia, Angalieni msiharibu mtoto. Mtoto mwenyewe hata kutembea hajatembea.....
 
Ebu kuwa specific kuhusu umri wa mwanao unaposema miezi 3-6 ina maana humjui umri wake au una maana kuwa unao wengi wenye umri kati ya miezi Mi-3 na 6!

Kama ni miezi hajui lolote, ila sijui kwanini husimwache anyonye bila bughudha! maana wakati huo mtoto mpenzi wake mkubwa ni mama tena hata akisogea mbali anastuka usingizini. Vitu vibaya kufanya mbele ya watoto wadogo siyo mapenzi bali ni kupigana na kujibisha kwa ugomvi hivi ndivyo vinamuharibu mtoto akili hata kama ni wa miezi michache! maana mtoto hujua mara moja kuwa hakuna amani na inamsumbua sana akilini mwake. Mapenzi hayana tatizo kwa watoto wadogo kuona haiwasumbui akili wanapenda pia mapenzi ndio maana utaona mtoto anapenda kukurukia, kukumbatia na hata kubusu na kushikana mikono hiyo ndio nature ya binadamu.

Mtoto kiasi anapaswa kujengwa kimapenzi, akikuona umemkumbatia mama yeye anachojifunza ni kuwa kuna amani na mapenzi roho yake ina furahi na anajengeka kiakili na mwili kwa furaha, yeye hajui hayo mambo ya tendo wala akilini mwake hayamo kabisa! Labda kama mnafanya kwa sarakasi, nderemo na vifijo hapo nilazima mumtatize kichwani mwake! Kila kitu Binadamu anajifunza kwa wazazi wake kama role-model kwa hakika ni vyema mwana tokea utotoni akijifunza mapenzi kutoka kwako kwa kuona unavyo mpenza *****, unavyomkumbatia na kumpiga busu hata kama ni mkubwa wa umri gani ajue! ila kufanya tendo lazima huache kwa watoto waliofikia miaka miwili kwenda juu maana hapo wanaanza kujua mambo na kuhoji ndipo anaweza kukuuliza baba ulikuwa unamfanya nini mama? ila kama ni busu unamwambia nilikuwa na mbusu na mpenda sana mama yenu ajue na ajifunze.
 
Jamani mtoto wa miezi 3-6 ana akili gani?????? Mtoto kama huyo bado hana akili yeyote ya kuweza kujua chochote.
We fanya tu kile unachotaka kukifanya maana huyo bado hana utambuzi wowote.
Ingelikuwa labda mtoto wa miaka 3-6 hapo noma tena sana.


Take care!!!!

...ngoja siku kana watazama, kagune na kucheka ndio utajua kana akili au la.
 
Back
Top Bottom