Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,431
Tumeanza kuona matunda ya ugatuzi wa Kenya. Kuna mama kutoka Ethiopia ambaye alishindwa kupata usaidizi wa kufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto aliyekufia tumboni mwake kwa miaka 13. Katiba mpya ilileta mfumo wa ugatuzi na hii iliiwezesha gatuzi la Mandera kujenga hospitali ya kisasa inayoweza kufanya oparesheni ya Cesarean section. Zamani kabla ya Ugatuzi kuwepo, iliwabidi wakaazi wa Mandera kuelekea maeneo mengine ya Kenya ili kufanyiwa upasuaji lakini sasa wanaweza kufanyiwa upasuaji katika gatuzi lao bila kusafiri kwingine. Sasa cha kushangaza ni kuwa hata raia wa Ethiopia pia wameanza kutiririka Kenya wakitafuta matibabu. Mama huyu kutoka Ethiopia amefanyiwa upasuaji bila bugdha.
Tazama hapa
Tazama hapa