Mtoto aliyekojolea msaafu kortini...

hivi watoto hushitakiwa pia!!!

Ndio under the Law of Child Act, lakini mfumo wako si kama unaotumika kwa watu waizima hata adhabu yake ni tofauti kabisa sana sana viboko
 
Issue kama hizi zinahitaji busara sana kudeal nazo. Sasa hawa watawala wetu hamna kitu kabisa aisee!

Yaani aliyekojolea msaafu anapandishwa kizimbani; wanaochoma magari, makanisa na mali wanadunda mitaani?
Kweli inashangaza sana. Ila ni kwa sababu huwa hawana muda wa kujipanga, ie wanalipuka tu. We have long way to go to justice!
 
Msichanganye issue, kuna mtoto mmoja wa Pemba alikojolea Msaafu siku mbili kabla ya Mbagala... Kesi yake ipo Mahakamani huko Pemba!

Huyo wa Pemba ni kijana wa miaka 23 muislam na amepelekwa mahakamani,

Source Zanzibar Leo ya Alhamisi

Kuna misikiti yoyote ilichomwa kutokana na tukio hilo ?

Muislam akikojolea Msahafu mtu mzima anapelekwa mahakamani, mtoto yuko polisi vurugu zinafanyika wapewe mtoto wajichukulie sheria mkononi

Tuvumilianeni jamani
 
Nataka kujua umri wa mtoto kwanza ndo naweza kutoa maoni yaliyonyooka
Kuna mtu hapa amesema ana miaka 14 tu. Na zaidi alikuwa anafanya experiment! Ndo kusema kundi zima waliokuwa wanabishana lazima wakatoe maelezo yao mbele ya hakimu!
 
Imagine una oga kwenye bafu la passport size akaja mtoto akachukua nguo zako pamoja na taulo,ukatoka nje uchi ukaanza kumkimbiza,nani ataonekana chizi?? Hii scenario inafanana na waislam wa mbagala walichofanya!

Hii issue ni ndogo sana tena imefanywa na mtoto ambaye yuko katika maturity age.

BUSARA NA HEKIMA ITUMIKE kwa huyu mtoto,kama busara ilivyotumika kwa waliokataa kuhesabiwa sensa ambao walivunja sheria. au busara ilivyotumika kumuachia DIBAGULA aliyekashifu wakiristo kuwa YESU SIO MUNGU, au busara ilivyotumika kumuachia kiongozi wa UAMSHO.

Busara itumike zaidi na huyo mtoto aachiwe huru la sivyo panaweza kuchimbika.
 
Sijajua wanapata nini wale wanaokashfu na kudharau imani za wengine, hili ni tatizo la kutokujitambua
 
unapokuwa mkristo automatically unakuwa mzungu kwa tabia, na pia unapokuwa Muislamu unakuwa Mwarabu kwa tabia, Kule Mbagala ilikuwa vita kati ya Mzungu na Mwarabu, Mwarabu alihisi kuwa amedhalilishwa na Mzungu.

Kwa namna tujue kuwa licha ya kuwa na imani zetu tulizorithishwa toka kwa Wazungu na Waarabu ambayo mengi ni mazuri, hatupaswi kuacha ile hali ya kuthaminiana kama Watanzania, Tujue tuu historia ya kile tulichorithishwa halafu kisitujengee chuki kati yetu, tuingie katika ugomvu usiotuhusu tuache wao wenyewe wapambane nasi tubaki na Tanzania yetu
 
kwanini tusiache Qur'an imuadhibu naturally huyu mtoto?
Nami nilikuwa nafatakari kitu kama hichohicho! Kama waislamu wangekaa kimya, mimi na wengine wengi tu tusingefahamu hiyo habari. Na pia kama ni kweli jambo alilofanya lingempatia madhara kulikuwa hakuna haja ya watu kuanza kushambulia makanisa. Reaction ya hawa wachache wenye jazba inasababisha watu baki wadhanie kwamba quran haina nguvu.
 
nakubalina na wewe, kijana ni jasili sana, anajaribu, ila iko siku atajaribu sumu ka kuramba sasa itakuwa balaaaaaa

mtoto huyu alitaka kumaliza ubishi kwamba huwezi kupata kichaa kwa kukojolea msahafu.

alitaka kuprove the null hypothesis...sioni kosa lake kwa sababu majibu tumeyapata.
 
hapa ndio utakapoona taaluma ikiingiliwa na siasa, walioingia chuoni mwaka wa1 kusoma LLB mwaka huu, wameshaanza kusoma Criminal Law, na inawezekana wameshaanza kusoma Actus Reus na Mens Rea, na kuna Latin Maxim inasema "Actus Non facit Mens Nici sit Rea" maana yake ni "mtu hata kuwa na hatia mpaka kitendo alichokifanya kiliambatana na nia Ovu" Sasa Emanueli Josephat alikuwa kwenye ubishi wa kiimani nkwamba akikojolea Qoran atakuwa Nyoka au la? hivyo hakuwa na nia yoyotu ovu.
 
haya yote ni mavuno ya pandikizi la udini ulioasisiwa na rais wakati wa uchaguzi, sijui kama hakujua hatima ya kauli hii, napia two weeks before kuna msg ilikuwa kwenye circulation kuhusu mkutano uliokuwa ukifanyika kilimanjaro hotel (wa waislam). kwa nini kuna matukio mawili yote yakihusisha kukojolewa kwa kuraan?! sio plan hii? halafu wanatumiwa watoto, maana wao reasoning capacity yao sio kubwa, hawawezi kujua mitego wakaiepuka.
swali langu tu je hao waislam wanaopanga hizo mbinu wana maana gani? wanataka vita na wakristo, kwa sababu hata reaction zinazojitokeza baada ya hayo matukio ni ya ajabu sana, wanataka kueliminate ukristo?!
mbona rais yuko kimya sana na haya matukio? ana maana gani? si aongee tu hata kwa unafiki tusikie anasemaje.. may be the ''guilty is afraid'' angesema ili tuone kuwa anajali, la sivyo ndivyo alivyoamua kuongoza. analea ugonjwa mbaya sana
 
Paulss said:
Yaani aliyekojolea msaafu anapandishwa kizimbani; wanaochoma magari, makanisa na mali wanadunda mitaani?
Mimi si mjuzi wa sheria za Tanzania ila nafikiria kuwa katika sheria zake anayefanya jambo huku akiwa provocated anaweza kuachiwa huru...jaribu kuulizia vizuri wanaojuwa sheria za Tanzania.
 
Tatizo lipo kwamba wakati vijana wale wanabishana mpaka shutuma za kuinajisi kuran, walikuwa wawili tu, ushahidi utakuwa mgumu kuthibitisha kama kweli kijana aliikojolea kuran.
 
kwanini tusiache Qur'an imuadhibu naturally huyu mtoto?

Na sio tu hivyo kiongozi, kwanini watu wazima wasitimize wajibu wao wa kulea watoto including kuwasahihisha kiustaarab pale wanapokosea? Kwa mtindo huo mbona watoto wate wataishia mahakamani?
 
Nashukuru sana kwa hii taarifa. Nilikuwa najiuliza sana huyo aliyenajisi kuran huko ZNZ ni dini gani? Wametaka kumuua? Mbona hii habari haukusikika sana, hata hapa JF haikuvuma. Kwa nn ya Mbagala imevuma sana? Nadhani haya yaliyotokea mbagala ni viashiria kwamba sasa mpasuko wa kiimani ni mkubwa sana. Na sababu ni nyepesi tu: Taifa limekosa viongozi wenye sifa, wenye uwezo wa kujenga Umoja wa kitaifa.
 

MKUU mbona unagombana na fact? "Watoto hufanya mambo ya kitoto" kwa hivyo wliocharuka nao wangelichukulia kuwa ni jambo la kitoto. Je huyo mtoto wa DINI gani?
 
Kuna swali limeulizwa na mimi nadhani linatakiwa liwe swali kuu la mjadala huu. Yule wa Pemba ambaye naye alifanya kitendo kama hiki cha kukojolea "msahafu" alisababisha misikiti kuchomwa kama haikuchomwa ni kwanini? Kwa nini yule wa Pemba tendo lake lichukuliwe kama ni tendo lake binafsi lakini tendo la mtoto huyu wa Mbagala lichukuliwe kama katumwa na watu wa dini yake?

Kwa nini yule wa Pemba hakufanyiwa kama alivyofanyiwa "mtoto wa Mbagala?" kwa nini wale wa Pemba hawakuchoma msikiti anaoswali yule bwana kwa hoja kwamba Msikiti huo umemtuma akojolee Msahafu? Huyu mtoto anafikishwa mahakamani kwa "kudhamiria" kukojolea msahafu au kwa "kushawishiwa" kukojolea Msahafu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…