Mtoto aliyepotea kwa siku 26 apatikana baada ya kuokotwa na Msamaria mwema

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bagara aliyepotea katika mlima wa Kwaraa baada ya kwenda kufanya utalii wa ndani pamoja na masomo Kwa vitendo, Mwanafunzi huyo amepatikana akiwa amedhoofika huku akiwa na majeraha ya kukwaruzwa na miti na miba.

Mtoto Joel amepatikana baada ya siku 26 licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa ambapo ziligonga mwamba na kumkabidhi Mungu kwani wazazi wa Joel walishakubaliana na mtoto wao kutokumuona tena au pengine kuupata mwili pekee lakini siku ya tarehe 9 October 2024 Kijana Joel anapatikana akiwa hai baada ya kuokotwa na msamaria mwema.

Endelea kufuatilia Clouds ili kufahamu nini kilimsibu Mtoto Joel Kufuatia kupotea mlimani kwa siku 26.

Soma Pia: Mwanafunzi Esther wa Panda Hill aliyepotea kwa siku 35 amepatikana, yadaiwa alitoroshwa na mchoma mkaa

Soka na wenzake wako wapi!?,.., mnaanza kusifia polisi wakati habari ya clouds inasema msamaria mwema!?,hivi huwa mnalipwa kwa kila thread mnayoanzisha ya kusifia!?..,
 
SIO KWELI!
Mama wa mtoto ameeleza viizuri sana hapa mtoto alivopatikana kupitia msamalia mwema.

Jeshi la polisi halijahusika katika upatikanaje wake. Huenda lilisaidia kutafuta ila halikuweza kumpata.

Sikiliza hii video hapa
 
Soka na wenzake wako wapi!?,.., mnaanza kusifia polisi wakati habari ya clouds inasema msamaria mwema!?,hivi huwa mnalipwa kwa kila thread mnayoanzisha ya kusifia!?..,
YAANI WEWE MPAKA UMUONE SOKA NDIYO UTAJUWA POLISI WANAFANYA KAZI HUYU MTOTO ALIYEPATIKANA SIYO BINADAMU? NDIYO MAANA NMNAAMBWA AKILIZENI HAZIFANYI KAZI
 
Pumbavu kabisa hapo jeshi la polisi limehusika vipi kupatika kwa huyo mtoto? Huu uchawa umekuwehusheni kabisa mumekuwa mataahira .
 
YAANI WEWE MPAKA UMUONE SOKA NDIYO UTAJUWA POLISI WANAFANYA KAZI HUYU MTOTO ALIYEPATIKANA SIYO BINADAMU? NDIYO MAANA NMNAAMBWA AKILIZENI HAZIFANYI KAZI
Nakuuliza tena kwenye taarifa umeona kuna sehemu Polisi wametajwa kusaidia kupatikana kwa mtoto!?, taarifa aliyoleta ya habariclouds inasema watu wote wakiwemo wazazi na polisi walishakubali mtoto hapatikani tena, msamaria mwema kamuokota mtoto,kwanini mnakimbilia kuwasifia polisi!?
 
YAANI WEWE MPAKA UMUONE SOKA NDIYO UTAJUWA POLISI WANAFANYA KAZI HUYU MTOTO ALIYEPATIKANA SIYO BINADAMU? NDIYO MAANA NMNAAMBWA AKILIZENI HAZIFANYI KAZI

..Polisi wamuokoe hata mpinzani mmoja, hata kama ni geresha tu.

..Na matukio dhidi ya wapinzani huwa yanafanyika ktk mazingira ambayo Polisi wakiwa na nia ya kuyachunguza lazima watapata majibu.
 
Jeshi liko kazini, limefanya lazi kubwa kumsaka mtanzania huyu ambaye alipotea, salsa amepatikana. Jeshi hili halilali

======

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bagara aliyepotea katika mlima wa Kwaraa baada ya kwenda kufanya utalii wa ndani pamoja na masomo Kwa vitendo, Mwanafunzi huyo amepatikana akiwa amedhoofika huku akiwa na majeraha ya kukwaruzwa na miti na miba.

Mtoto Joel amepatikana baada ya siku 26 licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa ambapo ziligonga mwamba na kumkabidhi Mungu kwani wazazi wa Joel walishakubaliana na mtoto wao kutokumuona tena au pengine kuupata mwili pekee lakini siku ya tarehe 9 October 2024 Kijana Joel anapatikana akiwa hai baada ya kuokotwa na msamaria mwema.

Endelea kufuatilia Clouds ili kufahamu nini kilimsibu Mtoto Joel Kufuatia kupotea mlimani kwa siku 26.
Sasa hapo kwa habari uliyonukuu, kuna sehemu Polisi wametajwa kuhusika katika upatikanaji wake?

Na kusema ' Jeshi halilali' ulimaanisha nini, yaani takribani mwezi mzima ambao mtoto aliopotea, wao hawakulala na walikesha wakifanya nini?

Pye pye pye nyingii kutaka kusahaulisha watu habari za kina Soka!

Nyie machawa wazandiki, siku moja moja muwe mnatumia akili basi mnapotoa taarifa muhimu kwa umma.
 
Back
Top Bottom